KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Friday, October 31, 2014

JCB - MTOTO MKALI (New Song from JCB Comming Soon

HIVI PUNDE MSANII JCB MAKALLA TOKA ARUSHA, ANATARAJI TUA MTAANI NA MZIGO MPYA UTAKAO KWENDA KWA JINA LA MTOTO MKALI, CHINI YA PRODUCER DAZ NALEDGE TOKA WATENGWA RECORDS. WIMBOO HUU UNAZUNGUMZIA MAPENZ. USIKAE MBALI NA UKURASA WETU PUNDE UTAKAPO ACHIWA RASMI UTAUPATA HAPA HAPA. KARIBU...

ANGEL BENARD - SHUJAA ( New Audio )


Huu ni wimbo wa pili kutoka album mpya NEW DAY kutoka kwa Angel Benard - wimbo unaitwa SHUJAA. 

SHUJAA.
Kuna wakati katika maisha tunakutana na mambo magumu na hakuna wa kukutia moyo, kwa sababu wengi waliotuzunguka ni watu ambao mara nyingi hufurahi tunapoumia. Huu ni wimbo ambao mtu unajikumbusha mwenyewe juu ya uhalisia wa maisha na kasha unajikumbusha kwamba “you are the hero of your own soul”. Mungu ametuamini na mitiani ya maisha, hivyo na sisi tunakubali kupambana na kila hali hadi kufikia ndoto zetu hata kama huko njiani kuna vikwazo.

HISIA - GIMME A CALL - (New Audio)


Mshiriki wa Tusker Project Fame HISIA anakuja na kibao chake kipya GIMME A CALL ambacho amemshirikisha producer John Blass kutoka Grand Master Records. Hisia mwenye kipaji cha vocals ameonesha uwezo wake mkubwa katika hii track iliyopo katika miondoko ya Afro Soul. Wimbo ulitambulishwa rasmi katika concert iliyoandaliwa viwanja vya Alliance Francaise akisindikizwa na Grace Matata pamoja na kundi la H_art the Band kutoka nchini Kenya. HISIA - GIMME A CALL Vocals: Hisia Drums: Nelson Martin Mugarula Bass guitar: Kelvin Samuel Guitars: Goodlucks Sway, Mzee Francis, Hisia Keys: John Blass Written by: Hisia Music consultant: BR Marungi Instruments recorded at Fnouk Music Studios Co-arranged by Kelvin Samuel Produced by: John Blass - Grand Master Records

Friday, October 24, 2014

ANGEL BENARD - NEED YOU TO RAIGN ( New Audio )


Episode 01: NEED YOU TO REIGN by ANGEL BENARD Wimbo wa kwanza katika album ya NEW DAY kutoka kwa ANGEL BENARD "Need you to reign" ni wimbo unaomuomba Mungu awepo katika maisha yake na amuongoze katika kila jambo. Wimbo huu umerekodiwa Mujwahuki Studios chini ya Producer Mujwahuki mwenyewe. Producer huyu pia alishawahi kufanya kazi na msanii Ben Pol katika wimbo wake wa Nikikupata. Nyimbo zote katika album hii zimetungwa na kuimbwa na Angel Benard.

MWANA FA FT ALIKIBA - KIBOKO YANGU ( New Audio )


Sote tumeusubiri kwa hamu na sasa wimbo mpya kabisa wa Mwana FA na Alikiba umewasili rasmi. Baada ya Mwana FA kutoa wimbo wa Mfalme live katika tuzo za KTMA 2014 msanii huyu ameungana na mfalme wa bongo flava yaani Alikiba ili kuwaletea mashabiki wake kazi nyingine kali. Producer wa wimbo huu si mwingine bali ni Marco Chali wa kutoka MJ Records ya jijini Dar Es Salaam. Katika kuurekodi wimbo huu kumekuwa na matoleo manne tofauti ambayo wadau walikuwa wakisindwa kuamua ni upi wa kuachia kwa kuwa zote zimesimamia kucha. Mwana FA na kampuni ya LifeLine ambaye yeye pia ni mkurugenzi wameamua kuuachia wimbo huu moja kwa moja kupitia Mkito.com ili kuhakikisha unawafikia wapenzi wake wengi zaidi na kuhakikisha kuwa kuna maslahi yanapatikana katika kazi hii. Pakua wimbo huu mpya kabisa sasa upate flava kali.

