Friday, December 12, 2014
Tuesday, December 9, 2014
ALICHOKIANDIKA AISHA SANDIGA KWA DIAMOND PLATNUMZ ( Storry )
Posted by NAOMIKADUMA On 11:42:00 AM
STORRY HII TOKA KWA AISHA SANDIGA ( Mtangazaji Ebony Fm Iringa ) Wow, worth sharing: HONGERA DIAMOND PLATNUMZ! Ngoja niseme kidogo kitu nilichojifunza kwa huyu kijana. Kuna wakati fulani Hezron Michael (Paul Mashauri) aliwahi kuandika kuhusu msanii wa muziki wa bongofleva Diamond akisifia bidii yake lakini sasa naelewa zaidi. Diamond huyu alikuwa hana hela ya kwenda studio mara ya kwanza (mtaji wa biashara) lakini hii hai kuwa kizuizi kwake. Kwa kuwa alitaka kutoka moyoni aisee hela ilipatikana! Ilikuwaje? Mama yake alimpa mkufu akauze ili apate hela ya studio. Na alienda studio. The rest is history. Sasa ili unielewe hapa naomba unisikilize kidogo. Unamjua Joseph Kusaga? Labda humjui. Huyu ni mmiliki wa Clouds FM na Clouds TV. Niliwahi kumsikiliza LIVE akisema kuwa wakati alipopata wazo la kufungua kituo cha redio mtaji "uligomba". Kwa kuwa alitaka saana kufungua redio alimfata mzazi wake akaomba HATI YA NYUMBA ili akakope pesa benki! Can you imagine? Mzazi alimpa akijua hiyo dream ikifa nyumba hawana. Hela ilikopwa nyumba ikawekwa rehani and the rest is history! Unamjua Jeff Bezoz? Kama humjui nisaidie tu kugoogle. Lol. Anyway. Huyu ni moja ya matajiri 20 wakubwa duniani. Hivi sasa akiwa No. 18 kwenye Forbes list utajiri wake ukiwa $32 billion! Lakini huyu bwana wakati anataka kuanzisha mtandao wake wa Amazon.com hakuwa na mtaji. Sasa huyu alichofanya aliwafata wazazi wake ambao walikuwa ndo wamestaafu. Akawaomba pensheni yao ili afungulie biashara. Can you imagine wazazi waliwaza nini? Wanamuuliza biashara gani anawambia ni mambo mapya ya internet nataka niuze vitabu kwa kutumia internet. Hawakuelewa lakini kwa vile alitaka wamkopeshe hiyo pensheni by hooks and crooks aisee walimpa! And the rest is history. Hebu jiulize leo wazazi wake wanaishije? Jiulize mzazi wa Jay Kusaga leo kama anashida ya nyumba (kama yupo hai.. Na kama yu hai aishi miaka mingi zaidi). Jiulize mama wa Diamond Platnumz leo anaishije. Kwanza tunavyoongea hayupo bongo yuko zake Sauzi na mwanaye! Yes. Jiulize kama ana shida ya hela ya kunulia mkufu tena. Sasa wengi mna woga! Ndoto unayo lakini ukiulizwa kidogo tu: We Salome unaomba hela ya biashara ukishindwa hela yangu itakuwaje..? Au ukiambiwa elimu ulishindwa biashara utaweza? Unajiinamia kesho unaenda kwenye mkesha kuomba Mungu afungue njia nyingine! Pshuuu! Hivi humo kichwani kuna maji au? Afu ukisikia watu wanafanikiwa ooh Freemason ooh one day nitamiliki na kutawaka. Tawala kwanza fikra zako! Fursa zinazidi kuja na kukupita uko tu reception unapata laki tatu kwa mwezi na degree yako ya Mass Communication! Pshuuu. Diamond alipouza mkufu hela nyingine alipeleka studio kurekodi nyingine akaenda British Council kusoma English! Mambo ya "Good morning" mambo ya "let me read the contact once again.." nini. Huyu ni mtu anayeona mbali. Wasanii Wangapi walikuwa maarufu kabla yake but hawakuwaza kama yeye. Niwataje? Halafu haohao wanamsengenya na kumponda. Hivi wasomi wangapi wanajua lugha zaidi ya Kiswahili. Honestly. Hivi nitajie wasomi wangapi wameitangaza nchi hii kimataifa kama Diamond Platnumz. Kila siku wasomi tunapost picha za graduation. "Thank God I have made it. Xoxo". You have made what? Joho au? Joho hata wanafunzi wa Nursery School wanavaa mbona. Ilipotokea uvumi kuwa anapewa degree ya heshima kila mtu alisema ooh sijui nini.. Umeitangaza nchi wewe?!! Diamond anasomesha watoto watatu IST. Unajua ada ya IST lakini? Au unadhani naongelea gari IST. Naongelea International School of Tanganyika ambao watoto wa mabalozi wa nchi za nje ndo wanasomeshwa na nchi zao! Huyo ni Diamond Platnumz! Wewe umesomesha wangapi hata shule ya Kata na una Masters ya UDSM sijui ya Mzumbe sijui ya Edinburgh, nk. Mentality is everything. Sasa Mungu akubariki wewe au yeye? Kila siku uko kwenye maombi ya kufunguliwa na kuinuliwa unarudi nyumbani saa tano usiku Diamond anatoka studio saa saba za usiku. Who is hard working? Siku ya mwisho walokole tutaabishwa na watu tunaowaona "namna gani vipi". Mungu atupe ujasiri wa kufanya makuu! Mentality ya utajiri haiangalii elimu. Shigongo na wewe nani kasoma zaidi. Nani tajiri? Nani anaweza kuitwa na rais awambie vijana kwenye TV kuhusu biashara Shigongo au wewe mwenye Degree ya biashara kutoka CBE? Jiulize maswali magumu. Usijipe FALSE HOPES. Ati hata nikikosa hela mbinguni naenda. Sikia wewe, kuna watu hawakwendaga mbinguni kwa sababu tu hawakumvisha mtu aliyekuwa na uhitaji wa Nguo. "Nalikuwa uchi...." Hilo tu. Nilikuwa namchekesha cousin wangu Haruni Leonard kuwa unaweza kwenda mbinguni ukamkuta BOB MARLEY na huku wewe ulikuwa unaimba gospel. Kama unataka kufanikiwa hebu acha excuses. Sina mtaji. Sina muda. Kwani kuna mwenye kiwanda cha kuzalisha muda? Muda wa Escrow uliupata. Muda wa kukaa kubadilishana mawazo na watu upate mtazamo mpya huna eti. We kaa hapo? December ndo hiyo imefika! Diamond akirudi hukawii kusikia kaenda ikulu. We roho inakuuma hata kazini kwako tu hutambuliki. Hukawii kusikia kaenda Marekani kufanya shoo. We mwisho wako Tabata Bima Buguruni Posta hata huko hawakujui. Success has nothing to do with your religion but your MENTALITY. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA NAMTUNZI ....
SHIZZE - SHINE ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 11:15:00 AM
Msanii wa Ragga kutoka nchini Kenya anakuletea wimbo wake mpya SHINE. Msanii SHIZZE amefanikiwa kushinda tuzo ya Best Ragga and Dance hall ya mwaka 2013 na pia amefanikiwa kuwashirikisha wasanii wakubwa wa nchini Kenya pamoja na nje ya Kenya.
MZUNGU KICHAA - TWENDE KAZI ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:54:00 AM
OFFICIAL PRESS RELEASE Mzungu Kichaa releases his first Swahili single since his award winning debut album Tuko Pamoja. The single titled ‘TWENDE KAZI’ (Let’s Work) is from his EP ‘HUSTLE’ which was released on the 12.12.12. Mzungu Kichaa and P Funk Majani have produced the song. With over 50 Bongo Flava albums to his name Majani is without a doubt the Godfater of Bongo Flava, one of East Africa strongest and most popular urban genres. Twende Kazi has been nominated for a Danish Music Award as Best World Track. The song is released on Mzungu Kichaa’s own label Caravan Records. It has been mixed and mastered at Copenhagen’s Winding Road Studios by Flemming Rasmussen, who, apart from producing some of Denmarks biggest artists, produced Metallica’s first four albums. “Staying true to who I am, this single off my EP ‘Hustle’, is first and foremost for my Tanzanian fans. However I will be pushing my personal boundaries when Hustle hits the streets; The EP also has two songs in English and a collaboration with one of my favorite Kenyan artists. I am very excited about this release, as I have been dying to show my non-Swahili speaking fans what I write about in my music”. The songs nomination for a Danish Music Award shows that Tanzanian Bongo Flava has a wider appeal than ever before. Since the release of his debut album, Tuko Pamoja, Mzungu Kichaa has been actively touring in Denmark with his Tanzanian band, which explains how the artist landed this nomination. Mzungu Kichaa has also toured Africa, with several concerts in Kenya, Uganda and Tanzania. Twende Kazi encourages youth to take their futures into their own hands. It condemns jealousy and the idea that success comes easily. Please see the lyrics for Twende Kazi below: CONTACT: Louise Kamin +255 789 275 947, +255 763 022 022 CRTanzania@gmail.com T: @caravanrec
TEL OMAINO - NIPENDE ( New Audio Coming soon )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:37:00 AM
Kutoka kipande cha Tunduru one,anaitwa Tel omaino,msanii wa bongo fleva yupo kwenye hatua za mwisho za kuachia ngoma yake mpya itakayoitwa 'nipende' ikiwa imefanyika studio za mkubwa music chini ya utayarishaji wa producer Necka beat. Soon Ujio wake utasomeka hapa hapa kwenye Ukurasa wetu. Anaomba support yako mdau na maoni, pale ikibidi.
