KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Saturday, March 29, 2014

Dee Gozba on LOCATION. (UP DATE NEWS)

Up coming mkari toka Mafinga Iringa Tayari Kisha ingia Location Kufanya video ya track yake Kama wewe chini ya Alama Xp Production.

Video hio Imefanyiwa location Dar na Dr Tenya Brown wa Alama Xp Production. Punde inataraji Ingia Mtaa. Utakua wakwanza kujuzwa na kuiona hapa hapa punde itakapo toka, endapo kama utakua ukitemblea ukurasa wetu huu mara kwa mara. Hizi picha ni baadhi ya picha zilizopigwa toka lokation ya video hio.

Thursday, March 27, 2014

Emmo da pro - My Body (NEW AUDIO)

New New New and Classic Joint from artist : Emmo Da Pro known as My Body, Noma saana hii Joint aisee. Kama hujapata time ya kuisikiliza ndo wakati wako sasa hapa hapa, kwenye ukurasa wetu. Iringa Stand Upppppppppppppppppppp. Sharaut kwa Emmo da pro kwa kuachia Joint ya moto na Next level kama hiii. Ukiisikiliza utaungana nami kwa niyasemayo. Support yako ndo kila kitu. KARIBU.

Mpili Square - Sina Dough (NEW VIDEO)

Mpili Square nia artist mpya toka iringa, kashuka na track iitwayo SINA DOUGH ilofanywa na Rebith corporation chini ya Dr Kagusa Adrew. Iringa na mikoa ya kusini inazidi kua siku hadi siku kwa sanaa ya muziki. Big Up Kagusa chini ya Rebith Corporation kwa video saafi. SUPPORT YAKO NDO KILA KITU MDAU.

Tuesday, March 25, 2014

SAMPAMBA ft MKWAWA, OB, GARDEE, RASCO J, CLOUD 9, JACK MEDIA, JOSH KILLER, MWENENDOX, MAC & MABAWA - KARIBU IRINGA (NEW AUDIO)


KARIBU IRINGA NI TRACK ILIYO FANYIKA CHINI YA SAMPAMBA MUIC INAYOZUNGUMZIA MJI WA IRINGA NA KUITANGAZA IRINGA DUNIANI KWOTE. TRACK HII WAMESHIRIKA WASANII ZAIDI YA 10 KAMA IFUATAVYO, SAMPAMBA ft MKWAWA, OB, GARDEE, RASCO J, CLOUD 9, JACK MEDIA, JOSH KILLER, MWENENDOX, MAC & MABAWA - KARIBU IRINGA

MWAGITO TOKA MAFINGA YATUA NJOMBE RASMI (COMMEDY)

Serious Comedy iliyofanyika Mafinga Chini ya Alama Xp Production sasa yaingia Mkoa mpya Njombe kwa bei ya 5000/- tu. Mi nisha daka nakala yangu tayar kama njia yakuunga mkono harakati za kuendeleza vipaji Mikoa ya kusini.

Masaa zaidi ya 02 yenye ujazo wa kutosha ndani ya CD Moja tu yatakufanya Ujifunze na kuburudika pia. Kama unahitaji nakala yako sasa Piga sim namba 0767 46 8484 or 0712 69 5805 au unaweza wasiliana nasi pia kupitia mail ya selengakaduma@gmail.com KUA MZALENDO ANZA NA NYUMBANI KWANZA KUKUUZA VIPAJI VYA WATOTO WA MIKOA YA KUSINI.

STANNA - The Best rapper from Mbeya, (News)

Add caption
Rapper mkali kwa miondoko ya Hip hop toka Mbeya na Mkali wao kama supper Nyota 2013 toka Mbeya, anaefanya vizuri zaidi saana katika Musi. Hayo yameweza dhihirika baada ya wasanii wakubwa kama Young D, Izzo B, Dully, Madee na wengine kibao kuonyesha kushtusha saana na uwezo wake kwenye gem na kumkubali pia, zaidi unaweza skiliza track iitwayo Rap, ili kujua uwezo wake zaidi. Punde anataraji tua na mzigo mpya. Hapa hapa utasomeka kama kawa.

Monday, March 24, 2014

Saturday, March 22, 2014

Friday, March 21, 2014

Sunday, March 9, 2014

MKULIMA COLLEGE - Tamthilia Toka Alama Xp Production. !!!COMMING SOON!!!

TAMTHILIA ILIO TENGENEZEA MAZINGIRA YA IRINGA INAKUJIA HIVI PUNDE TOKA ALAMA XP PRODUCTION (Dr Tenya Brown) INAFUNDISHA, INAELIMISHA, INABURUDISHA, INASISIMU NA PIA IMETAWALIWA NA UHALISIA WA MAZINGIRA YA MTANZANIA. (Mama Matha - Mafinga) Pichani.
MOJA YA LOCATION ZILIZOPO KWENYE TAMTHILIA HIO. (Dogo Scopy aka Fresh Andy Akiwa Location Pia)

TIZAMA TRAILER YA TAMTHILIA YA MKULIMA HAPA.

KOMEDI MPYA TOKA MAFINGA (Alama Xp Production) -MWAGITO

COMEDY MPYA TOKA MAFINGA IRINGA CHINI YA ALAMA XP  PRODUCTION Dr (Tenya Brown ) IITWAYO MWAGITO. BONGE MOJA COMEDY INAYOCHEKESHA NA KUFUNDISHA PIA. HIVI PUNDE ITAANZA TUA MTAANI KWA BEI PWAAA KABISAAA.

