PRESS RELEASE
Joett Aachia Singo Mpya
Akishirikisha Wasanii wa Bongo Flava G Fullah na Level One
Mwalimu wa kuimba na msanii wa ku-rekodi miondoko ya pop –
Joett, anaachia singo yake mpya I’m Gonna Live Forever Octoba 13 2014, ambayo
amewashirikisha wasanii wa bongo flava G Fullah na kundi la vijana wa kiume
(boyband) lijulikanalo kama Level One. Voko za trak hii zilirekodiwa na Max
Rioba pale Authentic Records, Dar es salaam, na kuandaliwa na producer mahiri
nchini Uingereza, Patrick Jonsson, ambae amefanya kazi na Joett kwa kipindi
kirefu. Mixing pamoja na mastering ya trak hiyo imefanyika na sound engineer na
producer King Penn (KP), wa Atlanta, Marekani, ambae amefanya kazi na lebo ya Madonna
ijulikanayo kama Maverick; Warner Bros, EMI, Beyonce, Solange, Columbia, 50
Cent, John Lennon Songwriters, MCA, The Big Boy Records, Def Jam, Dallas
Austin, na mamia ya wasanii wa lebo ndogo zijuliakanazo kama Indie Labels. Joett,
ambae hutoa singo moja tu kwa mawaka, aliamua kuwashirikisha vijana hawa ili
kuwapa fursa ya kutoka katika viwango vya kimataifa, na amedhamiria kuendelea
kufanya hivyo kwa miaka ijayo. “Ningependa sana kukuza vijana katika tasnia hii
ya mziki, na hasa kuwashukuru mashabik pamoja na wadau wa mziki kwa ushirikiano
wao enedelevu,” alisema Joett.
G Fullah alinyakuliwa na Joett toka kipindi cha ITV Hawavumi
Lakini Wamo; Abdul Kagoi toka Epiq Bongo Star Search 2013; Rahym alitambulishwa
kwa Joett na kaka yake, msanii wa bongo flava Mbongo Halisi, nakuchukuliwa na
Joett kufundishwa kuimba. Nixon alidhaminiwa na mama yake kufundishwa sauti kwa
Joett, alafu baadae Joett akamweka kwenye program yake ya misaada kwa wasanii
chipukizi na hatimae kummpa mkataba wa ku-rekodi chini ya lebo yake – Joett Music.
Kikundi cha Level One ni Abdul, Rahym na Nixon.
Kwa bahati mbaya, G Fullah alifariki asubuhi ya Jumapili
tarehe 5 October 2014. “Habari za kifo chake zimenishtua na kuleta huzuni kubwa
sana kwenye moyo wangu. Nilikua na mipango mikubwa kwa G Fullah katika tasnia
hii ya muziki. Alikua ni mtu mzuri sana. Tutamkumbuka milele, Mungu ailaze roho
yake pahali pema,” alisema Joett.
0 comments:
Post a Comment