KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Wednesday, August 27, 2014

Tuesday, August 26, 2014

Sunday, August 24, 2014

Thursday, August 21, 2014

Tuesday, August 19, 2014

Monday, August 18, 2014

Saturday, August 16, 2014

Friday, August 15, 2014

Thursday, August 14, 2014

Monday, August 11, 2014

Tuesday, August 5, 2014

NELLY BE FT CLOUDY 9, OBBY, KARIMUSIC & MKWAWA - THANK YOU ( NEW AUDIO )

Kwa Majina Yangu Naitwa Nelly Calocy Msamila ( Nelly Be) Mimi Ni Mwana Muziki wa Hip Hop, ( Rapper) na ni Mtangazaji wa Radio na Tv ..Pia na Ni Mwandaaji wa Vipindi Vya Radio….
Kwa Sasa ni Mtangazaji na Mwandaaji wa Vipindi Vya Burudani wa Radio Nuru Fm Iringa Tanzania
Kubwa zaidi Mimi Ni Mwanamuziki … Nina Wimbo Wangu Mpya Unaitwa THANK YOU Naombeni Sapoti ya Nguvu….Nafanya Muziki Kama Anavyofanya DJ KHALID, DJ DRAMA,,,
 Lakini Mimi Nipo Tofauti Nafanya Kazi na Wasanii/Rapper Ambao Wanachipukia., Amin Upcoming Atist..Ili Kuwapa Nguvu..na Sapoti.. Kwahiyo na Wewe Mdau Ukitoa Sapoti Kwangu Moja Kwa Moja Umewapa Sapoti Vijana Hawa Ambao Wamefanya au Kuimba Hii Track ya Thank You..
Rappers Wote Wanatokea Iringa na Mbeya Tusapoti Cha Nyumbani Tanzania.
Rapper Nelly Be – Thank You  Feat Nelly Be ( CLOUDY 9, OB, KARIMUSIC & MKWAWA)
Song : Thank You
1.Production Studios …; Uprise Music Producer Dupy ..( Beats Producer)
2.Production Studios….; Sampamba Music ( Vocal & Final Mixing)
Type ..; New Skull Hip Hop( Trap)
Email.. Yangu ni Nellybe4@gmail.com
Social Networks ni Twitter & Instagram ni @nellybe255 ..My Facebook Fun page  Nelly Be 255..
Nashukuru Kwa Sapoti Yenu…

