HATIMAE CHID BENZ AACHIWA HURU NA MAHAKA KWA KESI YA MADAWA YAKULEVYA.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Jana imemwachia mwanamuziki Rashid Makwilo 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya sh. 900,000 kufuatia kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya. ChidBenz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyere Jijini Dar es Salaam akiwa na madawa yakulevya aina ya bangi na Heroin. Mwanamuziki huyo ambae alikiri kosa hilo wiki ilio pita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa amejitayarisha kupanda ndege kwenda Jijini Mbeya kwenye Tamasha la Muziki. Sasa CHID BENZ kawa HURU kuanzia tarehe 26/02/2015 baada ya mahakama kutoa hukumu ya kifungo cha miaka Miwili jela, ama kutakiwa lipa fain ya pesa taslim Tsh 900,000/= Ambayo ililipwa mara moja nakumfanya kuwa huru.
0 comments:
Post a Comment