KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Saturday, November 29, 2014

WILLIAM OTUCK - ZAWADI YA X - MASS ( New Audio Album )


Album mpya ya Krismasi! Huu ndiyo wimbo wa utambulisho kutoka kwa William Otuck: https://mkito.com/song/zawadi-ya-x-mas/4691 Album nzima inapatikana hapa: https://mkito.com/artist-profile/otuck-william/964 Krismasi hii, Santa hatokuwa akitoa zawadi peke yake. Na hata hivyo inaonekana kuwa baadhi watamzidi katika hilo linapokuja suala la muziki! Otuck William, muimbaji wa soul, athibitisha hilo kwa kuleta mbele yako bidhaa mpya itakayobadili sura nzima ya msimu wa Krismas mwaka huu kimuziki. Ni santuri itakayokuwa imebeba nyimbo kumi na tano (15) mahususi kabisa kwa ajili ya Krismas. Akizungumzia album hiyo Otuck anasema; "“Zawadi Ya Krismasi” ni album yenye nyimbo 15 iliyotayarishwa kwa ushirikiano wa kwangu mwenyewe na Nach B, mtayarishaji kutoka studio za Beats Bank Music zilizopo jijini Mbeya. Hii si album ya dini (Gospel) japokuwa imebeba baadhi ya nyimbo za zamani za kidini za Krismas, ambazo tumezitayarisha katika mahadhi tofauti kidogo, lakini ni album inayohusu Familia, Matumaini, Faraja, Imani na Upendo. Kwa kadri ya ufahamu wangu inaweza kuwa album ya kwanza kabisa ya Krismas kuwahi kutengenezwa Tanzania au Afrika Ya Mashariki kwa ujumla”. Ni wazi kwamba kila mtu anatamani kujua nini hasa Otuck ametuandalia, kitakachodumu kwa muda mrefu na kutufariji kila ifikapo msimu kama huu. Album hiyo itakuwa ikipatikana katika mtandao wa Mkito.com kuanzia Tar 26 Novemba 2014. Lakini pia itauzwa katika mfumo wa CD. Kwa mawasiliano zaidi ya namna ya kupata CD hizo au kuwa wakala wa usambazaji, andika barua pepe kwa otuckwilliam@gmail.com au piga simu nambari +255712168011

0 comments:

Post a Comment