Saturday, December 6, 2014
PREZZO - BILA MUNDAI ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 12:16:00 PM
ANGEL BENARD - NUMBER 1 ( New Gospel Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 12:06:00 PM
Wimbo wa 7 kutoka kwenye album ya NEW DAY ya ANGEL BENARD unaitwa Number 1. "Katika number one, Ninazungumzia tabia za Mungu zinazomfanya yeye kuwa namba moja kwangu na hivyo ninakuwa nasimulia habari zake." - Angel Benard
TID FT NAZIZI - PRESSURE ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 11:59:00 AM
Mwanamuziki mkongwe TID anakuletea wimbo wake mpya uitwao PRESSURE aliomshirikisha NAZIZI kutoka nchini Kenya.
Saturday, November 29, 2014
WILLIAM OTUCK - ZAWADI YA X - MASS ( New Audio Album )
Posted by NAOMIKADUMA On 9:25:00 AM
Album mpya ya Krismasi! Huu ndiyo wimbo wa utambulisho kutoka kwa William Otuck: https://mkito.com/song/zawadi-ya-x-mas/4691 Album nzima inapatikana hapa: https://mkito.com/artist-profile/otuck-william/964 Krismasi hii, Santa hatokuwa akitoa zawadi peke yake. Na hata hivyo inaonekana kuwa baadhi watamzidi katika hilo linapokuja suala la muziki! Otuck William, muimbaji wa soul, athibitisha hilo kwa kuleta mbele yako bidhaa mpya itakayobadili sura nzima ya msimu wa Krismas mwaka huu kimuziki. Ni santuri itakayokuwa imebeba nyimbo kumi na tano (15) mahususi kabisa kwa ajili ya Krismas. Akizungumzia album hiyo Otuck anasema; "“Zawadi Ya Krismasi” ni album yenye nyimbo 15 iliyotayarishwa kwa ushirikiano wa kwangu mwenyewe na Nach B, mtayarishaji kutoka studio za Beats Bank Music zilizopo jijini Mbeya. Hii si album ya dini (Gospel) japokuwa imebeba baadhi ya nyimbo za zamani za kidini za Krismas, ambazo tumezitayarisha katika mahadhi tofauti kidogo, lakini ni album inayohusu Familia, Matumaini, Faraja, Imani na Upendo. Kwa kadri ya ufahamu wangu inaweza kuwa album ya kwanza kabisa ya Krismas kuwahi kutengenezwa Tanzania au Afrika Ya Mashariki kwa ujumla”. Ni wazi kwamba kila mtu anatamani kujua nini hasa Otuck ametuandalia, kitakachodumu kwa muda mrefu na kutufariji kila ifikapo msimu kama huu. Album hiyo itakuwa ikipatikana katika mtandao wa Mkito.com kuanzia Tar 26 Novemba 2014. Lakini pia itauzwa katika mfumo wa CD. Kwa mawasiliano zaidi ya namna ya kupata CD hizo au kuwa wakala wa usambazaji, andika barua pepe kwa otuckwilliam@gmail.com au piga simu nambari +255712168011
ANGEL BENARD - UFUNDISHE MOYO ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 9:17:00 AM
ANGEL BENARD - UFUNDISHE MOYO WIMBO WA 6 WIKI YA 6 KATI YA NYIMBO 10 ZINAZOTARAJIWA TOKA KWA WIKI 10 MFULULIZO. "Ni sala ambayo ninamuomba Mungu anifundishe kumuabudu katika roho ya kweli, na siyo tu nikiwa katika shida au ninapohitaji msaada fulani."
