![]() |
| Ahmed Ally Upete 'Geez Mabovu' ALIZALIWA MWAKA 1983 IRINGA TANZANIA.KAMA ARTIST MKUBWA WA HIP HOP TANZANIA, ALIWEZA FANYA HIT SONG KALI KADHAA, IKIWEMO MTOTO WA KIUME, DAKIKA 0, NA NYINGINE NYINGI |
Friday, November 14, 2014
Wednesday, November 12, 2014
Berry B ft Attu Mivoko Kura Zetu ( New Video )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:36:00 PM
VIDEO MPYA YA Berry B ft Attu Mivoko IITWAYO Kura Zetu, AUDIO IKIWA IMEFANYWA NA ecko top magic sound Iringa, na Video Director Punje. Hii video imerekodiwa katika mazingira halisi,Iringa kulingana nauhalisia waujumbe uliomo ndani. Tizama hapa bila kukosa.
GODZILA - KARIBU YAKO ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:18:00 PM
GODZILLA - ILLUMI NAUGHTY ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:13:00 PM
FM ACADEMIA - CHUKI YA NINI? ( New Album )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:00:00 PM
FM Academia wanakuletea albam yao mpya kabisa iitwayo CHUKI YA NINIi? Hizi ndizo nyimbo mbili za kwanza kwenye album hii ya wakali wa muziki wa dansi wazee wa Ngwasuma!
Tuesday, November 11, 2014
SALMA - KILABHO ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 1:00:00 PM
ARTIST: SALMA SONG: KILABHO PROD: TINO MAFIA & ESSEM CREATOR - ESSEM RECORDS MKALI WAMIDUARA TOKA MBEYA HUYU HAPA, ANAHITAJI SUPPORT YAKO MDAU. Kuupata wimbo huu Just Bofya hapa chini
OPK - NATAMANI ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 12:55:00 PM
SONG: NATAMANI
PROD: SUPER - SUPER RECORDS
KIZAZI KIPYA TOKA MKOA MPYA NJOMBE MAKAMBAKO. ANAOMBA SUPPORT YAKO MDAU WA MUSIC TANZANIA. Bofya hapa chini kuupata wimbo wake
MWASITI FT KINGZILLAH - ( New Audio Comming Soon )
Posted by NAOMIKADUMA On 12:39:00 PM
Ifikapo tar 17 / 11 / 2014 Mashabiki wa Mwasiti watakua wakionja Piko jipya toka kwa msanii huyo likiwa na ladha ya KingZilla aka GodZilla ndan. Wimbo huu utapatikana hapa hapa utakapo ruhisiwa tuu ingia mtaani siku hio. Karibu tena kwenyeukurasa wetu wakijanja.
BEEMAN FT DEAL, DULLAYO, JORDAN, WYRE, BANANA ZORRO, STEVE RNB & BEN POL - EMBEDODO ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 12:19:00 PM
BRAND NEW KUTOKA GRANDMASTER RECORDS Embe Dodo Remix - Hii ni kubwa kuliko kutoka Grandmaster Records kwa ushirikiano mkubwa na Lovechild Records, Beeman akiwa na Jordan, Wyre, Banana Zorro, Ben Pol, Jdeal, Steve RnB na Dullayo. Produced by John B #embedodormx #balaatupu #kubwakuliko #grandmasterrecords follow @johnbgrand @beemantz @wyredalovechild @bananazorro @iambenpol @stevernb powered by @fresh120media, www.fresh120media.com
MTOZA MC FT ONARY - DEEP DOWN ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 12:07:00 PM
Habari!poleni na kazi ya kujenga taifa.Tunautambulisha kwenu wimbo mpya wa'MTOZA MC'toka kundi la 'MICHANO LUKUKI lililopo kibena njombe linaloundwa na (MTOZA MC NA CHELLA)'.Wimbo unaitwa 'deep down'aliomshirikisha 'onory mchizi' na umefanywa na producer 'Tonny'toka 'E-LAB REC.MBEZI'.Tunaomba sapoti yenu.Mawasiliano yetu ni (MTOZA MC 0754871657)NA (CHELLA 0764191674)
JCB Makalla - MTOTO MKALI ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 12:02:00 PM
BRAND NEW JCB - MTOTO MKALI Hii ni ngoma mpya ya JCB Kutoka WATENGWA Kijenge Juu, ngoma inaitwa MTOTO MKALI (Ghetto Luv) imefanywa katika studio za Watengwa chini ya Daz Naledge na kufanyiwa Mastering na DX wa Noiz Maker. Featured kwenye huu wimbo ni Hisia kutoka Tusker Project Fame. Hii ngoma itapatikana katika Album mpya ya #YANIKAMBELEKABISA #YKMK ambayo itatoka hivi karibuni.
Saturday, November 8, 2014
ENDU G - SHOLELA ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:36:00 PM
Endru G mzee wa Skola anakuja na kibao chake kipya SHOLELA. Ujumbe wa wimbo huu unapatikana vizuri zaidi kupitia lyrics zake zilizopo hapa chini. SHOLELA BY ENDRU G Sholelaaa....uh badili tabia we,uh badili tabia wee.sholelaa,badili tabia we sholela sholelaa uyeee..ooh ohh..worker… VERSE 1 Nikweli umeumbika lady,kila jicho linakuona wewee,uzuri wako niwakipekee lakini kinachokuponza ni tabiaa, warembo mbona wako wengi eh,ila moyo umekuona wewee,ah unanigeuza mjinga sababu ninakupenda ahaah, kwani nilidata na ilo penzi lakoo,ila we unanichuna,amini ukukugana na moyo gwane,indumbula we bitee X2 CHORUS ujanja mwingi mbele giza usijione unaweza,sholelaa,dunia hii tunapita elewa mwisho utafikaa,ujanja mwingi mbele giza usijione umemalizaa,sholela,dunia hii tubapita elewa miaho utafikaaa VERSE 2 Uzuri wa usoni ungekuwa na na moyoni,usingepata tababu we niwakuwekwa ndani,kuliko kubadili awo mabwana every day,wanakutumia na kukuacha,uzuri wakoo,ingekuwa na moyoni ,usingepata tabu wa ni wakuwekwa ndani,amini today bora mimi nitembee ,dunia ikakufunze wewe, kwani nilisadata na ilo penzi lako ,ila we ukanichunaa,amini ukukugana na moyo gwane,indimbula we biteee X2 CHORUS ujanja mwingi mbele giza usijione unaweza,sholelaa,dunia hii tunapita elewa mwisho utafikaa,ujanja mwingi mbele giza usijione umemalizaa,sholela,dunia hii tubapita elewa miaho utafikaaa BRIDGE Sholela, ujana aufai, sholela, kubadili mabwana , sholela., kutembea na wanaume za watu, sholela, ujana aufai hiiiii CHORUS ujanja mwingi mbele giza usijione unaweza,sholelaa,dunia hii tunapita elewa mwisho utafikaa,ujanja mwingi mbele giza usijione umemalizaa,sholela,dunia hii tubapita elewa miaho utafikaaa
REDSAN FT NYLA - TOUCH ME THERE ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:28:00 PM
Msanii Redsan kutoka nchini Kenya anakuja na single yake mpya TOUCH ME THERE featuring Nyla. Redsan ameshika chati za Kenya kwa muda mrefu na nyimbo kama Step on it, Chicken, Apakatwe, Pain n.k. Huu wimbo unapatikana Tanzania exclusively kupitia Mkito.com
ANGEL BENARD - NEW DAY ( New Audio Gospel )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:23:00 PM
Wimbo mpya kila wiki kwa wiki 10 Wimbo wa 3 kutoka kwenye album NEW DAY ya Angel Benard, wimbo huu New day ndiyo unabeba jina la album. Katika huu wimbo siku ya jana inawakilisha "mambo yaliyopita" inaweza kuwa ni mtu, vitu, hali fulani n.k. Tunaiaga kwaheri na kukubali kuendelea na maisha yaliyopo mbele yetu. Hakuna kurudi nyuma.
