NEWS: Fire Star, Mac Mc watwaa tuzo KVOOS Multimedia 2015
Orodha ya washindi wa tuzo za KVOOS 2015
Wasanii chipukizi wa muziki wa bongo flava nchini, Mac Mc na Fire Star wamefanikiwa kutwaa tuzo za KVOOS Multimedia Awards zilizotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita Msasani jijini Dar es Salaam.
Wasanii hao wametwaa tuzo hizo huku fire star akitwaa katika kipengele cha Best Upcoming Music Song kupitia wimbo wake ‘She is Beautiful’ huku washindi wengine wakiwa ni Producer P, Zungu la Floo na Myself ambapo Appliciation award imeenda kwa Mac MC.
KVOOS Multimedia imetoa tuzo hizo ikiwa ni katika jitahada zake za kuinua vipaji vya wasanii wachanga wa muziki wa bongo flava kwani washindi wa tuzo hizo watapata fulsa ya kusambaziwa kazi zao bure na kampuni hiyo.
Tuzo za KVOOS zilianza rasmi January 15, 2015 ambapo zoezi la upigaji kura lilianza kukiwa na vipengele vinavyohusisha muziki wa Hip Hop video na Audio pia Bongo flava kwa Video na Audio ambapo zoezi la kupiga kura lilikamilika March 29, 2015 ambapo zoezi la upigaji kura lilisitishwa na wasanii hao kuibuka washindi.
Katika hatua nyingine Fire Star na Mac Mc wametoa shukrani zao za dhati kwa KVOOS kwa kuwathamini wasanii wachanga na kuwapa nafasi ya kushindania tuzo kama hizo walizotwaa huku akitoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa KVOOS.
0 comments:
Post a Comment