DENNIS DRAZZY - CHEZA ( New Audio )






CHEZA is a song performed and written by a young Upcoming artist from Tanzania, Dennis Drazzy (22) who does Rap with a twist. The song which is recorded and mastered at Hebron Studios and mixes elements of House music, pop and rap all in one resulting to a Rap House genre and is from the Black & White mixtape coming in 2015.

MAD ICE - EVERYTHING I DO ( New Audio )


Mad Ice ni msanii aliyezaliwa nchini Uganda na kuishi Tanzania kwa muda mrefu ambapo aliaanza rasmi kazi yake ya muziki na kutoa albam yake ya utmbulisho iitwayo BABY GAL (2003, Chini ya Miikka Mwamba). Msanii huyu wa Afro-Soul baada ya album hiyo alihamia nchini Finland ambapo aliendeleza kazi pamoja na producer Miikka Mwamba na studio nyingine nchini humo na kutoa nyimbo nyingi zilizoshika chati tofauti duniani kote zikiwemo Maneno, Mapaenzi Sumu na Te Amo. Single mpya kabisa ya Mad Ice inaitwa EVERYTHING I DO na imefanyika Sonic Pump Studios, Finland chini ya producer DJ Hermanni.

TIZAMA PICHA 5 ZA UJIO WA MAD ICE NA TOKA MOJA YA STUDIO KUBWA DUNIANI ( Up Date Info )







Mwanamuziki Mad Ice amerudi Tanzania kutoka nchini Finland ambapo ametoka kurekodi single yake mpya EVERYTHING I DO chini ya producer DJ Hermanni kwenye studio ya kimataifa ya Sonic Pump Studios (http://www.sonicpumpstudios.com/). Mara nyingine huwa inatosha kuangalia mandhari ya studio kujua kuwa kazi zinazotoka huko lazima ziwe na kiwango cha kimataifa. Tazama picha hizi za studio halafu tusubiri kusikia mapishi yake Jumatatu tarehe 20 Oktoka.

ANGEL BENARD - 10 SONGS 10 WEEKS ( UpDate Info )



ANGEL BENARD ni jina ambalo limekuwa likisikika kwa miaka kadhaa sasa kwenye ulimwengu wa muziki wa gospel. Angel Benard mwenye miaka 25 hatimaye sasa anaachia album yake NEW DAY kwenye mfumo wa digitali kupitia Mkito.com. Watu wengi wamekuwa wakisubiri kusikia nyimbo zake za zamani lakini haikuwa rahisi kuzipata. Album hii ni album ya 3 ya mwana dada huyu mwenye sauti ya maajabu. Ni wasanii wachache sana wa muziki wa gospel ambao wamefanikiwa kuvusha nyimbo zao zikapendwa na wapenzi wa gospel pamoja na wapenzi wa muziki wa bongo flava, RnB n.k. na mwimbaji huyu ni mmoja wapo. Katika kuitambulisha album hii Angel Benard ataachia wimbo mmoja kila siku ya Alhamis kwa wiki 10 mfululizo. Wimbo wa kwanza utatoka tarehe 23 October na unaitwa NEED YOU TO REIGN ukiwa katika minodoko ya Reggae.

HISIA - MAWAZO ( Vocal of New Audio )

Msanii Hisia ambaye aliiwakilisha vyema sana nchi yetu katika mashindano ya Tusker Project Fame mwaka jana anakaribia kuachia wimbo wake mpya uitwao GIVE ME A CALL hapo tarehe 25 Octoba katika show ya live. Katika kuusubiri wimbo huo tujikumbushe track yake ambayo imeshika chati nchini Kenya kwa wiki 6 mfululizo iitwayo MAWAZO. Wimbo huu pia unapatikana kama acapella, yaani vocal tu, ili wapenzi wake tusikie ni kwanini Hisia aliweza kufanya vizuri vile kwenye mashindano ya Tusker Project Fame. Kwa wale wote watakao taka kufika kwenye show yake itafanyika tarehe 25/10/2014 Alliance Francaise kuanzia saa moja jioni.