Monday, August 4, 2014

RISALA NA HISTORIA FUPI YA UMMOJA WA VIJANA IRINGA KWA WAGENI WAALIKWA 03.08.2014 MAFINGA - IRINGA

RISALA NA HISTORIA FUPI YA UMMOJA WA VIJANA IRINGA KWA WAGENI WAALIKWA. 03.08.2014 MAFINGA - IRINGA Mheshimiwa mgeni mkuu wa wilaya ya mufindi evarista kalalu. Wageni waalikwa Katibu wa ccm wilaya mufindi-miraj mtaturu Afisa maendeleo ya vijana wilaya-juma fuluge Mjumbe wa halmashauri kuu ccm-marcelina mkini Kaimu meneja waa benki ya mucoba-eliter maalangalila Mshauri wa umoja huu dr yahaya Msigwa UTANGULIZI Mheshimiwa mgeni rasmi, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia afya njema nakuweza kutukutanisha leo katika sikuu hii muhimu,awali ya yote nikupongeze kwa kukubali Ombi letu la kuwa Mgeni rasmi,Tunaimani una mambo mengi yakufanya ila ukapendezwa kuungana nasi katika uzinduzi huu, kwa niaba ya vijana WEnzangu nasema Ahsante na MUNGU AKUBARIKI niwapongeze pia vijana wenzangu wote kwa ujumla kwa kukubali kuundwa kwa umoja huu ili kuwa chombo cha mabadiliko chanya hasa katika kutetea maslahi na haki za vijana,. Mheshimiwa Mgeni Rasmi,Nianze kwa historia fupi mpaka leo tupo hapa,safari yakuanzisha umoja huu ilianza miezi nane iliyopita kwa kupita wilaya zote za Mkoa wa Iringa nakukutana na vijana wenzetu na kuwaelezea lengo lakuunda umoja huu ili kutengeneza mfumo ambao ndio msingi mkuu wa kuweza kutimiza ndoto zetu. ,Mheshimiwa Mgeni rasmi tungeweza kufanya kwa uchache wetu lakini tukaona ni vema kuwashirikisha wenzetu ili tuwe na nguvu ya pamoja,tulisisitiza umoja huu ni wetu sote hakuna kizuizi chochote kinachoweza kutukwamisha kwa malengo tuliojiwekea, tuliamini kila jambo lina changamoto zake na safari yeyote haiwezi kukosa vikwazo lakini yote tumevuka na leo na leo unauzindua rasmi Umoja wetu Mheshimiwa Mgeni Rasmi,umoja una jumla ya wanachama hai 970 ndani yake kuna wanachama waanzilishi,wanachama wa mkataba,wanachama wa kujiunga na wanachama wa heshima,ndani ya umoja tumeunda makundi matano kutokana na jografia mahali husika makundi hayo ni MUZIKI,FILAM,UJASILIAMALI,KILIMO,UFUGAJI,NA MICHEZO Mheshimiwa mgeni rasmi tuna mengi yakuyafanya lakini kwa kuanza tumeamua yafuatayoyafuatayo 1-kuanzisha mfuko wa kuweka na kukopa ambao utaitwa Vijana Iringa Vicoba mfuko huu utasaidia wanachama wetu kuweza kujiendelezaa kiuchumi. Na kuweza kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo 2-kuanzisha mfuko wa dharula aambao utakuwa wakusaidiana katika shida na rahaa na utalenga kusaidia mwanachama na familia yake kuu. 3-kuanzisha mfuko wa kukuza,kuendeleza na kusaidia wasanina paamoja ni michezo mbali mbali ukiwemo mpira wa miguu,pete,riadha nk. 4-kuanzisha kituo cha Michezo ambacho kitakuwa kikisimamiana kukuza vipaji vya vijana kuanziaa miaka 14-25 kwa mpira wa mguu VIJANA IRINGA FOOTBAL ACADEMY 5-kuanzisha kitua cha ambacho kitasimamiaa na kukuza vipaji vya wasanii muziki na filamu na kutoa elimu juu ya sanaa yaani IRINGA HOUSE OF TALENT. 6-kuanzisha kituo cha cha elimu kwa vijana ambacho kitaitwaa VIJANA IRINGA CENTRE,Kituo kitatoa elimu ya ujasiriamal,vita dhidi ya maadui watatu wa maendeleo ambao ni UJINGA,MARADHI na UMASIKINI,kutoa elimu juu ya kupinga matumiz ya madawa ya kulevya na elimu juu ya uzalendo wa ujenzi wa taifa letu na haswa kuhamasisha vijana katika kuipenda nchi yao. Mheshimiwa Mgeni rasmi, Tumedhamiria kufanya jambo ambalo litakuwa ni mfano wa kuigwa kwa jamii inayotuzunguka maana wahenga wanasema kuiga chema si dhambi nasi tunataka kuiga mema ili tuwe mfano bora kwa kizazi hiki na vizazi vijavyoi, tunaamini fursa za kujikomboa kimaendeleo ni nyingi bila jitihada zetu itabaki kuwa ndoto na historia na zaidi tukabaki kuwa walalamikaji na kujiingiza katika makundi hatarishi. Mheshimiwa Mgeni Rasmi ,tunazo siku 60 katika kuyatekeleza malengo yetu,Kupitia umoja huu tunataraji utakuwa mkombozi wetu kwa kutengeneza fursa ya ajira ambayo imekuwa changamoto kubwa si kwa nchi yetu tu bali dunia kwa ujumla tunataraji kupitia umoja huu vijana watajiajiri na sio kutegemea kuajiliwa kama ilivyo kauli mbiu yetu GEUZA KIPAJI KUWA AJIRA RASMI. . Mwisho Mheshimiw a mgeni rasmi kwa sasa nchi ipo katika mchakato wakutafuta katiba mpya na tumeshuhudida mengi yakijitokeza katika bunge la awali la kati wahenga wanasema yaliyopitaa si ndwele tgange yajayo kwa maneno hayo tunawaoma umoja wa katiba ukawaa warejee ili kuweza kuweka maridhiano ya upatikanaji wa ka tiba mpya,umoja wetu unaamini Ni jukumu la kila kiongozi kuongozwa na busara na kumwogopa mwenyezi MUNGU kwa kuwa kila mtanzania wa sasa atapenda kuwe na mabadiliko ambayo yatasaidia vizazi na vizazi. Hivyo katiba ya nchi ni muhimu katika kufikia maendeleo yanayohitajika na sisi vijana mkoa wa Iringa tunaomba sana salamu zetu utufikishie katika ngazi husika kwa kuwa kila mzalendo wa kweli hawezi kubishana na mawazo ya watanzania katika kufanikisha katiba mpya. Kwa kumalizia nakushukuru sana kwa kuweza kujumuika na sisi vijana katika tamasha hili na MUNGU akubariki sana katika kutekeleza majukumu yako na ya kiserikali. Sisi UMOJA WA VIJANA IRINGA (UVI)tuta hakikisha tunahamasisha vijana wote kupiga kura kwani kura ni haki ya kila mwananchi na tunaamini kuwa kupitia umoja huu vijana wengi watajitokeza kupiga kura. Napenda pia kuwakumbusha vijana wenzangu kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura unaotarajia kuanza mapema na kujitokeza katika kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa. MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA MUNGU UBARIKI MKOA WETU WA IRINGA. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA…… 03/08/2014

