KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Wednesday, December 31, 2014

ANGEL BENARD - NEED YOU TO RAIGN ( New Gospel Video )


ANGEL BENARD AMEKUA NI MWANAMUZIKI WAINJILI ANAEFANYA MUZIKI WA INJILI KWA STAILI TOFAUTI NA ILIYO ZOELEKA KWA WANII MBALIMBALI NCHINI. AMEWEZA AMSHA HISIA ZA WASIKILIZAJI MBALIMBALI KWA MUZIKI WAKE WAKIWAMO WAKRISTO NAWASIO WAKRISTO KUTOKANA NA STAILI YAKE TOFAUTI TOFAU ANAYOTUMIA KATIKA NYIMBO ZAKE. WAWEZA TIZAMA VIDEO YAKE HAPA CHINI ILI KUSHUHUDIA HILO. TULIWEZA HOJIANA NAE KWA NJIA YA SIMU TOKA ARUSHA. KAAHIDI MAPEMA MWAKANI KUANZA ACHIA VIDEO ZAIDI TOKA KWENYE ALBUM YAKE MPYA. MPAKA SASA BAADH YA VIDEO HIZO ZIMEKAMILIKA NANYINGINE ZIKIENDELEA ANDALIWA. MOJA YA VIDEO HIZO ZILIZOPO TAYARI NIHII HAPA CHINI.

Friday, December 26, 2014

CHELLA FT BECKA - NITAFIKA ( New Audio )


Habari!Poleni na majukumu ya mwaka mzima mpaka sasa tunaelekea kuumalizia.Kwa jina najulikana kama "CHELLA" toka kundi la "MICHANO LUKUKI"Natanguliza shukrani zangu kwa sapoti yenu katika mwaka unaoisha na niwatakieni heri ya christmass na mwaka mpya.Katika kuelekea kuumaliza mwaka nautambulisha kwenu wimbo wangu mpya ujulikanao kama "NITAFIKA"Niliomshirikisha "BECKA TITLE"toka kundi la "B.O.B CLICK".Wimbo umefanyika chini ya studio za Tongwe record,chini ya producer "GEOF MASTER/MANUVA'.Ni wimbo ambao upo kwenye album yangu mpya iliyoko sokoni ijulikanayo kama "RUDI MKOA"/Dar imekupa kiburi".Mawasiliano yangu ni 0764191674.Naombeni sapoti yenu ili tuzidi kukuza vipaji chipukizi na muziki wetu kiujumla.#Asanteni#

Tuesday, December 23, 2014

Monday, December 22, 2014

Saturday, December 20, 2014

MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU ALIE BADILI MAISHA YAWATU ZAIDI YA 117 MILLION DUNIANI KWOTE ( Makala Maalumu kwa Msimu wa X Mass )

Brian Deacon ndani ya filamu ya "JESUS" Mwaka 1979.

Ikiwa leo ni siku chache ambazo zimebakia kuelekea tar 25/12 yakila mwaka ambapo wakristo wote ulimwenguni wanakumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo kama mkombozi wa ulimwengu, Yesu Kristo aliyekuja duniani takribani miaka 2000 iliyopita.Ukurasa huu umeamua basi kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu kama mwana sanaa inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, Ukurasa huu umeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.
Brian Deacon Punde Baada ya Kumaliza Igiza filamu ya "JESUS" Mwaka 1980
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo. Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji. Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.
Watu wakitizama filamu ya "JESUS" Punde baadaya ya Kukamilika mwanzoni mwa miaka ya 1980 ambayo Brian Deacon  ndio alikua mwigizaji Mkuu
Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.
Sehemu ya Picha aliocheza Bwana Brian Deacon Kama Yesu katika filamu ya "JESUS" Mwaka 1979
Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye (Brian) azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon, akaamua kuzungumza nao, baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi. Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.
Watumishi wamungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya "JESUS" Katika Vitongoji vya huko Kongo
Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.
Huyu ndie Brian Deacon Mwigizaji Mkuu wa filamu ya "JESUS" alivyo sasa.
Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 133 (kwa takwimu za mwaka 2001), zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa. Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu. Kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985, The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles. Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel. Ukurasa huu unawatakia heri ya X Mass na mwaka Mpya. Endeleeni kuungana nasi Kila siku nakila saa, mahala hapa hapa. Kwa maoni na ushauri zaidi Unaweza tutumia kupitia Mail yetu selengakaduma@gmail.com Pia kupitia namba ya simu +255757363005 Muda wowote kuwa huru. Bwana awe nanyi siku zote. Tizama kipande cha dk 14 hapa chini cha sehemu ya Video ya "JESUS" Jinsi Yesu Alivyo Zaliwa Duniani.