BRAND NEW MKUBWA NA WANAWE - INOOH (Audio)


Wimbo mpya kutoka kwa Mkubwa na Wanawe ambao ni kati ya nyimbo zilizopo kwenye collection ya NISEME. Wimbo huu inaitwa INOOH. Mkubwa na Wanawe ni wansanii ambao kwa muda mfupi sana wameweza kuonekana katika majukwaa makubwa na kuwa na mafanikio makubwa sana kimuziki wakiwa chini ya usimamizi wa Mkubwa mwenyewe Saidi Fela. Fela ni meneja ambaye amesimamia na kuwatoa wasanii na makundi kama Juma Nature na Wanaume. Pata wimbo mpya kabisa kutoka kwa Mkubwa na Wanawe kupitia Mkito.com sasa.

Thursday, October 16, 2014

JOETT FT G FULLAH & LEVEL ONE - I'm gonna live forever ( New Audio )

PRESS RELEASE
Joett Aachia Singo Mpya Akishirikisha Wasanii wa Bongo Flava G Fullah na Level One
Mwalimu wa kuimba na msanii wa ku-rekodi miondoko ya pop – Joett, anaachia singo yake mpya I’m Gonna Live Forever Octoba 13 2014, ambayo amewashirikisha wasanii wa bongo flava G Fullah na kundi la vijana wa kiume (boyband) lijulikanalo kama Level One. Voko za trak hii zilirekodiwa na Max Rioba pale Authentic Records, Dar es salaam, na kuandaliwa na producer mahiri nchini Uingereza, Patrick Jonsson, ambae amefanya kazi na Joett kwa kipindi kirefu. Mixing pamoja na mastering ya trak hiyo imefanyika na sound engineer na producer King Penn (KP), wa Atlanta, Marekani,  ambae amefanya kazi na lebo ya Madonna ijulikanayo kama Maverick; Warner Bros, EMI, Beyonce, Solange, Columbia, 50 Cent, John Lennon Songwriters, MCA, The Big Boy Records, Def Jam, Dallas Austin, na mamia ya wasanii wa lebo ndogo zijuliakanazo kama Indie Labels. Joett, ambae hutoa singo moja tu kwa mawaka, aliamua kuwashirikisha vijana hawa ili kuwapa fursa ya kutoka katika viwango vya kimataifa, na amedhamiria kuendelea kufanya hivyo kwa miaka ijayo. “Ningependa sana kukuza vijana katika tasnia hii ya mziki, na hasa kuwashukuru mashabik pamoja na wadau wa mziki kwa ushirikiano wao enedelevu,” alisema Joett.
G Fullah alinyakuliwa na Joett toka kipindi cha ITV Hawavumi Lakini Wamo; Abdul Kagoi toka Epiq Bongo Star Search 2013; Rahym alitambulishwa kwa Joett na kaka yake, msanii wa bongo flava Mbongo Halisi, nakuchukuliwa na Joett kufundishwa kuimba. Nixon alidhaminiwa na mama yake kufundishwa sauti kwa Joett, alafu baadae Joett akamweka kwenye program yake ya misaada kwa wasanii chipukizi na hatimae kummpa mkataba wa ku-rekodi chini ya lebo yake – Joett Music. Kikundi cha Level One ni Abdul, Rahym na Nixon.
Kwa bahati mbaya, G Fullah alifariki asubuhi ya Jumapili tarehe 5 October 2014. “Habari za kifo chake zimenishtua na kuleta huzuni kubwa sana kwenye moyo wangu. Nilikua na mipango mikubwa kwa G Fullah katika tasnia hii ya muziki. Alikua ni mtu mzuri sana. Tutamkumbuka milele, Mungu ailaze roho yake pahali pema,” alisema Joett.