Wednesday, November 5, 2014
NEW WAKAZI - WANAWAKE WA DAR ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 11:50:00 AM
Exclusive release kutoka Mkito.com - Msanii wa Hip Hop WAKAZI ambaye kwa muda mrefu amekuwa akiishi nchini Marekani huku akifanya muziki anakuletea single yake mpya iitwayo WANAWAKE WA DAR. Wakazi anasifa ya kuitwa "Bilingual Beast" kwakuwa anauwezo wake mkubwa wa kuchanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza katika mashairi yake. Mpaka sasa Wakazi ameshaachia Mixtape 3 na yuko mbioni kuachia album. Sikiliza wimbo uliyokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa hapa:
Friday, October 31, 2014
YOU KILLER FT FID Q - 13 (New Audio)
Posted by NAOMIKADUMA On 6:57:00 PM
Wimbo mpya kabisa kutoka Young Killer Msodoki akishirikiana na mkongwe wa hip hop Fid Q pamoja na Belle 9. Wimbo huu umewashirikisha producer wanne yaani P Funk Majani kutoka Bongo Records, Palla Midundo, Amiga Tyga na Lol Pop. Wimbo unaitwa 13.
JCB - MTOTO MKALI (New Song from JCB Comming Soon
Posted by NAOMIKADUMA On 6:54:00 PM
ANGEL BENARD - SHUJAA ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 6:36:00 PM
Huu ni wimbo wa pili kutoka album mpya NEW DAY kutoka kwa Angel Benard - wimbo unaitwa SHUJAA.
SHUJAA.
Kuna wakati katika maisha tunakutana na mambo magumu na
hakuna wa kukutia moyo, kwa sababu wengi waliotuzunguka ni watu ambao mara
nyingi hufurahi tunapoumia. Huu ni wimbo ambao mtu unajikumbusha mwenyewe juu
ya uhalisia wa maisha na kasha unajikumbusha kwamba “you are the hero of your
own soul”. Mungu ametuamini na mitiani ya maisha, hivyo na sisi tunakubali
kupambana na kila hali hadi kufikia ndoto zetu hata kama huko njiani kuna
vikwazo.
WAKAZI - ONE DAY YES (New Audio)
Posted by NAOMIKADUMA On 6:24:00 PM
WAKAZI - DENGUE FEVER (New Audio)
Posted by NAOMIKADUMA On 6:19:00 PM
HISIA - GIMME A CALL - (New Audio)
Posted by NAOMIKADUMA On 5:53:00 PM
Mshiriki wa Tusker Project Fame HISIA anakuja na kibao chake kipya GIMME A CALL ambacho amemshirikisha producer John Blass kutoka Grand Master Records. Hisia mwenye kipaji cha vocals ameonesha uwezo wake mkubwa katika hii track iliyopo katika miondoko ya Afro Soul. Wimbo ulitambulishwa rasmi katika concert iliyoandaliwa viwanja vya Alliance Francaise akisindikizwa na Grace Matata pamoja na kundi la H_art the Band kutoka nchini Kenya. HISIA - GIMME A CALL Vocals: Hisia Drums: Nelson Martin Mugarula Bass guitar: Kelvin Samuel Guitars: Goodlucks Sway, Mzee Francis, Hisia Keys: John Blass Written by: Hisia Music consultant: BR Marungi Instruments recorded at Fnouk Music Studios Co-arranged by Kelvin Samuel Produced by: John Blass - Grand Master Records
Friday, October 24, 2014
ANGEL BENARD - NEED YOU TO RAIGN ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 11:01:00 PM
Episode 01: NEED YOU TO REIGN by ANGEL BENARD Wimbo wa kwanza katika album ya NEW DAY kutoka kwa ANGEL BENARD "Need you to reign" ni wimbo unaomuomba Mungu awepo katika maisha yake na amuongoze katika kila jambo. Wimbo huu umerekodiwa Mujwahuki Studios chini ya Producer Mujwahuki mwenyewe. Producer huyu pia alishawahi kufanya kazi na msanii Ben Pol katika wimbo wake wa Nikikupata. Nyimbo zote katika album hii zimetungwa na kuimbwa na Angel Benard.