TIZAMA PICHA ZAID YA 13 HAPA ZA UZINDUZI WA UMMOJA WA VIJANA IRINGA (UVI) - ULIO FANYIKIA MAFINGA IRINGA NA ZAIDI YA VIJANA 450 KATI YA 970 YA WANAUMOJA HUO TAREHE 03/08/2014 ( NEWZ )





SHUKRANI ZA DHATI ZIWAENDEE, 1)Mheshimiwa mgeni mkuu wa wilaya ya mufindi evarista kalalu. 2)Wageni waalikwa 3)Katibu wa ccm wilaya mufindi-miraj mtaturu 4)Afisa maendeleo ya vijana wilaya-juma fuluge 5)Mjumbe wa halmashauri kuu ccm-marcelina mkini 6)Kaimu meneja waa benki ya mucoba-eliter maalangalila 7)Mshauri wa umoja huu dr yahaya Msigwa 8)Eddo Bashiri Mwenyekiti wa ummoja wa vijana Iringa 9)Rashid Msigwa Katibu wa Umoja wa vijana Iringa 10)Wanachama wote zaid ya 970 wa umoja wavijana Iringa pamoja na walio fanikisha Mchakato huu. MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA MUNGU UBARIKI MKOA WETU WA IRINGA.

Sunday, August 3, 2014

NELLY B FT CLOUD 9, OBBY, KARIMUSIC & MKWAWA - THANK YOU ( comming soon New Joint )

BAADAY YA MY VALENTINE TOKA KWA NELLY B (Mtangazaji toka Nuru Fm Iringa) SASA KUTUA MTAANI NA MZIGO MPYA WIKI MOJA MBELE MAPEMA SAANA NA MZIGO UITWAO ( THANK YOU ) NDANI YAKE KUKIWA NA VICHWA KAMA, CLOUD9, OBBY, KARIMUZIC, NA MKWAWA. PRODUCER Duppy kafanya bonge moja beat kama kawaida yake NA Silley toka Sampamba kafanya bonge moja la mixing kama kawaida yake [Nerry B] kawashirikisha wasanii wa kali kama kawaida yake wiki ya kesho ngoma inafanyiwa final mixing apa S.M.G Sampamba Music Group
Endelea kutembelea hapa, www.selengakaduma.blogspot.com Ili uwe wakwanza kuupata Mzigo huu wiki Ijayo.

Saturday, August 2, 2014

MAC MC FT DARK MASTER & ANGER TAINER - MTAONA ( PICHA ZA LOCATION )


MAC MC NI MSANII MCHANGA, AMBAE ANAKUJA VIZURI SANA KATIKA TASNIA YA MUZIKI. HIVI PUNDE AMEKUA LOCATION IRINGA AKIPIGWA PICHA ZA VIDEO ZINAZO TARAJIWA KUA ZA WIMBO WAKE MPYA UITWAO MTAONA, ULOFANYIKA BANTU MUSIC CHINI YA MAPRODUCER WAWILI GERALD NA LUSUNGU.

VIDEO HII IMESHUTIWA NA KAMPUNI YA EMAGINATION - KAMPUNI MPYA YA VIDEO TOKA IRINGA.

VIDEO HII INATARAJIWA KUINGIA MTAANI TAREHE 01/09/2014.


MAC MC AKIWA KAMSHIRIKISHA  DARK MASTER MWANA CHEMBER SQUIRED, NA ANGER TAINER NDANI. KAENI MKAO WA KULA KUIPATA VIDEO KALI HAPA HAPA.