KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Friday, October 24, 2014

ANGEL BENARD - NEED YOU TO RAIGN ( New Audio )


Episode 01: NEED YOU TO REIGN by ANGEL BENARD Wimbo wa kwanza katika album ya NEW DAY kutoka kwa ANGEL BENARD "Need you to reign" ni wimbo unaomuomba Mungu awepo katika maisha yake na amuongoze katika kila jambo. Wimbo huu umerekodiwa Mujwahuki Studios chini ya Producer Mujwahuki mwenyewe. Producer huyu pia alishawahi kufanya kazi na msanii Ben Pol katika wimbo wake wa Nikikupata. Nyimbo zote katika album hii zimetungwa na kuimbwa na Angel Benard.

MWANA FA FT ALIKIBA - KIBOKO YANGU ( New Audio )


Sote tumeusubiri kwa hamu na sasa wimbo mpya kabisa wa Mwana FA na Alikiba umewasili rasmi. Baada ya Mwana FA kutoa wimbo wa Mfalme live katika tuzo za KTMA 2014 msanii huyu ameungana na mfalme wa bongo flava yaani Alikiba ili kuwaletea mashabiki wake kazi nyingine kali. Producer wa wimbo huu si mwingine bali ni Marco Chali wa kutoka MJ Records ya jijini Dar Es Salaam. Katika kuurekodi wimbo huu kumekuwa na matoleo manne tofauti ambayo wadau walikuwa wakisindwa kuamua ni upi wa kuachia kwa kuwa zote zimesimamia kucha. Mwana FA na kampuni ya LifeLine ambaye yeye pia ni mkurugenzi wameamua kuuachia wimbo huu moja kwa moja kupitia Mkito.com ili kuhakikisha unawafikia wapenzi wake wengi zaidi na kuhakikisha kuwa kuna maslahi yanapatikana katika kazi hii. Pakua wimbo huu mpya kabisa sasa upate flava kali.

DENNIS DRAZZY - CHEZA ( New Audio )






CHEZA is a song performed and written by a young Upcoming artist from Tanzania, Dennis Drazzy (22) who does Rap with a twist. The song which is recorded and mastered at Hebron Studios and mixes elements of House music, pop and rap all in one resulting to a Rap House genre and is from the Black & White mixtape coming in 2015.

MAD ICE - EVERYTHING I DO ( New Audio )


Mad Ice ni msanii aliyezaliwa nchini Uganda na kuishi Tanzania kwa muda mrefu ambapo aliaanza rasmi kazi yake ya muziki na kutoa albam yake ya utmbulisho iitwayo BABY GAL (2003, Chini ya Miikka Mwamba). Msanii huyu wa Afro-Soul baada ya album hiyo alihamia nchini Finland ambapo aliendeleza kazi pamoja na producer Miikka Mwamba na studio nyingine nchini humo na kutoa nyimbo nyingi zilizoshika chati tofauti duniani kote zikiwemo Maneno, Mapaenzi Sumu na Te Amo. Single mpya kabisa ya Mad Ice inaitwa EVERYTHING I DO na imefanyika Sonic Pump Studios, Finland chini ya producer DJ Hermanni.

TIZAMA PICHA 5 ZA UJIO WA MAD ICE NA TOKA MOJA YA STUDIO KUBWA DUNIANI ( Up Date Info )







Mwanamuziki Mad Ice amerudi Tanzania kutoka nchini Finland ambapo ametoka kurekodi single yake mpya EVERYTHING I DO chini ya producer DJ Hermanni kwenye studio ya kimataifa ya Sonic Pump Studios (http://www.sonicpumpstudios.com/). Mara nyingine huwa inatosha kuangalia mandhari ya studio kujua kuwa kazi zinazotoka huko lazima ziwe na kiwango cha kimataifa. Tazama picha hizi za studio halafu tusubiri kusikia mapishi yake Jumatatu tarehe 20 Oktoka.

ANGEL BENARD - 10 SONGS 10 WEEKS ( UpDate Info )



ANGEL BENARD ni jina ambalo limekuwa likisikika kwa miaka kadhaa sasa kwenye ulimwengu wa muziki wa gospel. Angel Benard mwenye miaka 25 hatimaye sasa anaachia album yake NEW DAY kwenye mfumo wa digitali kupitia Mkito.com. Watu wengi wamekuwa wakisubiri kusikia nyimbo zake za zamani lakini haikuwa rahisi kuzipata. Album hii ni album ya 3 ya mwana dada huyu mwenye sauti ya maajabu. Ni wasanii wachache sana wa muziki wa gospel ambao wamefanikiwa kuvusha nyimbo zao zikapendwa na wapenzi wa gospel pamoja na wapenzi wa muziki wa bongo flava, RnB n.k. na mwimbaji huyu ni mmoja wapo. Katika kuitambulisha album hii Angel Benard ataachia wimbo mmoja kila siku ya Alhamis kwa wiki 10 mfululizo. Wimbo wa kwanza utatoka tarehe 23 October na unaitwa NEED YOU TO REIGN ukiwa katika minodoko ya Reggae.

HISIA - MAWAZO ( Vocal of New Audio )

Msanii Hisia ambaye aliiwakilisha vyema sana nchi yetu katika mashindano ya Tusker Project Fame mwaka jana anakaribia kuachia wimbo wake mpya uitwao GIVE ME A CALL hapo tarehe 25 Octoba katika show ya live. Katika kuusubiri wimbo huo tujikumbushe track yake ambayo imeshika chati nchini Kenya kwa wiki 6 mfululizo iitwayo MAWAZO. Wimbo huu pia unapatikana kama acapella, yaani vocal tu, ili wapenzi wake tusikie ni kwanini Hisia aliweza kufanya vizuri vile kwenye mashindano ya Tusker Project Fame. Kwa wale wote watakao taka kufika kwenye show yake itafanyika tarehe 25/10/2014 Alliance Francaise kuanzia saa moja jioni.

BRAND NEW MKUBWA NA WANAWE - INOOH (Audio)


Wimbo mpya kutoka kwa Mkubwa na Wanawe ambao ni kati ya nyimbo zilizopo kwenye collection ya NISEME. Wimbo huu inaitwa INOOH. Mkubwa na Wanawe ni wansanii ambao kwa muda mfupi sana wameweza kuonekana katika majukwaa makubwa na kuwa na mafanikio makubwa sana kimuziki wakiwa chini ya usimamizi wa Mkubwa mwenyewe Saidi Fela. Fela ni meneja ambaye amesimamia na kuwatoa wasanii na makundi kama Juma Nature na Wanaume. Pata wimbo mpya kabisa kutoka kwa Mkubwa na Wanawe kupitia Mkito.com sasa.