KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Tuesday, December 9, 2014

ALICHOKIANDIKA AISHA SANDIGA KWA DIAMOND PLATNUMZ ( Storry )


STORRY HII TOKA KWA AISHA SANDIGA ( Mtangazaji Ebony Fm Iringa ) Wow, worth sharing: HONGERA DIAMOND PLATNUMZ! Ngoja niseme kidogo kitu nilichojifunza kwa huyu kijana. Kuna wakati fulani Hezron Michael (Paul Mashauri) aliwahi kuandika kuhusu msanii wa muziki wa bongofleva Diamond akisifia bidii yake lakini sasa naelewa zaidi. Diamond huyu alikuwa hana hela ya kwenda studio mara ya kwanza (mtaji wa biashara) lakini hii hai kuwa kizuizi kwake. Kwa kuwa alitaka kutoka moyoni aisee hela ilipatikana! Ilikuwaje? Mama yake alimpa mkufu akauze ili apate hela ya studio. Na alienda studio. The rest is history. Sasa ili unielewe hapa naomba unisikilize kidogo. Unamjua Joseph Kusaga? Labda humjui. Huyu ni mmiliki wa Clouds FM na Clouds TV. Niliwahi kumsikiliza LIVE akisema kuwa wakati alipopata wazo la kufungua kituo cha redio mtaji "uligomba". Kwa kuwa alitaka saana kufungua redio alimfata mzazi wake akaomba HATI YA NYUMBA ili akakope pesa benki! Can you imagine? Mzazi alimpa akijua hiyo dream ikifa nyumba hawana. Hela ilikopwa nyumba ikawekwa rehani and the rest is history! Unamjua Jeff Bezoz? Kama humjui nisaidie tu kugoogle. Lol. Anyway. Huyu ni moja ya matajiri 20 wakubwa duniani. Hivi sasa akiwa No. 18 kwenye Forbes list utajiri wake ukiwa $32 billion! Lakini huyu bwana wakati anataka kuanzisha mtandao wake wa Amazon.com hakuwa na mtaji. Sasa huyu alichofanya aliwafata wazazi wake ambao walikuwa ndo wamestaafu. Akawaomba pensheni yao ili afungulie biashara. Can you imagine wazazi waliwaza nini? Wanamuuliza biashara gani anawambia ni mambo mapya ya internet nataka niuze vitabu kwa kutumia internet. Hawakuelewa lakini kwa vile alitaka wamkopeshe hiyo pensheni by hooks and crooks aisee walimpa! And the rest is history. Hebu jiulize leo wazazi wake wanaishije? Jiulize mzazi wa Jay Kusaga leo kama anashida ya nyumba (kama yupo hai.. Na kama yu hai aishi miaka mingi zaidi). Jiulize mama wa Diamond Platnumz leo anaishije. Kwanza tunavyoongea hayupo bongo yuko zake Sauzi na mwanaye! Yes. Jiulize kama ana shida ya hela ya kunulia mkufu tena. Sasa wengi mna woga! Ndoto unayo lakini ukiulizwa kidogo tu: We Salome unaomba hela ya biashara ukishindwa hela yangu itakuwaje..? Au ukiambiwa elimu ulishindwa biashara utaweza? Unajiinamia kesho unaenda kwenye mkesha kuomba Mungu afungue njia nyingine! Pshuuu! Hivi humo kichwani kuna maji au? Afu ukisikia watu wanafanikiwa ooh Freemason ooh one day nitamiliki na kutawaka. Tawala kwanza fikra zako! Fursa zinazidi kuja na kukupita uko tu reception unapata laki tatu kwa mwezi na degree yako ya Mass Communication! Pshuuu. Diamond alipouza mkufu hela nyingine alipeleka studio kurekodi nyingine akaenda British Council kusoma English! Mambo ya "Good morning" mambo ya "let me read the contact once again.." nini. Huyu ni mtu anayeona mbali. Wasanii Wangapi walikuwa maarufu kabla yake but hawakuwaza kama yeye. Niwataje? Halafu haohao wanamsengenya na kumponda. Hivi wasomi wangapi wanajua lugha zaidi ya Kiswahili. Honestly. Hivi nitajie wasomi wangapi wameitangaza nchi hii kimataifa kama Diamond Platnumz. Kila siku wasomi tunapost picha za graduation. "Thank God I have made it. Xoxo". You have made what? Joho au? Joho hata wanafunzi wa Nursery School wanavaa mbona. Ilipotokea uvumi kuwa anapewa degree ya heshima kila mtu alisema ooh sijui nini.. Umeitangaza nchi wewe?!! Diamond anasomesha watoto watatu IST. Unajua ada ya IST lakini? Au unadhani naongelea gari IST. Naongelea International School of Tanganyika ambao watoto wa mabalozi wa nchi za nje ndo wanasomeshwa na nchi zao! Huyo ni Diamond Platnumz! Wewe umesomesha wangapi hata shule ya Kata na una Masters ya UDSM sijui ya Mzumbe sijui ya Edinburgh, nk. Mentality is everything. Sasa Mungu akubariki wewe au yeye? Kila siku uko kwenye maombi ya kufunguliwa na kuinuliwa unarudi nyumbani saa tano usiku Diamond anatoka studio saa saba za usiku. Who is hard working? Siku ya mwisho walokole tutaabishwa na watu tunaowaona "namna gani vipi". Mungu atupe ujasiri wa kufanya makuu! Mentality ya utajiri haiangalii elimu. Shigongo na wewe nani kasoma zaidi. Nani tajiri? Nani anaweza kuitwa na rais awambie vijana kwenye TV kuhusu biashara Shigongo au wewe mwenye Degree ya biashara kutoka CBE? Jiulize maswali magumu. Usijipe FALSE HOPES. Ati hata nikikosa hela mbinguni naenda. Sikia wewe, kuna watu hawakwendaga mbinguni kwa sababu tu hawakumvisha mtu aliyekuwa na uhitaji wa Nguo. "Nalikuwa uchi...." Hilo tu. Nilikuwa namchekesha cousin wangu Haruni Leonard kuwa unaweza kwenda mbinguni ukamkuta BOB MARLEY na huku wewe ulikuwa unaimba gospel. Kama unataka kufanikiwa hebu acha excuses. Sina mtaji. Sina muda. Kwani kuna mwenye kiwanda cha kuzalisha muda? Muda wa Escrow uliupata. Muda wa kukaa kubadilishana mawazo na watu upate mtazamo mpya huna eti. We kaa hapo? December ndo hiyo imefika! Diamond akirudi hukawii kusikia kaenda ikulu. We roho inakuuma hata kazini kwako tu hutambuliki. Hukawii kusikia kaenda Marekani kufanya shoo. We mwisho wako Tabata Bima Buguruni Posta hata huko hawakujui. Success has nothing to do with your religion but your MENTALITY. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA NAMTUNZI ....