Wednesday, November 26, 2014
LAMECK DITTO - HERI YA CHRISTMAS ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:25:00 PM
Msimu wa Christmas ndiyo unatufikia sasa na wimbo wa kwanza wa Christmas ndiyo huu hapa kutoka kwa Ditto. Ditto ambaye ameandika nyimbo nyingi ambazo ni hits kubwa katika muziki wa Tanzania pia ni mwimbaji na mwalimu wa muziki Tanzania House of Talent.
NAVY KENZO - MOYONI ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:16:00 PM
Wimbo mpya kutoka kwa Navy Kenzo unaitwa MOYONI na unatoka kwenye album mpya ya NIROGE. Wimbo unaongelea wapenzi wawili ambao wanataka kuchukua hatua nyingine kubwa katika uhusiano wao. Wimbo umekuwa produced na Nahreel mwenyewe.
QUICK ROCKA FT YOUNG DEE - BISHOO ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:16:00 PM
Wimbo mpya kabisa kutoka kwa bingwa wa tongue twister. QUICK ROCKA anakuletea BISHOO ambao ni wimbo amemshirikisha Young Dee.
Monday, November 24, 2014
NAVY KENZO - NEW SONG COMING SOON ( Update Info )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:01:00 PM
UJIO MPYA WA ANAVIKENZO HUU HAPA, KAMA KAWA WAPENZ WA MZIKI WA KIZAZI KIPYAA KAENI MKAO WAKUPATA VITU VYAMOTO, SOON HAPA HAPA KWENYE UKURASA WENU WAKIJANJA. TAR 25/11/ 2014 TRACK HII ITAINGIA MTAANI RASMI. JIPANGEEEEEEEEEEEEEEEE,.
JAY DEE FT DABO - FOREVER ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 5:55:00 PM
JAY DEE FT. DABO - FOREVER Pakua wimbo mpya kabisa kutoka kwa Lady Jay Dee na Dabo. Jay Dee amehama kidogo kutoka style yake ya kawaida ya Zouk Rhumba na kuimba wimbo huu katika style ya Reggae. Amemshirikisha mdogo wake Dabo ambaye ni mshindi wa tuzo ya KTMA best reggae artist wa Tanzania mwaka 2013.
PICHA MTIKISIKO 2014 - IRINGA ( Photos )
Posted by NAOMIKADUMA On 12:46:00 PM
KAMA ULIPITWA NA SHOW YA MTIKISIKO 2014, ILIOFANYIKA UWANJA WA SAMORA IRINGA USIKU WA TAREHE 22/11 KUAMKIA SIKU YA TARE 23/11. UNGANA NASI HAPA KUONA KILICHOJIRI HUKO KWANJIA YA PICHA MNATO ZAIDI YA .
SHOW HIO KUBWA INAYOFANYIKA NYANDA ZA JUU KUSINI KILA MWAKA MSIMU KAMA HUU, CHINI YA KITUO BORA CHA RADIO EBONY FM IRINGA. IMEKUA GUMZO SAANA KWA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KAMA SHUKRANI NA KUWAKUTANISHA WASIKILIZAJI WAKE WOTE WA MIKOA YA KUSINI PAMOJA, KWA KUPONGEZANA NAKUSHEREKEA. IMEKUA PIA IKIHUSISHA WANANII WAKUBWA MBALIMBALI TANZANIA, NA NJE YA TANZANIA. MFANO, WASANII WALOSHIRIKI KATIKA TAMASHA HILI BAADH, WALIKUA NI DIAMOND PLATNUMZ, KALA JEREMIA, T.I.D, LINEX, IZZO B, NAWENGINE WENGI, WAKISINDIKIZWA NA WASANII WACHANGA TOKA MIKOA YA KUSINI KAMA, MEDDA CLASSIC, OBBY, DEE GOSBA, MAC MC, NEMMY MC, NA WENGINE WENGI...
ZAIDI ENDELEA TIZAMA MAPICHA HAPA CHINI....
