RISALA NA HISTORIA FUPI YA UMMOJA WA VIJANA IRINGA KWA WAGENI WAALIKWA. 03.08.2014 MAFINGA - IRINGA Mheshimiwa mgeni mkuu wa wilaya ya mufindi evarista kalalu. Wageni waalikwa Katibu wa ccm wilaya mufindi-miraj mtaturu Afisa maendeleo ya vijana wilaya-juma fuluge Mjumbe wa halmashauri kuu ccm-marcelina mkini Kaimu meneja waa benki ya mucoba-eliter maalangalila Mshauri wa umoja huu dr yahaya Msigwa UTANGULIZI Mheshimiwa mgeni rasmi, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia afya njema nakuweza kutukutanisha leo katika sikuu hii muhimu,awali ya yote nikupongeze kwa kukubali Ombi letu la kuwa Mgeni rasmi,Tunaimani una mambo mengi yakufanya ila ukapendezwa kuungana nasi katika uzinduzi huu, kwa niaba ya vijana WEnzangu nasema Ahsante na MUNGU AKUBARIKI niwapongeze pia vijana wenzangu wote kwa ujumla kwa kukubali kuundwa kwa umoja huu ili kuwa chombo cha mabadiliko chanya hasa katika kutetea maslahi na haki za vijana,. Mheshimiwa Mgeni Rasmi,Nianze kwa historia fupi mpaka leo tupo hapa,safari yakuanzisha umoja huu ilianza miezi nane iliyopita kwa kupita wilaya zote za Mkoa wa Iringa nakukutana na vijana wenzetu na kuwaelezea lengo lakuunda umoja huu ili kutengeneza mfumo ambao ndio msingi mkuu wa kuweza kutimiza ndoto zetu. ,Mheshimiwa Mgeni rasmi tungeweza kufanya kwa uchache wetu lakini tukaona ni vema kuwashirikisha wenzetu ili tuwe na nguvu ya pamoja,tulisisitiza umoja huu ni wetu sote hakuna kizuizi chochote kinachoweza kutukwamisha kwa malengo tuliojiwekea, tuliamini kila jambo lina changamoto zake na safari yeyote haiwezi kukosa vikwazo lakini yote tumevuka na leo na leo unauzindua rasmi Umoja wetu Mheshimiwa Mgeni Rasmi,umoja una jumla ya wanachama hai 970 ndani yake kuna wanachama waanzilishi,wanachama wa mkataba,wanachama wa kujiunga na wanachama wa heshima,ndani ya umoja tumeunda makundi matano kutokana na jografia mahali husika makundi hayo ni MUZIKI,FILAM,UJASILIAMALI,KILIMO,UFUGAJI,NA MICHEZO Mheshimiwa mgeni rasmi tuna mengi yakuyafanya lakini kwa kuanza tumeamua yafuatayoyafuatayo 1-kuanzisha mfuko wa kuweka na kukopa ambao utaitwa Vijana Iringa Vicoba mfuko huu utasaidia wanachama wetu kuweza kujiendelezaa kiuchumi. Na kuweza kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo 2-kuanzisha mfuko wa dharula aambao utakuwa wakusaidiana katika shida na rahaa na utalenga kusaidia mwanachama na familia yake kuu. 3-kuanzisha mfuko wa kukuza,kuendeleza na kusaidia wasanina paamoja ni michezo mbali mbali ukiwemo mpira wa miguu,pete,riadha nk. 4-kuanzisha kituo cha Michezo ambacho kitakuwa kikisimamiana kukuza vipaji vya vijana kuanziaa miaka 14-25 kwa mpira wa mguu VIJANA IRINGA FOOTBAL ACADEMY 5-kuanzisha kitua cha ambacho kitasimamiaa na kukuza vipaji vya wasanii muziki na filamu na kutoa elimu juu ya sanaa yaani IRINGA HOUSE OF TALENT. 6-kuanzisha kituo cha cha elimu kwa vijana ambacho kitaitwaa VIJANA IRINGA CENTRE,Kituo kitatoa elimu ya ujasiriamal,vita dhidi ya maadui watatu wa maendeleo ambao ni UJINGA,MARADHI na UMASIKINI,kutoa elimu juu ya kupinga matumiz ya madawa ya kulevya na elimu juu ya uzalendo wa ujenzi wa taifa letu na haswa kuhamasisha vijana katika kuipenda nchi yao. Mheshimiwa Mgeni rasmi, Tumedhamiria kufanya jambo ambalo litakuwa ni mfano wa kuigwa kwa jamii inayotuzunguka maana wahenga wanasema kuiga chema si dhambi nasi tunataka kuiga mema ili tuwe mfano bora kwa kizazi hiki na vizazi vijavyoi, tunaamini fursa za kujikomboa kimaendeleo ni nyingi bila jitihada zetu itabaki kuwa ndoto na historia na zaidi tukabaki kuwa walalamikaji na kujiingiza katika makundi hatarishi. Mheshimiwa Mgeni Rasmi ,tunazo siku 60 katika kuyatekeleza malengo yetu,Kupitia umoja huu tunataraji utakuwa mkombozi wetu kwa kutengeneza fursa ya ajira ambayo imekuwa changamoto kubwa si kwa nchi yetu tu bali dunia kwa ujumla tunataraji kupitia umoja huu vijana watajiajiri na sio kutegemea kuajiliwa kama ilivyo kauli mbiu yetu GEUZA KIPAJI KUWA AJIRA RASMI. . Mwisho Mheshimiw a mgeni rasmi kwa sasa nchi ipo katika mchakato wakutafuta katiba mpya na tumeshuhudida mengi yakijitokeza katika bunge la awali la kati wahenga wanasema yaliyopitaa si ndwele tgange yajayo kwa maneno hayo tunawaoma umoja wa katiba ukawaa warejee ili kuweza kuweka maridhiano ya upatikanaji wa ka tiba mpya,umoja wetu unaamini Ni jukumu la kila kiongozi kuongozwa na busara na kumwogopa mwenyezi MUNGU kwa kuwa kila mtanzania wa sasa atapenda kuwe na mabadiliko ambayo yatasaidia vizazi na vizazi. Hivyo katiba ya nchi ni muhimu katika kufikia maendeleo yanayohitajika na sisi vijana mkoa wa Iringa tunaomba sana salamu zetu utufikishie katika ngazi husika kwa kuwa kila mzalendo wa kweli hawezi kubishana na mawazo ya watanzania katika kufanikisha katiba mpya. Kwa kumalizia nakushukuru sana kwa kuweza kujumuika na sisi vijana katika tamasha hili na MUNGU akubariki sana katika kutekeleza majukumu yako na ya kiserikali. Sisi UMOJA WA VIJANA IRINGA (UVI)tuta hakikisha tunahamasisha vijana wote kupiga kura kwani kura ni haki ya kila mwananchi na tunaamini kuwa kupitia umoja huu vijana wengi watajitokeza kupiga kura. Napenda pia kuwakumbusha vijana wenzangu kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura unaotarajia kuanza mapema na kujitokeza katika kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa. MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA MUNGU UBARIKI MKOA WETU WA IRINGA. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA…… 03/08/2014
Monday, August 4, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment