KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Tuesday, January 26, 2016

SWEET FLAVOUR - POLE POLE ( New Audio )


Hello! Mpaka hivi sasa kumekua na so many short video clips za watu mbali mbali zilizo sambaa sana sana mitandaoni wakiji record huku wakiimba nakutumiana wimbo wa Pole Pole ulioimbwa na vijana wapya katika tasnia hii ya Music. Vijana hawa wenye sauti yakubembeleza wanaoitwa Sweet Flavour wamekua nitishio sana kwa wengi kutokana na vile wimbo wao ulivyoweza kusambaa kama umeme mitandaoni. Kwa muda mchache tu baada ya wimbo huu kudakwa na moja kati ya watu waliotembelea studio za Kaburu Records nakuutuma kwa mwenzake na mwenzake pia kwa mwenzake wimbo huu umekua ukisambaa kwa kasi sana nakuinua maswali mengi kwa wapenzi wa Music. Wengi wamekua wakitaka kuwajua zaidi vijana hawa wenye sauti zakuwavutia na kuwaburudisha wengi haswaa wakina dada mpaka kuwapelekea kuushika wimbo huu kwa kipindi kifupi tu na hapa ndipo utakapo pata nafasi yakuwajua Sweet Flavour. Sweet Flavour nikundi la vijina wawili toka Kaburu Entertainment wakiwa kama label nakusimamiwa kazi zao zote hapo chini ya Kaburu Entertainment. Vijana hawa T More na Singano huu ni wimbo wao wa kwanza kabisa na umeonyesha neema kubwa baada yamashabika kuupokea vyema. Wimbo umefanyika Kaburu Music Studio chini ya Producer Father Beat a.k.a Kona nakusimamiwa na CBH a.k.a Sampa Music King. Zaidi na zaidi wimbo huu wenye melody yakuto toka kichwani pindi ukiusikia, vijana hawa wameweka kilio chao chote ndani ya mapenzi nakulalamika juu ya mapenzi yanayowatesa wengi huku bado wakijishusha kinyonge! Wamejaribu kuwakilisha kila chozi la mnyonge wamapenzi nakumfanya kila mtu aguswe nakuhisi wimbo huu ni sahihi kumtumia mpenzi wake. Sio maneno tu! Sikiliza wibo huu hapa alafu utajua nikipi kimeupa nafasi yakupenya nakupendwa nawatu wengi.

0 comments:

Post a Comment