Friday, December 19, 2014

Thursday, December 18, 2014

ANGEL BENARD - LINDA MOYO WAKO ( New Audio )


LINDA MOYO WAKO ni wimbo wa 9 kutoka kwenye album ya nyimbo 10 NEW DAY ya ANGEL BENARD: "Ni inspirational song ambayo inalenga kuonya na kushauri namna mtu mwenye ndoto au maono fulani yatatimieje. Ni maneno yenye faida kumsaidia mtu namna ya kuishi na watu 'si kila achekae akupenda, tabasamu ni mwamvuli kuficha yalo ndani ya mtu' sasa ili kujiepusha na tabu na watu, jua we ni nani, unaenda wapi na waliokuzunguka ni watu wa namna gani."

909 - NJOO HAPA ( New Audio )


Baada ya mafanikio mbali mbali yakiwemo kuachia Mixtape yao ya kwanza (Here Goes Nothing), na kuperfom kwenye stage mbali mbali kwa mwaka 2014 sasa Mwaka unavyoelekea ukingoni,kundi la muziki 909 wanakuetea wimbo wa kusikiliza na uwapendao msimu huu wa Kristmasi, ikiwa bonus track ya Album yao inayotarajiwa kutoka mwanzoni mwa mwaka 2015

Tuesday, December 16, 2014

Friday, December 12, 2014

ANGEL BENARD - DREAMER ( New Gospel Audio )


Wimbo wa 8 Wiki ya 8 kutoka kwenye album ya NEW DAY ya ANGEL BENARD yenye nyimbo 10, unaitwa DREAMER. "I'm letting go, all of my pity parties,I'm building up my life again..yeah... no more hiding behind my fears, I'm standing up, once again." - Angel Benard. Download hapa pamoja na lyrics: https://mkito.com/song/dreamer/7922

Tuesday, December 9, 2014

ALICHOKIANDIKA AISHA SANDIGA KWA DIAMOND PLATNUMZ ( Storry )