MWANA FA FT ALIKIBA - KIBOKO YANGU ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:42:00 PM
Sote tumeusubiri kwa hamu na sasa wimbo mpya kabisa wa Mwana FA na Alikiba umewasili rasmi. Baada ya Mwana FA kutoa wimbo wa Mfalme live katika tuzo za KTMA 2014 msanii huyu ameungana na mfalme wa bongo flava yaani Alikiba ili kuwaletea mashabiki wake kazi nyingine kali. Producer wa wimbo huu si mwingine bali ni Marco Chali wa kutoka MJ Records ya jijini Dar Es Salaam. Katika kuurekodi wimbo huu kumekuwa na matoleo manne tofauti ambayo wadau walikuwa wakisindwa kuamua ni upi wa kuachia kwa kuwa zote zimesimamia kucha. Mwana FA na kampuni ya LifeLine ambaye yeye pia ni mkurugenzi wameamua kuuachia wimbo huu moja kwa moja kupitia Mkito.com ili kuhakikisha unawafikia wapenzi wake wengi zaidi na kuhakikisha kuwa kuna maslahi yanapatikana katika kazi hii. Pakua wimbo huu mpya kabisa sasa upate flava kali.
DENNIS DRAZZY - CHEZA ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:32:00 PM
CHEZA is a song performed and written by a young Upcoming artist from Tanzania, Dennis Drazzy (22) who does Rap with a twist. The song which is recorded and mastered at Hebron Studios and mixes elements of House music, pop and rap all in one resulting to a Rap House genre and is from the Black & White mixtape coming in 2015.
MAD ICE - EVERYTHING I DO ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:20:00 PM
Mad Ice ni msanii aliyezaliwa nchini Uganda na kuishi Tanzania kwa muda mrefu ambapo aliaanza rasmi kazi yake ya muziki na kutoa albam yake ya utmbulisho iitwayo BABY GAL (2003, Chini ya Miikka Mwamba). Msanii huyu wa Afro-Soul baada ya album hiyo alihamia nchini Finland ambapo aliendeleza kazi pamoja na producer Miikka Mwamba na studio nyingine nchini humo na kutoa nyimbo nyingi zilizoshika chati tofauti duniani kote zikiwemo Maneno, Mapaenzi Sumu na Te Amo. Single mpya kabisa ya Mad Ice inaitwa EVERYTHING I DO na imefanyika Sonic Pump Studios, Finland chini ya producer DJ Hermanni.
TIZAMA PICHA 5 ZA UJIO WA MAD ICE NA TOKA MOJA YA STUDIO KUBWA DUNIANI ( Up Date Info )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:10:00 PM
Mwanamuziki Mad Ice amerudi Tanzania kutoka nchini Finland ambapo ametoka kurekodi single yake mpya EVERYTHING I DO chini ya producer DJ Hermanni kwenye studio ya kimataifa ya Sonic Pump Studios (http://www.sonicpumpstudios.com/). Mara nyingine huwa inatosha kuangalia mandhari ya studio kujua kuwa kazi zinazotoka huko lazima ziwe na kiwango cha kimataifa. Tazama picha hizi za studio halafu tusubiri kusikia mapishi yake Jumatatu tarehe 20 Oktoka.
