KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Tuesday, March 25, 2014

STANNA - The Best rapper from Mbeya, (News)

Add caption
Rapper mkali kwa miondoko ya Hip hop toka Mbeya na Mkali wao kama supper Nyota 2013 toka Mbeya, anaefanya vizuri zaidi saana katika Musi. Hayo yameweza dhihirika baada ya wasanii wakubwa kama Young D, Izzo B, Dully, Madee na wengine kibao kuonyesha kushtusha saana na uwezo wake kwenye gem na kumkubali pia, zaidi unaweza skiliza track iitwayo Rap, ili kujua uwezo wake zaidi. Punde anataraji tua na mzigo mpya. Hapa hapa utasomeka kama kawa.

Monday, March 24, 2014

Saturday, March 22, 2014

Friday, March 21, 2014

Sunday, March 9, 2014

MKULIMA COLLEGE - Tamthilia Toka Alama Xp Production. !!!COMMING SOON!!!

TAMTHILIA ILIO TENGENEZEA MAZINGIRA YA IRINGA INAKUJIA HIVI PUNDE TOKA ALAMA XP PRODUCTION (Dr Tenya Brown) INAFUNDISHA, INAELIMISHA, INABURUDISHA, INASISIMU NA PIA IMETAWALIWA NA UHALISIA WA MAZINGIRA YA MTANZANIA. (Mama Matha - Mafinga) Pichani.
MOJA YA LOCATION ZILIZOPO KWENYE TAMTHILIA HIO. (Dogo Scopy aka Fresh Andy Akiwa Location Pia)

TIZAMA TRAILER YA TAMTHILIA YA MKULIMA HAPA.

KOMEDI MPYA TOKA MAFINGA (Alama Xp Production) -MWAGITO

COMEDY MPYA TOKA MAFINGA IRINGA CHINI YA ALAMA XP  PRODUCTION Dr (Tenya Brown ) IITWAYO MWAGITO. BONGE MOJA COMEDY INAYOCHEKESHA NA KUFUNDISHA PIA. HIVI PUNDE ITAANZA TUA MTAANI KWA BEI PWAAA KABISAAA.

TAYARI NAKALA ZISHAANZA FOTOLEWA. ANDAA TSH 5000 TU KUPATA NAKALA YAKO. KWA MAONI USHAURI NA KUHITAJI BEI ZA JUMLA, CHUKUA NAMBA KWENYE POSTERS HAPO JUU AMA TUTUMIE HAPA selengakaduma@gmail.com

SIDE BALLO - JICHUNGE

SIDE BALLO NI ARTIST MPYA IRINGA TOWN KATIKA GEMU YA MUSIKI, AMBAE KWASASA ANADHAMINIWA NA UONGOZI WA MIALE SANAA GROUP ULIOPO CHINI YA KHAMIS NURDIN. VIDEO HII NI VIDEO ZA MWANZO KABISA KUFANYWA NA REBIRTH CORPORATION- CHINI YA KAGUSA aliekua kazoeleka kwenye Audio Production. Chungulia Video Hio taaaaam hapa.

Sunday, March 2, 2014

LONKA KUINGIA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA TUZO ZA KTMA 2014

LONKA NI ARTIST TOKA IRINGA ANAEFANYA VIZURI SAANA KATIKA TASNIA YA MUSIC DAR NA TANZANIA KWA UJUMLA. HII IMEDHIHIRIKA BAADA YA KUPATA CHANCE YA KUINGIA KWENYE NOMINATION ZA TUZO ZA KILL MUSIC AWARDS MWAKA 2014, KWA KUINGIA NA WIMBA WA HAKUNA MATATA KAMA WIMBO BORA WA RAGGAE. HIVYO MDAU UNAOMBWA SAANA SUPPORT YAKO KATIKA KUMPIGIA KURA MSANII HUYU ILI AWEZE KUTUWAKILISHA VYEMA NYANDA ZA JUU KUSINI KATIKA RAGGAE. KUMPIGIA KURA ANDIKA 04 LONKA HAKUNA MATATA THE TUMA KWENDA NAMBA 15440 KWA NJIA YA SIMU. AU WAWEZA TEMBELEA www.kilitime.co.tz/ktma

Saturday, March 1, 2014

La - Parte JIONEE MWENYEWE NIGHT CLUB BORA NYANDA ZA JUU KUSINI NA TANZANIA KWA UJUMLA.

