KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Thursday, May 29, 2014

STORI YA KUSISIMUA YA KAGUSA KIHESA MANJEMU JINSI ALIVYO PAMBANA MPAKA KUA DIRECTOR MKALI WA VIDEO ( STORY )

STORI HII INASIKITISHA NA INAFUNDISHA PIA KWA VIJANA NA WATANZANIA WANAOPAMBANA NA MAISHA YA KILA SIKU, NA WALIO KATA TAMAA. SOMA HAPA CHINI KUJUA NINI KILIMSIBU KAGUSA TOKA AUDIO PRODUCTION MPAKA KUA DIRECTOR WA VIDEO LEO. KARIBU..... Awali ya yote sipendi kufanya kazi huku nahuzunika na penda kufanya kazi inayonifurahisha hata kama napata kidogo kuliko kazi ya baniani nitakayolipwa vizuri....... kusema za ukweli kwangu furaha ndo kila kitu...... sikuwahi kuwa na ndoto za kuwa produzer mkubwa na ndomaana nyimbo nilizotengeneza hazifiki 50 na nikaachana na hako kakazi........ nilikua naamka nafocus beat... nafocus kufanya kazi na wasanii wanaojielewa nakumbuka mwaka 2008 nilianza kurekodia sebuleni... sitasahau kusikia sauti ya jogoo kabla ya kiitikio nafikiri alikuwa jogoo wa kina Alfa Urassa jirani yangu ....... pamoja na kuwa na focus yote na attention ya muziki muziki si kitu tu unachoweza kufanya kinahitaji akili nguvu na jitihada... inahitajika sapoti ya familia ambayo niwe tu mkweli nasapotiwa kwa kila ninachokifanya pengine kasoro tu upande wa kifedha kitu ambacho kila mtanzania ni changamoto yake........ Ukosefu wa kozi fupi za muziki nchini ulinifanya nijifunze muziki in hard way naposema ni hardway namaanisha ngumu haswa kuanzia kompyuta duni mpaka spika mbovu watu wangu wajirani wanajua........ am serious only when i must........ kwa kipindi ambacho nimeanza muziki nilikuwa sio kama mnavonijua sasa nilikua sina netwek kabisa hakuna ambaye angeweza kuniamini that time..... nilichukua muda kujifunza na niseme naishukuru sana intanet nashukuru sana waliokuwa wananipa plugin kina joshua god knows walikokuwa wakizitoa........ Ikafika muda nikawa nakaribia kufika sehemu niliyokua naitaraji pengine juu kuliko nilipokadiria kufikia tatizo likawa ni kufanya evolution yaani ukubwa wa kipaji ulishinda upatikanaji wa vifaa vya kisasa motivation ikakatika nikaa studio miezi sita bila kutengeneza nyimbo.... hivyo nikatangaza kuacha muziki it was frustrating moments in life ukizingatia vifaa vya studio ni kama niliazimwa tu na marafiki wenye roho safi it was like loosing everything you fought for... lakini mungu wetu mkubwa anajua kwanini ilitokea hivyo...... Wakati nahangaika na audio pia nilikua naunganisha vipicha kwenye windows movimaker kuanzia hapo nikawa napumzika hapo..... nilifanikiwa pia kujifunza software ya kwanza ya kueditia video profeshno... naizungumzia sonny vegas japo niliipata kwa shida kwakuwa mji mzima alikua nayo muongozaji mmoja tu na wakati huo hatukua marafiki akashindwa kuwa mkarimu lakini cha kushangaza nikakutana tena na joshua mbwanji aliyenipa software ya kutengenezea muziki ndo alinipa ya kueditia video at that time nilikua na kompyuta ram 126 na hd disk g 6 gb sijui nilikua nafanya nini lakini ndo kompyuta iliyonipa hiki nilicho nacho leo.............. nimejifunza kila kitu geto... Nilikua natamani sana kufanya video za muziki lakini angeniamini nani? kamera angenipa nani? mwezi wa kumi na moja mwaka 2009 nikiwa tumaini first year ndo niliweza kufanya nyimbo na ikaisha na kuweza kusikilizika sio muda mprefu kabisa ukiangalia calender ... nakumbuka nilikua nataka kusample biti ya no woman no cry ya bob and all over sudden nikapata idea ambayo lazima niseme ilibadilishia lyfe style maana ndo ilikua mara ya kwanza kutengeneza nyimbo ambayo hata mtu asiyesikiliza mzima na akili yake anaweza kuisikiliza nyimbo hiyo ilikuwa ya kaka angu aliyekua akinisuport katika muziki George Msandi anajiitaga man kichefu the dramacyder...... nilifanya nyimbo iliyokua ikiitwa kadi ya msiba..... iyo kadi ya msiba ni wimbo ambao nilirekodia george records wilolesi it was hard na vifaa vilikua robo tu tena vichakavu hivi nilipomaliza niliibeba kwa cd kwaajili ya kufanyia mixing nyumbani ile mixing nilifanya karibu miez mitatu ... haikuwa nzuri lakini inasikilizika hivi..... Ikaja aidea ya kurekodi video so boom langu la kwanza lote nilinunua kikamera kidogo pale kwa kibbs huku nikishindia viazoi vya mama obama hahahah David Agalla anajua