TAYARI NAKALA ZISHAANZA FOTOLEWA. ANDAA TSH 5000 TU KUPATA NAKALA YAKO. KWA MAONI USHAURI NA KUHITAJI BEI ZA JUMLA, CHUKUA NAMBA KWENYE POSTERS HAPO JUU AMA TUTUMIE HAPA selengakaduma@gmail.com

SIDE BALLO - JICHUNGE

SIDE BALLO NI ARTIST MPYA IRINGA TOWN KATIKA GEMU YA MUSIKI, AMBAE KWASASA ANADHAMINIWA NA UONGOZI WA MIALE SANAA GROUP ULIOPO CHINI YA KHAMIS NURDIN. VIDEO HII NI VIDEO ZA MWANZO KABISA KUFANYWA NA REBIRTH CORPORATION- CHINI YA KAGUSA aliekua kazoeleka kwenye Audio Production. Chungulia Video Hio taaaaam hapa.

Sunday, March 2, 2014

LONKA KUINGIA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA TUZO ZA KTMA 2014

LONKA NI ARTIST TOKA IRINGA ANAEFANYA VIZURI SAANA KATIKA TASNIA YA MUSIC DAR NA TANZANIA KWA UJUMLA. HII IMEDHIHIRIKA BAADA YA KUPATA CHANCE YA KUINGIA KWENYE NOMINATION ZA TUZO ZA KILL MUSIC AWARDS MWAKA 2014, KWA KUINGIA NA WIMBA WA HAKUNA MATATA KAMA WIMBO BORA WA RAGGAE. HIVYO MDAU UNAOMBWA SAANA SUPPORT YAKO KATIKA KUMPIGIA KURA MSANII HUYU ILI AWEZE KUTUWAKILISHA VYEMA NYANDA ZA JUU KUSINI KATIKA RAGGAE. KUMPIGIA KURA ANDIKA 04 LONKA HAKUNA MATATA THE TUMA KWENDA NAMBA 15440 KWA NJIA YA SIMU. AU WAWEZA TEMBELEA www.kilitime.co.tz/ktma

Saturday, March 1, 2014

La - Parte JIONEE MWENYEWE NIGHT CLUB BORA NYANDA ZA JUU KUSINI NA TANZANIA KWA UJUMLA.

Hii ndio Night Club Bora kwa sasa Tanzania Inayopatikana Iringa, Ambayo Imezinduliwa Rasmi tar 14/02/2014 Siku ijulikanayo kama Valentine Day. Club Hii tangu izinduliwe na Kuanza kazi Rasmi Imejizolea Umaarufu Mkubwa kutoka kwa wadau na Raia Mbalimbali.
Huu ndio Muonekano wa Nje wa club La - Parte Ambayo Ipo Chini ya Ebony Entertainment, Inayomilikiwa Na Mr Mfugale.
Hapa Ndio Lango la kuingilia ndani ya Club Hio. Twende Ndani Ukajionee mwenyewe.
Hii ndio sehemu ya kwanza na Counter ya kwanza unapoingia tu kati ya Tatu zilizomo ndani Humo. Aibu Manzeeeee.
Wakati nilipo pata nafasi ya Kuitembelea, ndipo nilipo Data na Counter hio na kuamua japo tokelezea tuu kwa mbele hata kama nlishindwa kalia vizuri sturi za humo ndani Pengine Yawezakana ilikua kuduwaa tuu.
Hii ni moja ya Kumbi zilizomo humo ndani ambayo pia Ilinidatisha kwa kua na sakafu ya Kioo kama Unapoiona hapo na yenye taa kwa Chini. Kufuru Aiseeeee, Nlibaki nimeduwaaaaa coz nimezoea kuona vioo madirishani na sio sakafuni.
Upekuzi haukuishia hapo tuu niliingia mpaka maliwatoni kujionea mwenyewe, Huku nako ilikua balaa tuu kama unavyoona, Bombazakunawa mikono hazina koki, ila ukisogeza tuu mikono zinatoa maji, na utakapotoa mikono zinakata zenyewe. TV Flat Screen Ipo pia mpaka chooni, Zaidi tembelea mwenyewe kajionee.
Baada ya hapo nlipata time ya kutembezwa kumbi nyingine ya ghorofan Ambayo ni Red Carpet.
Hapa nlikua ngazini nilielekea Ukumbi wa ghorofani ambao ni Red Carpet.
Manzee, Sikuamini machoyangu nilio yaona Huko. Kweli Ilikua Red Carpet na Kuna Kaunter nyingine pia, projector na TV Kubwa Flat screen.
Burudani pia kama kawa zipo wanapiga mpaka Live Band, Nilikutana na Drums humo humo nikaamua tokelezeaa nayo. Kuyasadiki haya Tembelea Mwenyewe kajionee na sio kusimuliwa, kama nlivyo tembelea mwenyewe. Nimeingia Club Nyingi lakini hii ni  Funiko. Shukrani Ziwaende Mmiliki wa club Ndugu Mfugale, Ebony Entertainment, Emmo Da Pro' Pamoja na Eddo Bashir kwa kuweza nifanikishia Jionea maajabu haya. Kwa maoni Ushauri karibu hapa selengakaduma@gmail.com

BIG JOFF, RASCO J, & JESSEY - TROUBLE

TOKA BATU MUSIC IRINGA, ARTIST WATATU WASIMAMA NA KUFANYA TRACK MOJA INAYOKWENDA KWA JINA LA TROUBLE, CHINI YA  PRODUCER GERALD, ARTISI HAO NI BIG JOFF, RASCO J NA JESSEY. BIG UP KWAO KWAKUA NI KAZI NZURI SAANA. WANAOMBA SUPPORT YENU KAMA WADAU. KWA MAONI ZAIDI UNAWEZA KUTUTUMIA HAPA selengakaduma@gmail.com