Hii ndio Night Club Bora kwa sasa Tanzania Inayopatikana Iringa, Ambayo Imezinduliwa Rasmi tar 14/02/2014 Siku ijulikanayo kama Valentine Day. Club Hii tangu izinduliwe na Kuanza kazi Rasmi Imejizolea Umaarufu Mkubwa kutoka kwa wadau na Raia Mbalimbali.
Huu ndio Muonekano wa Nje wa club La - Parte Ambayo Ipo Chini ya Ebony Entertainment, Inayomilikiwa Na Mr Mfugale.
Hapa Ndio Lango la kuingilia ndani ya Club Hio. Twende Ndani Ukajionee mwenyewe.
Hii ndio sehemu ya kwanza na Counter ya kwanza unapoingia tu kati ya Tatu zilizomo ndani Humo. Aibu Manzeeeee.
Wakati nilipo pata nafasi ya Kuitembelea, ndipo nilipo Data na Counter hio na kuamua japo tokelezea tuu kwa mbele hata kama nlishindwa kalia vizuri sturi za humo ndani Pengine Yawezakana ilikua kuduwaa tuu.
Hii ni moja ya Kumbi zilizomo humo ndani ambayo pia Ilinidatisha kwa kua na sakafu ya Kioo kama Unapoiona hapo na yenye taa kwa Chini. Kufuru Aiseeeee, Nlibaki nimeduwaaaaa coz nimezoea kuona vioo madirishani na sio sakafuni.
Upekuzi haukuishia hapo tuu niliingia mpaka maliwatoni kujionea mwenyewe, Huku nako ilikua balaa tuu kama unavyoona, Bombazakunawa mikono hazina koki, ila ukisogeza tuu mikono zinatoa maji, na utakapotoa mikono zinakata zenyewe. TV Flat Screen Ipo pia mpaka chooni, Zaidi tembelea mwenyewe kajionee.
Baada ya hapo nlipata time ya kutembezwa kumbi nyingine ya ghorofan Ambayo ni Red Carpet.
Hapa nlikua ngazini nilielekea Ukumbi wa ghorofani ambao ni Red Carpet.
Manzee, Sikuamini machoyangu nilio yaona Huko. Kweli Ilikua Red Carpet na Kuna Kaunter nyingine pia, projector na TV Kubwa Flat screen.
Burudani pia kama kawa zipo wanapiga mpaka Live Band, Nilikutana na Drums humo humo nikaamua tokelezeaa nayo. Kuyasadiki haya Tembelea Mwenyewe kajionee na sio kusimuliwa, kama nlivyo tembelea mwenyewe. Nimeingia Club Nyingi lakini hii ni  Funiko. Shukrani Ziwaende Mmiliki wa club Ndugu Mfugale, Ebony Entertainment, Emmo Da Pro' Pamoja na Eddo Bashir kwa kuweza nifanikishia Jionea maajabu haya. Kwa maoni Ushauri karibu hapa selengakaduma@gmail.com

BIG JOFF, RASCO J, & JESSEY - TROUBLE

TOKA BATU MUSIC IRINGA, ARTIST WATATU WASIMAMA NA KUFANYA TRACK MOJA INAYOKWENDA KWA JINA LA TROUBLE, CHINI YA  PRODUCER GERALD, ARTISI HAO NI BIG JOFF, RASCO J NA JESSEY. BIG UP KWAO KWAKUA NI KAZI NZURI SAANA. WANAOMBA SUPPORT YENU KAMA WADAU. KWA MAONI ZAIDI UNAWEZA KUTUTUMIA HAPA selengakaduma@gmail.com

Friday, February 28, 2014

Saturday, February 15, 2014

NELLY BE FT MAC,CLOUDY 9,MKWAWA SILE, - LOVE

TRACK Inaitwa LOVE, na Imesimamiwa na NELLY CALOCY MSAMILLA Katika Music Industries natumia Jina La NELLY BE Pia Mimi ni Mwandaaji na Mtangazaji wa Vipindi Vya Burudani na Music Director/Music Manager NURU FM Iringa Tanzania  , Ni Wimbo Unao Husu Maswala ya Wapendanao. Ni Wimbo Ambao Unatoka Katika Mixtape na Albamu ya B.M.B..Naomba Sapoti yenu , Huu Ni Mwanzo Tu nimeanza na Upcoming Artst Track ya Pili Itahusisha Mastaa wakubwa.