hivi......hiyo ikanifanya niweze kurekodi video yangu ya kwanza mwaka 2010 nimerekodi hiyo video mwezi wa tatu hivi nimemaliza editing karibuni mwezi wa saba it was trully disapointing lakini i was proud na nilichokifanya nikawaambia ndugu zangu naelekea ninakokujua na natumia usafiri sahihi.... nikafanya video kadhaa sikulipwa na nyingi zilikuwa mbaya kuliko hata ya kwanza nakumbuka kuna moja nilishoot pale twisterz mwaka 2011 na kina Honnory Haule mwanzoni lakini sikuwa na mafanikio ikafika sehemu nikawa sijui nifanye nini ingawa sikuwa nawaambia watu lakini nilikua sijui nifanye nini kamera yangu ndogo ilipoharibika nikawa nashindwa kufanya miradi mipya kiukweli i had to lay low sasa huna kamera ukashuti nini? nikawa nagonga tu bit nyingi nagawa bure hata silipwi shida tupu ..... kwa nafsi moja nikaamua nisome tu sasa nitafanya nini? nikairudia shule moja kwa moja yaani nafanya assigment na kila kitu kuhusu shule moja ya kumbukumbu langu kubwa ntakayozeeka nayo... kuna siku nilikua sinahela sina hela kabisa nikampigia simu askari flani hivi anaimbaga nikamwambia niko sehemu flani njoo chukua bit nilipe walau kidogo.... ilikuwa biti bora kabisa......... kiukweli alipa buku tano na ilikua mwaka 2012 daa nakumbukaga na natamani kulia jinsi sanaa inavyochukuliwa bongo lakini kikubwa kuliko yote " KITU AMBACHO KIMESHINDWA KUKUUA KITAKUFANYA UWE SHUPAVU TU" ikawa imefika sehemu shule ngumu na sina matumaini si kwenye video wala kwenye mziki...... nikawa nalala tu lakini siku moja nikafikiria kuna kaka angu ana vyombo vya studio lakini havitumii ......... nikaenda kwao nikazungumza nae kwamba nataka nifanyie kazi vifaa vyake pengine ningekuwa namtumia aliko kiwango cha faida kinachopatikana muendelezo kutokana na muendelezo matumizi ya vifaa pindi nitakapomaliza chuo na ilikuwa hivyo ... tarehe 17 mwezi wa sita mwaka 2012 nilikua namiliki studio yaani nilikua na sehemu ninayoshinda yenye walau robo ya vifaa vinavyohitajika niaanzisha REBIRTH... na mwanzo kila kitu kilikua sawa lakini mh ! kadri siku zilivyokua zikienda ilikua ni shida ni mara nyingi tu nimeuza vitu vyangu kama simu to pay bills..... ikafika sehemu nikachoka ujue kinachoingia kilikua tofauti na kinachotakiwa kitumike nikafanya nyimbo kadhaa......lakini kamwe sikuwahi kutoa rushwa kwa presenter... Pamoja hayo kufanya video ilikuwa daima ni kitu ninachokipenda nilikua nikiomba kila siku nipate vifaa vya kisasa.....lakini kama tunavyojua MUNGU ANA MAKUSUDI YAKE kiukweli kuna kipindi your just smilling to people lakini moyoni unakuwa umenuna una basic skills lakini talent yako haikulipi......SIKU moja nikakaa nikaanza kutafakari kipi nakijua kuliko kingine lakini kwa roho moja nikawa na wasiwasi vipi hii nayo ikiwa ni illusion ? nikajua ni lazima nifanye maamuzi ........ nikafanya maamuzi ya kuwa director in full nikaachana na muziki rasmi mwaka 2013 mwishoni............... Leo hii miezi kadhaa baada ya kuamua nifanye video tu nahisi nimepiga hatua kuliko kile nilichokua nakifanya mwanzo... sijaacha kabisa kugonga beat ni kitu nikachokifanya part tyme sina starehe nyingi mimi natengeneza video na nashukuru wote walionipa sapoti nawashukuru wanaoniamini na kunipa kazi........... kuna kipindi huwa nawashangaa wanaonikuta nafanya video katika mazingira magumu huwaga nawashangaa haswa kwakuwa mi naona hii ni paradiso na nimebakisha step kadhaa kufikia level ambayo kila mtu anaitaka ..... .. nichukue nafasi hii ya time line zenu kuwataarifu naanza kufanya movie pia na nataka kufanya kitu cha kipekee...... nichukue tymeline zenu kuwaambia watu walioko kwenye harakati kama mimi kwamba our tyme is now never retreat.... lets just say never to defeat.... nimeshare hii stori nanyinyi kwakuwa nimekutana na mtu aliyekata tamaa hadi anatamani kujiua...... mjue kukata tamaa kuna muuzi mungu .... mungu hapendi loosers.... mungu anasaport watu wenye ushujaaa ndani yao kama daudi .... its funy though WAKATABAHU TEAM REBIRTH THE LAST TEAM TO STAND Nachukua nafasi hii ya kipekee kuwatambulisha video yangu ya kwanza kuifanya na nyimbo yangu ya kwanza kuirekodi..... hahahhahh kipind hiko najiita KAGUSA MARSHAL about 5 yrs ago ........daaamn SEARCH YOUTUBE.COM - KADI YA MSIBA - MAN KICHEFU