ANGEL BENARD - 10 SONGS 10 WEEKS ( UpDate Info )
Posted by NAOMIKADUMA On 10:00:00 PM
ANGEL BENARD ni jina ambalo limekuwa likisikika kwa miaka kadhaa sasa kwenye ulimwengu wa muziki wa gospel. Angel Benard mwenye miaka 25 hatimaye sasa anaachia album yake NEW DAY kwenye mfumo wa digitali kupitia Mkito.com. Watu wengi wamekuwa wakisubiri kusikia nyimbo zake za zamani lakini haikuwa rahisi kuzipata. Album hii ni album ya 3 ya mwana dada huyu mwenye sauti ya maajabu. Ni wasanii wachache sana wa muziki wa gospel ambao wamefanikiwa kuvusha nyimbo zao zikapendwa na wapenzi wa gospel pamoja na wapenzi wa muziki wa bongo flava, RnB n.k. na mwimbaji huyu ni mmoja wapo. Katika kuitambulisha album hii Angel Benard ataachia wimbo mmoja kila siku ya Alhamis kwa wiki 10 mfululizo. Wimbo wa kwanza utatoka tarehe 23 October na unaitwa NEED YOU TO REIGN ukiwa katika minodoko ya Reggae.
HISIA - MAWAZO ( Vocal of New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 9:52:00 PM
Msanii Hisia ambaye aliiwakilisha vyema sana nchi yetu katika mashindano ya Tusker Project Fame mwaka jana anakaribia kuachia wimbo wake mpya uitwao GIVE ME A CALL hapo tarehe 25 Octoba katika show ya live. Katika kuusubiri wimbo huo tujikumbushe track yake ambayo imeshika chati nchini Kenya kwa wiki 6 mfululizo iitwayo MAWAZO. Wimbo huu pia unapatikana kama acapella, yaani vocal tu, ili wapenzi wake tusikie ni kwanini Hisia aliweza kufanya vizuri vile kwenye mashindano ya Tusker Project Fame.
Kwa wale wote watakao taka kufika kwenye show yake itafanyika tarehe 25/10/2014 Alliance Francaise kuanzia saa moja jioni.
BRAND NEW MKUBWA NA WANAWE - INOOH (Audio)
Posted by NAOMIKADUMA On 9:18:00 PM
Wimbo mpya kutoka kwa Mkubwa na Wanawe ambao ni kati ya nyimbo zilizopo kwenye collection ya NISEME. Wimbo huu inaitwa INOOH. Mkubwa na Wanawe ni wansanii ambao kwa muda mfupi sana wameweza kuonekana katika majukwaa makubwa na kuwa na mafanikio makubwa sana kimuziki wakiwa chini ya usimamizi wa Mkubwa mwenyewe Saidi Fela. Fela ni meneja ambaye amesimamia na kuwatoa wasanii na makundi kama Juma Nature na Wanaume. Pata wimbo mpya kabisa kutoka kwa Mkubwa na Wanawe kupitia Mkito.com sasa.
Mr.LOVA & JACKA - NEVER IN LOVE AGAIN ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 8:44:00 PM
Track- Never in love Again by Mr.Lova and Jacka UNGANA NASI HAPA KUUPATA WIMBO HUU MPYA KWA KUBOFYA HAPA
Thursday, October 16, 2014
G wyder ft meda__morelove ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 3:40:00 PM
NIKKI MBISHI, ONE INCREDIBLE, SONGA, FT LADY JAY DEE - KUPANDA NA KUSHUKA ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 3:33:00 PM
Wimbo mpya kutoka kwa Nikki Mbishi Ft Jay Dee, One The Incredible na Songa. Huu wimbo Kupanda na Kushuka umetayarishwa na producer Man Water.
