Mambo mazuri yamewadia! Ule uliokuwa ukiusubiri kwa hamu huu hapa - Nagharamia, Christian Bella & Alikiba
Link 👉🏾
Wednesday, November 18, 2015
Joh Makini Ft. AKA - Don't Bother ( Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 8:41:00 PM
Wimbo mpya uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kutoka kwa mkali hizi flow DON'T BOTHER sasa upo hewani!
Link >
KUTOKA KWA PRINCE:USHUHUDA WA JINSI YESU ALIVYOMTOKEA NA KUMPA UTUME NA KUMUAMURU AWE RASTA
Posted by NAOMIKADUMA On 8:25:00 PM
Ilikua ni siku ya Ijumaa Terehe 13/2/2015 Usiku nikiwa Daresalam Tanzania maeneo ya Sinza, chumbani kwangu usiku nikiwa nimemaliza maombi na ninasoma Neno la Mungu, ghafla Nguvu ya Mungu kubwa sana ilinishukia nikiwa nimefunga macho nakuanza kutetemeka maana nilidhani mwisho wa Dunia ndio umefika, Ghafla ilitokea Nuru kubwa sana zaidi ya mwanga wa jua ikawa inanimulika usoni na kukimulika chumba chote. Niliogopa sana nami nikaanza kujiona kua ni mwenye dhambi kuliko wenye dhambi wote Duniani pia nilijiona kwamba simjui Mungu hata kidogo yaaani elimu yote mafundisho yote ninayo yajua kuhusu Mungu niliyaona ni sifuri nawala hayalingani kwa vyovyote na jinsi ukuu wa Mungu ulivyo. Nuru ilizidi kuongezeka mara nikaona mwanga mwingine mkali sana katikati ya Nuru ile; Ndipo nikasikia sauti kutoka katika mwanga ule ikisema "Amos Amos Amos Usiogope, mimi ni Yesu na nimekutokea kukupatia utume na kazi kubwa utakayoifanya Duniani kote, Nimekutia mafuta uwe Nabii na wewe ni mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa mama yako, Kwanzia leo wembe usipite kichwani mwako wala ndevuni mwako. Nakutuma uende kwa Ndugu zako Marasta (Rastafariansi) uwaambie kwamba kurudi kwangu kuwachukua watu wangu kumekaribia sana, nimekaribia sana kutoka katika chumba cha Patakatifu pa patakatifu pa mbinguni ninakofanya kazi ya Ukuhani na muda sio mrefu mlango wa Rehema utafungwa. Waambie waache kumwabudu Haile selassie kwani Yeye sio Mungu, yeye ni mwanadamu tu na alishakufa na anasubiri hukumu ya mwisho. Waambie wanigeukie mimi wapate Uzima wa milele. Kwanzia leo Amos nataka utoke kwenye mifumo yote (Systems) na uishi kama Nabii na Mnadhiri wa Mungu nami nitakua pamoja nawe popote uendapo. Pia utaacha vishungi (Dreadlocks) vya nywele za kichwa chako vikue viwe virefu maisha yako yote. Pia nakutuma uende kwa ndugu zako Watoto wanaoishi mitaani, ukawahubirie Neno langu waokoke. Dunia haitakuelewa, utapokea upizani mkubwa sana kutoka kwa ndugu zako wa Kristo na wale ninaokutuma kwao, lakini usiogope maana mimi ni pamoja nawe. Kwanzia leo nakupa Nguvu za Uponyaji na kutenda miujiza, utafanya Huduma za maombezi na watu wengi watafunguliwa. Viwete watatembea, Vipofu wataona, Wafu watafufuka kwa jina langu (Yesu) Je uko tayari?". Nikiwa nimejifunika kwa shati langu hapo chini huku nikilia na kutetemeka nilijibu niko tayari kwenda niko tayari kufanya kazi yako Bwana. Mara nilishukiwa na umeme mkali sana wa mbinguni Nguvu na Nuru ambayo sina lugha ya kuelezea. Lugha ya kibinadamu haitoshi kuelezea mambo makubwa Bwana aliyo nionyesha. Tangu siku hiyo maisha na mtazamo wangu vimebadilika kabisa. Naishi nakutembea na Nguvu kubwa sana za Mungu na nimekua katika maombi ya kufunga na Kukesha kwa muda mrefu sana. Mambo makubwa yanatendeka katika maisha yangu. Malaika wa Mbinguni wamekua wakinitokea mara kwa mara na kunitia moyo na Nguvu katika kazi hii ninayo ifanya. Yako mambo mengi aliyo nionyesha Yesu nami nitakua naya andika kidogo kidogo kwa kadiri Bwana atakavyokua akiniruhusu kufanya hivyo
By PRINCE AMOS MWANAMUZIKI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA
BARNABA FT JOSE CHAMILIONE - NAKUTUNZA ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 7:47:00 PM
255 imekutana na 256 hivi karibuni na wameahidi kukutunza! Sikiliza wimbo mpya wa Barnaba na Jose Chameleone
Link >
HARMONIZE - KIDONDA CHANGU ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 7:18:00 PM
Harmonize amekuwepo katika game kwa muda na kurekodi nyimbo kadhaa kabla hajanza kusikika kila kona. KIDONDA CHANGU ni wimbo aliyeurekodi kipindi cha nyuma kidogo lakini hukupata airplay ambao wimbo huu ulikuwa unastahili. Pakua wimbo hapa na ufurahie kipaji cha kijana huyu HARMONIZE.
Subscribe to:
Posts (Atom)