| IZZO B MTOTO WAMBEYA AKIFANYA YAKE. |
| KALA JEREMIAH PIA ALITISHA NAE |
| DJ NASS (kushoto) na EDDO BASHIR ( kulia ) WAKIAMSHA AMSHA KWA STAGE KAMA ILIVYO KAWAIDA YAO. |
| EDDO BASHIRI - ( mtangazaji Ebony FM ) AKIZIDI PAGAWAWISHA MASHABIKI, BAADA YA MIZUKA KUMPANDA. |
| MAMA LA MAMA AKIYARUDI JUKWAANI NAMIONDOKO YAPWANI |
| DIAMOND PLATNUMZ ALIEBEBWAJUU NA WACHEZAJI WAKE. |
| NAHUYU NDIO YULE MTOTO MEDDA CLASSIC ALIE MWANDIKIA BARUA DIAMOND, AKIWAKILISHA VYEMA. |
| T.I.D NAE HAKUA NYUMA KUONYESHA UKONGWE WAKE ALONAO KATIKA KIPAJI CHAKE CHAKUPAGAWISHA MASHABIKI. |
YOUNG KILLER Ft FID Q & BELLE 9 - 13 "Kumi na Tatu" ( New Video )
Posted by NAOMIKADUMA On 11:35:00 AM
Young Killer Ft Fid Q & Belle 9 - 13 (Kumi na Tatu) BONGE MOJA KICHUPA, KIKIWA KIMESIMAMIWA NA DR MTU MZIMA, NISHER ( VIDEO ) NA AUDIO CHINI YA MKONO WA P-FUNK MAJANI BONGO RECORDS ( AUDIO )
Saturday, November 22, 2014
ANGEL BENARD - MIMI NA YESU ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:24:00 PM
ANGEL BENARD - MIMI NA YESU Wimbo wa 5 wiki ya 5 Kati ya Nyimbo 10 zinazotakiwa ingia mtaani. Ni wimbo unaoelezea jinsi ambavyo Mungu ni ukamilifu wa maisha ya mwanadamu. Na hivyo hakuna cha kuogopa wala wa kumuogopa humu duniani. Kila kitu kimetoka kwa Mungu, kinapatikana kwake na mwisho wa siku tuna kila sababu ya kutoogopa na kukiri kwa ujasiri kuwa yote yanapatikana kwake. LYRICS MI NA YESU VERSE1 Bwana ni ngome yangu, wimbo wangu milele, uuuu... Bwana ni mwamba wanguu, sitaogopa kamwe, yeeaahh.. Bwana ni wokovu wangu, utukufu wangu, Bwana ni nguvu zangu, nimwogope nani... -- Bwana ni wokovu wangu, utukufu wangu, Bwana ndiye nguvu zangu, nimwogope nani yeaahh uuu nimwogope nani*2 CHORUS Mi na yesu tu*3 milele*3 VERSE2: Bwana ni tumaini langu, kimbilio milele, mmhhh Bwana ni uzima wangu, msaada ulio tele, yeehh uu Bwana ni mchungaji wangu, ni pumzi yangu, Bwana ni utajiri wangu, mimi nimwogope nani Bwana ni mchungaji wangu, ndiye pumzi yangu, Bwana ni utajiri wangu, nimwogope nani CHORUS Mi na Yesu tuuu*...
Thursday, November 20, 2014
WITNESZ TZ - CHUNGA MDOMO WAKO ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:51:00 PM
hi ninatumai uko poa my new song, hope utaipenda na kuisapoti, ninakaribisha maoni na maswali pamoja na interview kupitia 07171757582 Upendo tele Witnesz the fitnes
MAKOMANDO - SHERIKOKO ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:45:00 PM
KITU KIPYAA, KUINGIA MTAANI PUNDE KWA JINA LA "NITAPATA WAPI" ( Up Date Info )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:29:00 PM
Tuesday, November 18, 2014
IRINGA ALL STARS - R.I.P GEEZ MABOVU ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:45:00 PM
HUU NDIO WIMBO ULIOTENGENEZWA NA SAMPAMBA MUSIC - IRINGA CHINI YA PRODUCER MWASILE AKA SILEEY. NYIMBO HII IMETENGENEZWA NA WASANII WACHANGA TOKA IRINGA KAMA WAWAKILISHI WAWASANII WOTE WA IRINGA NA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KATIKA KUMUENZI MAREHEM GEEZ MABOVU BAADA YA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWA WASANII WACHA. NDANI ZIMEHUSIKA SAUTI ZA WASANII ZAIDI YA 13. UNGANA NASI HAPA KUUSIKILIZA WIMBO HUU.