JOETT FT G FULLAH & LEVEL ONE - I'm gonna live forever ( New Audio )
Posted by NAOMIKADUMA On 3:24:00 PM
PRESS RELEASE
Joett Aachia Singo Mpya
Akishirikisha Wasanii wa Bongo Flava G Fullah na Level One
Mwalimu wa kuimba na msanii wa ku-rekodi miondoko ya pop –
Joett, anaachia singo yake mpya I’m Gonna Live Forever Octoba 13 2014, ambayo
amewashirikisha wasanii wa bongo flava G Fullah na kundi la vijana wa kiume
(boyband) lijulikanalo kama Level One. Voko za trak hii zilirekodiwa na Max
Rioba pale Authentic Records, Dar es salaam, na kuandaliwa na producer mahiri
nchini Uingereza, Patrick Jonsson, ambae amefanya kazi na Joett kwa kipindi
kirefu. Mixing pamoja na mastering ya trak hiyo imefanyika na sound engineer na
producer King Penn (KP), wa Atlanta, Marekani, ambae amefanya kazi na lebo ya Madonna
ijulikanayo kama Maverick; Warner Bros, EMI, Beyonce, Solange, Columbia, 50
Cent, John Lennon Songwriters, MCA, The Big Boy Records, Def Jam, Dallas
Austin, na mamia ya wasanii wa lebo ndogo zijuliakanazo kama Indie Labels. Joett,
ambae hutoa singo moja tu kwa mawaka, aliamua kuwashirikisha vijana hawa ili
kuwapa fursa ya kutoka katika viwango vya kimataifa, na amedhamiria kuendelea
kufanya hivyo kwa miaka ijayo. “Ningependa sana kukuza vijana katika tasnia hii
ya mziki, na hasa kuwashukuru mashabik pamoja na wadau wa mziki kwa ushirikiano
wao enedelevu,” alisema Joett.
G Fullah alinyakuliwa na Joett toka kipindi cha ITV Hawavumi
Lakini Wamo; Abdul Kagoi toka Epiq Bongo Star Search 2013; Rahym alitambulishwa
kwa Joett na kaka yake, msanii wa bongo flava Mbongo Halisi, nakuchukuliwa na
Joett kufundishwa kuimba. Nixon alidhaminiwa na mama yake kufundishwa sauti kwa
Joett, alafu baadae Joett akamweka kwenye program yake ya misaada kwa wasanii
chipukizi na hatimae kummpa mkataba wa ku-rekodi chini ya lebo yake – Joett Music.
Kikundi cha Level One ni Abdul, Rahym na Nixon.
Kwa bahati mbaya, G Fullah alifariki asubuhi ya Jumapili
tarehe 5 October 2014. “Habari za kifo chake zimenishtua na kuleta huzuni kubwa
sana kwenye moyo wangu. Nilikua na mipango mikubwa kwa G Fullah katika tasnia
hii ya muziki. Alikua ni mtu mzuri sana. Tutamkumbuka milele, Mungu ailaze roho
yake pahali pema,” alisema Joett.
Subscribe to:
Comments (Atom)
Total Pageviews
Popular Posts
-
Mwanamuziki mkongwe TID anakuletea wimbo wake mpya uitwao PRESSURE aliomshirikisha NAZIZI kutoka nchini Kenya.
-
Ndox_Lete Glass_[Pro by Sampamba music] Kuupakua wimbo huu Bofya hapa chini Kuusikiliza online Gusa hapa chini
-
ARTIST: ATTU FT IBRA SONG: DO YOU PROD: LUSUNGU & GERALD - BANTU MUSIC SHOW LOVE NA MZIKI MZURI TOKA KUSINI MWA TANZANIA>>>...
-
NIMEKUSOGEZEA WIMBO MPYA KABISA WAINJILI UNAOITWA SAFARI BADO TOKA KWA MWANAMUZIKI MKONGWE TANZANIA BONY MWAITEGE.
-
Kua wakwanza kuupata wimbo wa Izzo Bizness Ft. Barnaba & Shaa - Usijiovadoze | Mp3 Download Unaweza play Online kwa kubofya k...
Recent Posts
Categories
BEST TWEET
Selenga Kaduma Blog: NAOMI KADUMA - NASONGA MBELE | Video Gospel https://t.co/nuZSSkQv7i
— selenga kaduma (@selengakaduma3) July 30, 2017
Blog Archive
- ► 2015 (544)
- ► 2014 (253)






















































.jpg)