KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Saturday, March 1, 2014

La - Parte JIONEE MWENYEWE NIGHT CLUB BORA NYANDA ZA JUU KUSINI NA TANZANIA KWA UJUMLA.

Hii ndio Night Club Bora kwa sasa Tanzania Inayopatikana Iringa, Ambayo Imezinduliwa Rasmi tar 14/02/2014 Siku ijulikanayo kama Valentine Day. Club Hii tangu izinduliwe na Kuanza kazi Rasmi Imejizolea Umaarufu Mkubwa kutoka kwa wadau na Raia Mbalimbali.
Huu ndio Muonekano wa Nje wa club La - Parte Ambayo Ipo Chini ya Ebony Entertainment, Inayomilikiwa Na Mr Mfugale.
Hapa Ndio Lango la kuingilia ndani ya Club Hio. Twende Ndani Ukajionee mwenyewe.
Hii ndio sehemu ya kwanza na Counter ya kwanza unapoingia tu kati ya Tatu zilizomo ndani Humo. Aibu Manzeeeee.
Wakati nilipo pata nafasi ya Kuitembelea, ndipo nilipo Data na Counter hio na kuamua japo tokelezea tuu kwa mbele hata kama nlishindwa kalia vizuri sturi za humo ndani Pengine Yawezakana ilikua kuduwaa tuu.
Hii ni moja ya Kumbi zilizomo humo ndani ambayo pia Ilinidatisha kwa kua na sakafu ya Kioo kama Unapoiona hapo na yenye taa kwa Chini. Kufuru Aiseeeee, Nlibaki nimeduwaaaaa coz nimezoea kuona vioo madirishani na sio sakafuni.
Upekuzi haukuishia hapo tuu niliingia mpaka maliwatoni kujionea mwenyewe, Huku nako ilikua balaa tuu kama unavyoona, Bombazakunawa mikono hazina koki, ila ukisogeza tuu mikono zinatoa maji, na utakapotoa mikono zinakata zenyewe. TV Flat Screen Ipo pia mpaka chooni, Zaidi tembelea mwenyewe kajionee.
Baada ya hapo nlipata time ya kutembezwa kumbi nyingine ya ghorofan Ambayo ni Red Carpet.
Hapa nlikua ngazini nilielekea Ukumbi wa ghorofani ambao ni Red Carpet.
Manzee, Sikuamini machoyangu nilio yaona Huko. Kweli Ilikua Red Carpet na Kuna Kaunter nyingine pia, projector na TV Kubwa Flat screen.
Burudani pia kama kawa zipo wanapiga mpaka Live Band, Nilikutana na Drums humo humo nikaamua tokelezeaa nayo. Kuyasadiki haya Tembelea Mwenyewe kajionee na sio kusimuliwa, kama nlivyo tembelea mwenyewe. Nimeingia Club Nyingi lakini hii ni  Funiko. Shukrani Ziwaende Mmiliki wa club Ndugu Mfugale, Ebony Entertainment, Emmo Da Pro' Pamoja na Eddo Bashir kwa kuweza nifanikishia Jionea maajabu haya. Kwa maoni Ushauri karibu hapa selengakaduma@gmail.com

BIG JOFF, RASCO J, & JESSEY - TROUBLE

TOKA BATU MUSIC IRINGA, ARTIST WATATU WASIMAMA NA KUFANYA TRACK MOJA INAYOKWENDA KWA JINA LA TROUBLE, CHINI YA  PRODUCER GERALD, ARTISI HAO NI BIG JOFF, RASCO J NA JESSEY. BIG UP KWAO KWAKUA NI KAZI NZURI SAANA. WANAOMBA SUPPORT YENU KAMA WADAU. KWA MAONI ZAIDI UNAWEZA KUTUTUMIA HAPA selengakaduma@gmail.com