KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Friday, October 31, 2014

JCB - MTOTO MKALI (New Song from JCB Comming Soon

HIVI PUNDE MSANII JCB MAKALLA TOKA ARUSHA, ANATARAJI TUA MTAANI NA MZIGO MPYA UTAKAO KWENDA KWA JINA LA MTOTO MKALI, CHINI YA PRODUCER DAZ NALEDGE TOKA WATENGWA RECORDS. WIMBOO HUU UNAZUNGUMZIA MAPENZ. USIKAE MBALI NA UKURASA WETU PUNDE UTAKAPO ACHIWA RASMI UTAUPATA HAPA HAPA. KARIBU...

ANGEL BENARD - SHUJAA ( New Audio )


Huu ni wimbo wa pili kutoka album mpya NEW DAY kutoka kwa Angel Benard - wimbo unaitwa SHUJAA. 

SHUJAA.
Kuna wakati katika maisha tunakutana na mambo magumu na hakuna wa kukutia moyo, kwa sababu wengi waliotuzunguka ni watu ambao mara nyingi hufurahi tunapoumia. Huu ni wimbo ambao mtu unajikumbusha mwenyewe juu ya uhalisia wa maisha na kasha unajikumbusha kwamba “you are the hero of your own soul”. Mungu ametuamini na mitiani ya maisha, hivyo na sisi tunakubali kupambana na kila hali hadi kufikia ndoto zetu hata kama huko njiani kuna vikwazo.

HISIA - GIMME A CALL - (New Audio)


Mshiriki wa Tusker Project Fame HISIA anakuja na kibao chake kipya GIMME A CALL ambacho amemshirikisha producer John Blass kutoka Grand Master Records. Hisia mwenye kipaji cha vocals ameonesha uwezo wake mkubwa katika hii track iliyopo katika miondoko ya Afro Soul. Wimbo ulitambulishwa rasmi katika concert iliyoandaliwa viwanja vya Alliance Francaise akisindikizwa na Grace Matata pamoja na kundi la H_art the Band kutoka nchini Kenya. HISIA - GIMME A CALL Vocals: Hisia Drums: Nelson Martin Mugarula Bass guitar: Kelvin Samuel Guitars: Goodlucks Sway, Mzee Francis, Hisia Keys: John Blass Written by: Hisia Music consultant: BR Marungi Instruments recorded at Fnouk Music Studios Co-arranged by Kelvin Samuel Produced by: John Blass - Grand Master Records