Humo Ndani yupo NELLY BE FT MAC,CLOUDY 9,MKWAWA SILE, _LOVE Ni Zawadi ya VALENTINE

Saturday, February 8, 2014

Thursday, January 30, 2014

DEE GOZBA ft VEDASTO - KAMA WEWE

Dee Gozba, Artist Mchanga anae kuja kwa kasi, toka Mikoa ya nyanda za Juu Kusini, akiiwakilisha Mafinga. Akiwa kama Mdogoake na Jay Mutta anakuja, na Track iitwayo Kama Wewe, alio mshirikisha Vedasto. Kwasasa Yupo Dar es salaam Kimasomo zaidi But anaomba msaada wenu wadau kwa maoni Ushauri kwenye tasnia ya Music ili aweze fika mbali. Zaidi skiliza nyimboyake hio mpya Hapa chin

Wednesday, January 29, 2014

NAS WAKITAA FT CHIBWA - MONEY ON MA MIND

Anajulikana kama Nas Wakitaa, Huku jina lake halisi likiwa Nasibu Luvanda, Tokea Mafinga Iringa, Ingawa kwa sasa Husling anafanyia Dar, Amekuja na Traki Mpya Ijulikanayo kama MONEY ON MA MIND Ambayo kamshirikisha CHIBWA. Anaomba saana Support yako Mdau kama. Zaidi chungulia Track yake hapa.

JOVIARY FT BENADO - USINIWEKEE HILA

Joviary ni Artist Anaetokea mbaye anakuja, kwa kasi zaidi kwenye gem na nyimboyake Iitwayo USINIWEKEE HILA Chini ya Tabasam Music. Amejaliwa kua na sauti nzuri, ni mwenye kipaji kuanzia utunzi mashairi mpaka Vocal. Mtaani kaanza na kazi hii kama kaziyake ya kwanza, Na mpaka leo ana kazi nyingine Mpya inayokuja, baada ya hii, Anaomba Saana Msaada wako, wa mawazo, Maoni, Ushauri na Ikiwezekana management. Week Hii Mwishon atakua Mafinga kufanya Video ya wimbowake mwengine Mpya Kwa Ofa Maalum Kutoka Alama Xp Video Production. Unataka Jua zaidi juu ya Artist Huyu Mpya Toka Mbeya? Uscose tembelea hapa mara kwa mara Kila kitu utakipata.


Sunday, January 26, 2014

Sunday, January 5, 2014

MIKE TEE aka MNYALU KUJA NA MIKAKATI MIPYA YA KIMUZIKI 2014.

Baada ya Kimya kingi Mwana Mziki Mkongwe Wa Gem la Kusini Mike Tee, aka Mnyalu, Afunguka na Mkakati wake mpya wa Kimuziki, Hii ni baada ya kuachi nyimbo yake Mpya ujulikanao kama Uliniona Sina Maana,  alofanya na JumaNature aka Kiroboto, ambayo Imeleta Taswira Kubwa saana Na mpya katika Maskio ya walio wengi na kufanya vizuri katika media mbali mbali. Mwanamziki Huyo kaahidi kua Atakua akitoka na Traki mpya Kila ifikapo Tar 01 ya kila mwezi, na mpaka sasa asha Anza na track Mbili. Anawaomba mashabiki kumuunga mkono kwa harakati zake na pia Mtegemee mambo makubwa katika tasniya ya Muziki hasa mwaka huu 2014. Unalakusema, tutumie maoni yako hapa selengakaduma@gmail.com





HERI YA KRISMAS NA MWAKAMPYA/ PIA KUTIMIZA MWAKA 01 WA MTANDAO HUU KUWA HEWANI.

BLOG YENU YENU YA KIJANJA IMETIMIZA MWAKA MMOJA SASA RASMI TANGU ILIPO ACHIWA HEWANI, TAR 02/01/2013. SHUKRANI ZA DHATI ZIWAFIKIE  Tenya Brown, (blog launch designer and editor)  Emmo da Pro, ( blog advisor) Lusimiko Unyax Kaduma (Blog founder), Dogo Scopy (Blog advisor), James Mtalemwa (Blog Advisor), and Selenga Kaduma (Blog CEO/ Owner) Kama washauri na wahusika wakubwa kwa uwepo wa blog hii www.selengakaduma.blogspot.com , mpaka leo Inatimiza mwaka Mmoja sasa.Tunashukuru wadau kwa mani yenu na tunaomba zidi pewa maoni pale unapo huwishwa kufanya hivyo ili koboresha zaidi kwa tuyafanyayo. Karibuni.
KWANIABA YA WAENDESHA BLOG HII WOTE KAMA BLOG CEO, NAPENDA KUWATAKIA SIKUKU NJEMA YA KRISMAS NA MWAKAMPYA WADAU WOOTE WA SANAA, WANAHABARI, NDUGU, JAMAA, NA MARAFIKI. YESU AZALIWE MIOYONI MWENU UPYA, ASANTENI NYOTE.

