KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Friday, November 14, 2014

HII NDIO SAFARI YA MWISHO YA MAISHA YA Ahmed Ally Upete 'Geez Mabovu' DUNIANI.

Ahmed Ally Upete 'Geez Mabovu' ALIZALIWA MWAKA 1983 IRINGA TANZANIA.KAMA ARTIST MKUBWA WA HIP HOP TANZANIA, ALIWEZA FANYA HIT SONG KALI KADHAA, IKIWEMO MTOTO WA KIUME, DAKIKA 0, NA NYINGINE NYINGI
PICHANI NI PRODUCER LAMAR AMBAE MPAKA UMAUTI UNAMKUTA GEEZ ALIKUA AKIFANYA PROJECT NAE YAKUMUANDALIA GEEZ ALBUM YAKE AMBAYO ILITARAJIWA KUWA ALBUM YAKWANZA KUTOKWA KWA GEEZ KUINGIA MTAA. KWAMUJIBU WA MDOGOAKE GEEZ MABOV, MAD P, TULIPO ZUNGUMZANAE ALISEMA ALBUM HIO ILIKUA IMESHA KAMILIKA NA INANYIMBO 13 ILA ILIKUA KWENYE HATUA ZAMWISHO. ALIPOULIZWA JUU YAKUTOKA ALISEMA NIMAPEMA MNO KULIZUNGUMZIA HILO.










Ahmed Ally Upete 'Geez Mabovu' amefariki dunia Jumatano, mida ya Saa Moja akiwa mkoani Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita akitokea jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa bwana Dennis ambaye alikuwa mtu wa karibu wa Geez Mabovu amethibitisha kuhusu kifo hicho na kusema rapa huyo aliondoka Dar kwenda Iringa akiwa kwenye hali ambayo sio nzuri kiafya.

EMMANUEL ATMIN aka Emmo AMEWEZA MZUNGUMZIA ZAIDI GEEZ MABOV KAMA MTANGAZAJI KATIKA REDIO NDINGALA ILIOPO MKOANI RUKWA-SUMBAWANGA KATIKA KIPINDI CHAKE MAARUFU CHA AFRO CIRCLE KINACHOFANYIKA KILA SIKU KUANZIA SAA MBILI KAMILI USIKU HADI SAA NNE KAMILI. ZAIDI MSIKILIZE HAPA CHINI KATIKA KIPINDI CHAKE ALICHOFANYA TARE 13/11/2014 BAADA YA MAZISHI YA GEEZ MABOV IRINGA.