Inasikitisha sana kuona baadhi ya vyombo vya habari haviupi promotion ya kutosha wimbo wa wanandoto wa kala jeremiah. Ukizingatia wimbo huo unaongelea maswala ya watoto yatima inamaana vyombo vya habari havinauchungu na watoto yatima. Wimbo siyo wa watoto yatima tu bali ni wimbo pekee mkubwa kwa mwaka huu. Kama mtu anabisha kuwa huu siyo wimbo pekee mkubwa kwa mwaka huu aniambie ni wimbo gani unauzidi wanandoto. Hii ni dalili mbaya sana kwa ustawi wa muziki wetu. Tumesahahau tulikotoka na hatujui tunapokwenda. Wimbo wa wanandoto naufananisha na wimba wa starehe wa ferouz hii inamana ferouz angetoa wimbo huu miaka hii usingechezwa kama ulivyochezwa na usinge kubalika kama ulivyokubalika.watu wa vyombo vya habari tuweni wa kweli mtu akifanya kitu kizuri kisapotini. Basi hata fanyeni kwa ajili ya watoto yatima. Au watoto yatima sichochote kwenu?.simanishi vyombo vya habari vyote ila baadhi hawautendei haki wimbo huu.
Hivyo kama Mdau wa Muziki na kama unamchango katika sanaa ya Muziki, unaombwa kua real katika kusaport kazi nzuri na zenye matokeo Chanya katika jamii.
By Selenga Kaduma