STORRY HII TOKA KWA AISHA SANDIGA ( Mtangazaji Ebony Fm Iringa ) Wow, worth sharing: HONGERA DIAMOND PLATNUMZ! Ngoja niseme kidogo kitu nilichojifunza kwa huyu kijana. Kuna wakati fulani Hezron Michael (Paul Mashauri) aliwahi kuandika kuhusu msanii wa muziki wa bongofleva Diamond akisifia bidii yake lakini sasa naelewa zaidi. Diamond huyu alikuwa hana hela ya kwenda studio mara ya kwanza (mtaji wa biashara) lakini hii hai kuwa kizuizi kwake. Kwa kuwa alitaka kutoka moyoni aisee hela ilipatikana! Ilikuwaje? Mama yake alimpa mkufu akauze ili apate hela ya studio. Na alienda studio. The rest is history. Sasa ili unielewe hapa naomba unisikilize kidogo. Unamjua Joseph Kusaga? Labda humjui. Huyu ni mmiliki wa Clouds FM na Clouds TV. Niliwahi kumsikiliza LIVE akisema kuwa wakati alipopata wazo la kufungua kituo cha redio mtaji "uligomba". Kwa kuwa alitaka saana kufungua redio alimfata mzazi wake akaomba HATI YA NYUMBA ili akakope pesa benki! Can you imagine? Mzazi alimpa akijua hiyo dream ikifa nyumba hawana. Hela ilikopwa nyumba ikawekwa rehani and the rest is history! Unamjua Jeff Bezoz? Kama humjui nisaidie tu kugoogle. Lol. Anyway. Huyu ni moja ya matajiri 20 wakubwa duniani. Hivi sasa akiwa No. 18 kwenye Forbes list utajiri wake ukiwa $32 billion! Lakini huyu bwana wakati anataka kuanzisha mtandao wake wa Amazon.com hakuwa na mtaji. Sasa huyu alichofanya aliwafata wazazi wake ambao walikuwa ndo wamestaafu. Akawaomba pensheni yao ili afungulie biashara. Can you imagine wazazi waliwaza nini? Wanamuuliza biashara gani anawambia ni mambo mapya ya internet nataka niuze vitabu kwa kutumia internet. Hawakuelewa lakini kwa vile alitaka wamkopeshe hiyo pensheni by hooks and crooks aisee walimpa! And the rest is history. Hebu jiulize leo wazazi wake wanaishije? Jiulize mzazi wa Jay Kusaga leo kama anashida ya nyumba (kama yupo hai.. Na kama yu hai aishi miaka mingi zaidi). Jiulize mama wa Diamond Platnumz leo anaishije. Kwanza tunavyoongea hayupo bongo yuko zake Sauzi na mwanaye! Yes. Jiulize kama ana shida ya hela ya kunulia mkufu tena. Sasa wengi mna woga! Ndoto unayo lakini ukiulizwa kidogo tu: We Salome unaomba hela ya biashara ukishindwa hela yangu itakuwaje..? Au ukiambiwa elimu ulishindwa biashara utaweza? Unajiinamia kesho unaenda kwenye mkesha kuomba Mungu afungue njia nyingine! Pshuuu! Hivi humo kichwani kuna maji au? Afu ukisikia watu wanafanikiwa ooh Freemason ooh one day nitamiliki na kutawaka. Tawala kwanza fikra zako! Fursa zinazidi kuja na kukupita uko tu reception unapata laki tatu kwa mwezi na degree yako ya Mass Communication! Pshuuu. Diamond alipouza mkufu hela nyingine alipeleka studio kurekodi nyingine akaenda British Council kusoma English! Mambo ya "Good morning" mambo ya "let me read the contact once again.." nini. Huyu ni mtu anayeona mbali. Wasanii Wangapi walikuwa maarufu kabla yake but hawakuwaza kama yeye. Niwataje? Halafu haohao wanamsengenya na kumponda. Hivi wasomi wangapi wanajua lugha zaidi ya Kiswahili. Honestly. Hivi nitajie wasomi wangapi wameitangaza nchi hii kimataifa kama Diamond Platnumz. Kila siku wasomi tunapost picha za graduation. "Thank God I have made it. Xoxo". You have made what? Joho au? Joho hata wanafunzi wa Nursery School wanavaa mbona. Ilipotokea uvumi kuwa anapewa degree ya heshima kila mtu alisema ooh sijui nini.. Umeitangaza nchi wewe?!! Diamond anasomesha watoto watatu IST. Unajua ada ya IST lakini? Au unadhani naongelea gari IST. Naongelea International School of Tanganyika ambao watoto wa mabalozi wa nchi za nje ndo wanasomeshwa na nchi zao! Huyo ni Diamond Platnumz! Wewe umesomesha wangapi hata shule ya Kata na una Masters ya UDSM sijui ya Mzumbe sijui ya Edinburgh, nk. Mentality is everything. Sasa Mungu akubariki wewe au yeye? Kila siku uko kwenye maombi ya kufunguliwa na kuinuliwa unarudi nyumbani saa tano usiku Diamond anatoka studio saa saba za usiku. Who is hard working? Siku ya mwisho walokole tutaabishwa na watu tunaowaona "namna gani vipi". Mungu atupe ujasiri wa kufanya makuu! Mentality ya utajiri haiangalii elimu. Shigongo na wewe nani kasoma zaidi. Nani tajiri? Nani anaweza kuitwa na rais awambie vijana kwenye TV kuhusu biashara Shigongo au wewe mwenye Degree ya biashara kutoka CBE? Jiulize maswali magumu. Usijipe FALSE HOPES. Ati hata nikikosa hela mbinguni naenda. Sikia wewe, kuna watu hawakwendaga mbinguni kwa sababu tu hawakumvisha mtu aliyekuwa na uhitaji wa Nguo. "Nalikuwa uchi...." Hilo tu. Nilikuwa namchekesha cousin wangu Haruni Leonard kuwa unaweza kwenda mbinguni ukamkuta BOB MARLEY na huku wewe ulikuwa unaimba gospel. Kama unataka kufanikiwa hebu acha excuses. Sina mtaji. Sina muda. Kwani kuna mwenye kiwanda cha kuzalisha muda? Muda wa Escrow uliupata. Muda wa kukaa kubadilishana mawazo na watu upate mtazamo mpya huna eti. We kaa hapo? December ndo hiyo imefika! Diamond akirudi hukawii kusikia kaenda ikulu. We roho inakuuma hata kazini kwako tu hutambuliki. Hukawii kusikia kaenda Marekani kufanya shoo. We mwisho wako Tabata Bima Buguruni Posta hata huko hawakujui. Success has nothing to do with your religion but your MENTALITY. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA NAMTUNZI ....