MZUNGU KICHAA - TWENDE KAZI ( New Audio )


OFFICIAL PRESS RELEASE Mzungu Kichaa releases his first Swahili single since his award winning debut album Tuko Pamoja. The single titled ‘TWENDE KAZI’ (Let’s Work) is from his EP ‘HUSTLE’ which was released on the 12.12.12. Mzungu Kichaa and P Funk Majani have produced the song. With over 50 Bongo Flava albums to his name Majani is without a doubt the Godfater of Bongo Flava, one of East Africa strongest and most popular urban genres. Twende Kazi has been nominated for a Danish Music Award as Best World Track. The song is released on Mzungu Kichaa’s own label Caravan Records. It has been mixed and mastered at Copenhagen’s Winding Road Studios by Flemming Rasmussen, who, apart from producing some of Denmarks biggest artists, produced Metallica’s first four albums. “Staying true to who I am, this single off my EP ‘Hustle’, is first and foremost for my Tanzanian fans. However I will be pushing my personal boundaries when Hustle hits the streets; The EP also has two songs in English and a collaboration with one of my favorite Kenyan artists. I am very excited about this release, as I have been dying to show my non-Swahili speaking fans what I write about in my music”. The songs nomination for a Danish Music Award shows that Tanzanian Bongo Flava has a wider appeal than ever before. Since the release of his debut album, Tuko Pamoja, Mzungu Kichaa has been actively touring in Denmark with his Tanzanian band, which explains how the artist landed this nomination. Mzungu Kichaa has also toured Africa, with several concerts in Kenya, Uganda and Tanzania. Twende Kazi encourages youth to take their futures into their own hands. It condemns jealousy and the idea that success comes easily. Please see the lyrics for Twende Kazi below: CONTACT: Louise Kamin +255 789 275 947, +255 763 022 022 CRTanzania@gmail.com T: @caravanrec

TEL OMAINO - NIPENDE ( New Audio Coming soon )


Kutoka kipande cha Tunduru one,anaitwa Tel omaino,msanii wa bongo fleva yupo kwenye hatua za mwisho za kuachia ngoma yake mpya itakayoitwa 'nipende' ikiwa imefanyika studio za mkubwa music chini ya utayarishaji wa producer Necka beat. Soon Ujio wake utasomeka hapa hapa kwenye Ukurasa wetu. Anaomba support yako mdau na maoni, pale ikibidi.