KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Thursday, December 18, 2014

ANGEL BENARD - LINDA MOYO WAKO ( New Audio )


LINDA MOYO WAKO ni wimbo wa 9 kutoka kwenye album ya nyimbo 10 NEW DAY ya ANGEL BENARD: "Ni inspirational song ambayo inalenga kuonya na kushauri namna mtu mwenye ndoto au maono fulani yatatimieje. Ni maneno yenye faida kumsaidia mtu namna ya kuishi na watu 'si kila achekae akupenda, tabasamu ni mwamvuli kuficha yalo ndani ya mtu' sasa ili kujiepusha na tabu na watu, jua we ni nani, unaenda wapi na waliokuzunguka ni watu wa namna gani."

909 - NJOO HAPA ( New Audio )


Baada ya mafanikio mbali mbali yakiwemo kuachia Mixtape yao ya kwanza (Here Goes Nothing), na kuperfom kwenye stage mbali mbali kwa mwaka 2014 sasa Mwaka unavyoelekea ukingoni,kundi la muziki 909 wanakuetea wimbo wa kusikiliza na uwapendao msimu huu wa Kristmasi, ikiwa bonus track ya Album yao inayotarajiwa kutoka mwanzoni mwa mwaka 2015