Sunday, October 12, 2014

LIL STIGGAR - MIXTAPE ( RISE AND SHINE )

MSANII MKALI WAMIONDOKO YA HIPHOP KWA AKINA DADA TOKA MBEYA - TANZANIA SASA KATUA NA MIX TAPE YAKE MTAAN IITWAYO RISE AND SHINE (VIDEO). MWANADADA HUYU AMBAYE KWASASA ANAJULIKANA KWA JINA LA LIL STIGGAR AKA QUEEN OF HIPHOP AMEJIZOLEA SAANA UMAARUFU HIVI KARIBUNI BAADA YA NYIMBO YAKE INAYOKWENDA KWA JINA LA "YES I CAN" KUANZA CHEZWA MPAKA MOJA YA VITUO VIKUBWA VYA TV DUNIANI MTV BASE. KWASASA PIA ANATAMBA NA KIBAOCHAKE KIPYA MTAANI KIJULIKANACHO NKAMA "NATAFUTA KIKI",ALICHO MSHIRIKISHA QUEEN DARLIN & NASH DESIGNER, NA KINGINE KIITWACO "LIKE". KUIPATA MIX TAPE HIO WASILIANA NA NAMBA HII POPOTE ULIPO 0654079930 KUIPATA KWA TSH 5000/- TU.

HABARI NJEMA KWA WANAMUZIKI WOTE TANZANIA. ( Up Date Info )

Habari, Tunayofuraha ya kukukaribisha kuanza kutumia Widget mpya ya Mkito.com kwaajili ya kuuza nyimbo zako kwa wasanii wote Tanzania. Tofauti na Widget za Hulkshare na SoundCloud, kwa kutumia widget ya Mkito.com utalipwa kwa kila download itakayo pitia katika blog yetu. Malipo ni kama ifuatayvo: Msanii = 60% Mkito.com = 32% Blogger = 8% Jumla = 100% Blog yako hii ya selengakaduma, imeamua jiunga rasmi na mtandao huu wa Mkito.com kuanzia tar 11/10/2014 ili kuweza kuwanufaisha zaidi wasanii kwa kazi zao wanazo fanya,kwa kila Download itakayofanyika ya wimbo wake utakao kua katika mtandao wetu. Malipo yamezingatia zaidi maslahi ya msanii, kama ulivyoweza ona mpangilio wamalipo hapo juu. Kwa maoni na ushauri,zaidi waweza tembelea mtandao wa mkito.com ama 0767 769 921 au tuandikie kupitia info@mkito.com USIPOTEZE BAHATI HII KAMA MWANAMUZIKI, KUWA WAKWANZA KUNUFAIKA NA KAZI ZAKO. ASANTE KWAKUTEMBELEA UKURASA WETU. NA KARIBU TENA.

Saturday, October 11, 2014

KHALID CHOKORAA FT MSAGA SUMU - MANENO ( New Audio )

Msanii Khalid Chokoraa ambaye pia ni bondia wa kulipwa anakuletea track yake mpya Maneno amabapo amemshirikisha mzee wa Kigodoro a.k.a Msaga Sumu. Hii ni colabo ambayo siyo ya kawaida lakini matokeo yake yamekuwa ni mazuri kupindukia. Download wimbo mpya sasa.

Tuesday, October 7, 2014

Wednesday, October 1, 2014

LIL STIGGAR FT QUEEN DARLEEN & NASH DESIGNER - ANATAFUTA KICK ( NEW AUDIO Comming Soon )


UJIO MPYA WA MWANADADA LIL STIGGAR - MKALI WA MIONDOKO YA HIP HOP KWA WANADADA, MIKOA YAKUSINI, MASAA MACHACHE BAADAE ANATARAJI TUA MTAANI NA TRACK YAKE MPYA IITWAYO "ANATAFUTA KICK" ALOMSHIRIKISHA Queen Darleen & Nash Designer INAYOTARAJIWA FANYA MAPINDUZI ZAID YA TRACK YAKE YASASA AMBAYO INACHEZWA MPAKA MTV BASE. KAMA WADAU ANAOMBA SUPPORT YENU SOON ITAKAVYO TUA MTAANI TRACK HIO. ZAIDI ITAPATIKANA HAPA HAPA, USISITE KUTEMBELEA UKURASA WETU KUIPATA TRACK HIO.