Saturday, December 14, 2013

B ALONE ( Artist toka Njombe Mkali wa stage Nyanda za Juu Kusini, yaani Hakunaga 2013)

B ALONE MWANA MUZIKI TOKA MKOANI NJOMBE MWENYE CREW IJULIKANANAYO KAMA LUCK NUMBERS, CHINI YA DPM ENTERTAINMENT  KWA MUJIBU WA MASHABIKI NA CREW NZIMA YA BLOG HII HUYU NDIE MSANII BORA KWA KUMILIKI JUKWAA NA KUPIGA SHOW KALI. LICHA YA KUA ANA MADANSA PIA ANAJUA KUCHEZA NA KWENDA SAWA NA MADANSA WAKE ANAPOKUA JUKWAANI. PIA AMEKUA AKIPIGA SHOW LIVE, WALIO WAHI HUDHURIA SHOWZ ZAKE, WANAWEZA KUA MASHAHIDI, WAKIFANANISHA NA WASANII WENGINE WA NYANDA ZA JUU KUSINI. MFANO, SHOW YA MTIKISIKO MAKAMBAKO 2013, ALIFUNIKA NOOOMA.
PIA NDIE MWANAMUZIKI PEKEE AMBAE ANAKUBALIKA NYUMBANI YAANI KWAO NJOMBE. UKIFIKA NJOMBE NA UKAANDAA SHOW YAKO BILA B ALONE KUWEPO HUFANYI BIASHARA. HAYA NIMEWEZA YASHUHUDIA MWENYEWE. ALIPOULIZWA NAE KWANINI, AMEKIRI KUA NA MAHUSIANO MAZURI NA MASHABIKI WAKE PAMOJA NA JAMII INAYO MZUNGUKA, KUANZIA WATOTO MPAKA VIKONGWE. PIA AMEKUA HACHAGUI SHOW ZA NYUMBANI KINA ANAPO ALIKWA.
BAADHI YA WANAMUZIKI WAKONGWE KWENYE GEM WALIO KIRI KUMKUBALI B ALONE NI, MRISHO MPOTO, NURU ELY, LINA, NA WENGINE KIBAO, INGAWA TETESI ZA KITAA ZINASEMA NA MKUBWA DIAMOND, ANAMHOFIA SANA HUYU DOGO KWA UJIO WAKE STEJINI.
BAADHI YA MAVAZI ANAYO PENDELEA TUPIA HASA ANAPOKUA JUKWAANI NI KAMA YENYEMTINDO HUU.
HUYU NDIE NABII PEKEE MIKOA YA KUSINI ANAEKUBALIKA KWAO. MWAKANI ANANDOTO ZAKUFANYA MAKUBWA SANA KWENYE GEMU YA MUZIKI. PIA ANAMPENDA SAAANA MAMA YAKE MZAZI, NA WANA LUCK NUMBERS. MWISHO KABISA ANATOA SHUKURANI ZAKE ZA DHATI KWA BWANA DEO MWANYIKA KWA KUMWEZESHA KIMUZIKI MPAKA SASA ANAFAHAMIKA TANZANIA NZIMA KATIKA TASNIA YA MUZIKI, KUPITIA DPM ENTERTAINMENT. ZAIDI TEMBELEA HAPA CHINI KUTIZAMA VIDEO YA BAADHI YA SHOW ZAKE MWAKA 2013. http://youtu.be/APUAUZuLHW4  

EMMO DA PRO' FT MED C - NIPE KIDOGO ( Mwanamuziki Bora katika miondoko ya POP na Mbunifu Zaidi Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania 2013)



EMMO DA PRO' NDIE MWANAMUZIKI BORA WA MWAKA 2013 KATIKA MIONDOKO YA POP, NA PIA NDIE MWANAMUZIKI MCHANGA PEKEE TOKA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI ALIEWEZA ONEKANA ANAWEZA PAMBANA NA SOKO LAKIMATAIFA KWA UBUNIFU ZAIDI KATIKA KAZI ZAKE,NA KATIKA KUUTANGAZA MUSIC WA KIAFRIKA. HII IMEWEZA DHIHIRIKA KWA BAADHI YA NYIMBO ALIZOWEZA FANYA MWAKA HUU. NA PIA KUTO FANANA NA MWANAMUZIKI YEYOTE KATIKA STAIL ANAYO FANYA MPAKA MIDUNDO ANAYOTEMBEA NAYO AMBAYO PIA AMEKUA AKIIFANYA MWENYEWE. MFANO UNAWEZA SIKILIZA WIMBO WAKE MPYA HAPA CHINI UITWAO NIPE KIDOGO, NA UKAFANANISHA NA NYIMBO ZOTEE UZIJUAZO WEWE TOKA MIKOA YA KUSINI, UNAWEZA GUNDUA KITU. KIKUBWA ANAHITAJI SUPPORT YAKO MDAU NA USHAURI PIA ILI KUTIMIZA NDOTOZAKE ZA MUSIC NA KUKUBURUDISHA ZAIDI.