MZUNGU KICHAA - TWENDE KAZI ( New Audio )


OFFICIAL PRESS RELEASE Mzungu Kichaa releases his first Swahili single since his award winning debut album Tuko Pamoja. The single titled ‘TWENDE KAZI’ (Let’s Work) is from his EP ‘HUSTLE’ which was released on the 12.12.12. Mzungu Kichaa and P Funk Majani have produced the song. With over 50 Bongo Flava albums to his name Majani is without a doubt the Godfater of Bongo Flava, one of East Africa strongest and most popular urban genres. Twende Kazi has been nominated for a Danish Music Award as Best World Track. The song is released on Mzungu Kichaa’s own label Caravan Records. It has been mixed and mastered at Copenhagen’s Winding Road Studios by Flemming Rasmussen, who, apart from producing some of Denmarks biggest artists, produced Metallica’s first four albums. “Staying true to who I am, this single off my EP ‘Hustle’, is first and foremost for my Tanzanian fans. However I will be pushing my personal boundaries when Hustle hits the streets; The EP also has two songs in English and a collaboration with one of my favorite Kenyan artists. I am very excited about this release, as I have been dying to show my non-Swahili speaking fans what I write about in my music”. The songs nomination for a Danish Music Award shows that Tanzanian Bongo Flava has a wider appeal than ever before. Since the release of his debut album, Tuko Pamoja, Mzungu Kichaa has been actively touring in Denmark with his Tanzanian band, which explains how the artist landed this nomination. Mzungu Kichaa has also toured Africa, with several concerts in Kenya, Uganda and Tanzania. Twende Kazi encourages youth to take their futures into their own hands. It condemns jealousy and the idea that success comes easily. Please see the lyrics for Twende Kazi below: CONTACT: Louise Kamin +255 789 275 947, +255 763 022 022 CRTanzania@gmail.com T: @caravanrec

TEL OMAINO - NIPENDE ( New Audio Coming soon )


Kutoka kipande cha Tunduru one,anaitwa Tel omaino,msanii wa bongo fleva yupo kwenye hatua za mwisho za kuachia ngoma yake mpya itakayoitwa 'nipende' ikiwa imefanyika studio za mkubwa music chini ya utayarishaji wa producer Necka beat. Soon Ujio wake utasomeka hapa hapa kwenye Ukurasa wetu. Anaomba support yako mdau na maoni, pale ikibidi.

Saturday, December 6, 2014