picha za Location ya WITNESZ TZ - Chunga mdomo wako ( New video Comming soon )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:16:00 PM
hapa ni moja y location wakati tunarekodi video ya chunga mdomo wako, na ni video ya kwanza ya peke yangu kurekodi na wasichana tu[pu pia ni kati ya video queens walioo kwenye otchunes 20 video queens ambapo otchunes 20 ni kipindi cha tv kinchohusika na kutafuta na kuendeleza vipaji mbali mbali ikwemo ,muziki acting,video dancers,video queens wote wanapatikana wakihitajika hata sasa ambapo mara nyingi ilikua taabu sana kwangu mimi kupata wasichana ili washiriki nami kwenye music videos ila kwa sasa kwa kuwa ninao na ninawaandaa kmwenyewe ndo maana nimepata urahisi wa kuwatumia kwa mswali zaidi nicheki hewani 0717 757 75 82
DIAMOND AMPA SHAVU MEDA CLASSIC BAADA YA KUPATA BARUA YAKE ( Up Date Info )
Posted by NAOMIKADUMA On 5:46:00 PM
SIKU CHACHE BAADA YA VIDEO YA MSANII MEDA WA IRINGA IITWAYO BARUA KWA DIAMOND KUINGIA MTAANI, HATIMAE BARUA HIO IMEWEZA MFIKIA DIAMOND NA KUMFANYA AYASEME HAYA KUPITIA UKURASA WAKWE WA Twitter na Instagram " Kiukweli simfahamu, sijawahi hata kumuona wala kuzungumza nae. Na sio kwasababu eti kaniimba mimi, Hapana! Ila ni serious na uzuri wa kazi alioifanya ndivyo vimenifanya nione ni vizuri kumleta hapa wadau ili kwa pamoja tumsupport naye kesho na keshokutwa afikie malengo ya kaziyake na kua balozi mzuri wa nchi yetu kupitia Bongo Flavour. Huyu hapa anaitwa MEDA kutoka IRINGA." HIVYO NDIVYO ALIVYO ANDIKA DIAMOND. HUENDA OMBI LA MEDA LIKAFANIKIWA KWENYE BARUA HIO, MIMI NAWEWE HATUJUI. Endelea Kutembelea Ukurasa wetu kwamaInfo na mastory Zaidi...
Monday, November 17, 2014
MWASITI FT KINGZILLA - LEO ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:27:00 PM
Wimbo mpya kutoka kwa Mwasiti akimshirikisha Kingzilla. Wimbo unaitwa Leo. Pakua kwakuubofya hapa chini...
DULLY SKYES FT MAUNDA ZORRO - THAT'S THE WAY ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:26:00 PM
WALICHOKIFANYA EDDO BASHIRI NA DJ NAS MTIKISIKO MAKAMBAKO 2014 KWA MASHABIKI ( Up Date Info Video )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:13:00 PM
KAMA ULIMISI HUDHURIA SHOW YA MTIKISIKO MAKAMBAKO 2014, HIZI NDIZO KUFURU ZILIZOFANYWA KWA STAGE KATI YA EDDO BASHIRI,(MTANGAZAJI EBONY FM), NA DJ NAS, (DJ TOKA EBONY FM), DHIDI YA MASHABIKI WAO. NAN ALIFUNIKA? TIZAMA VIDEO HIO HAPO CHINI...
Sunday, November 16, 2014
ANGEL BENARD - HAVE YOUR WAY ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 12:00:00 PM
WIKI 10, NYIMBO 10 MPYA! Wimbo mpya wa 4 wa Angel Benard kutoka albam yake NEW DAY. Wimbo unaitwa HAVE YOUR WAY.
NAY WAMITEGO - AKADUMBA ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 11:51:00 AM
DARK MASTER ATANGAZA KUOKOKA RASMI BAADA YA KIFO CHA GEEZ MABOV. ( Exclussive Interview Na Nelly B - Nuru FM )
Posted by NAOMIKADUMA On 11:41:00 AM
Kipindi ; STREET BAMIZA Radio : NURU FM 93.5B IRINGA Host & Producer NELLY BE.. EXCLISSIVE INTERVIEW YA NELLY B NA DARK MASTER TOKA NURU FM IRINGA BAADA YA KIFO CHA MSANII GEEZ MABOVU ATANGAZA KUOKOKA. SIKILIZA HAPA CHINI.
MEDA - BARUA KWA DIAMOND ( New Video )
Posted by NAOMIKADUMA On 11:10:00 AM
ARTIST: MEDA SONG: BARUA KWA DIAMOND AUDIO: SAMPAMBA MUSIC VIDEO: NICLASS - IMAGENATION VIDEO LOCATION IMEFANYIKA IRINGA, AUDIO IRINGA. TIZAMA HAPA BONGE MOJA KICHUPA.
Subscribe to:
Posts (Atom)













.png)




















