KITAA SHOP |Bofya Picha Kutembelea Kitaa Shop

Sunday, September 6, 2015

NAKAAYA FT KALA JEREMIAH - NIMECHOKA ( New Audio )


MANENO KUTOKA KWA NAKAAYA: Leo ndio siku ninayoachia nyimbo yangu "nimechoka" naomba uisikilize, vilevile mtumie na mwenzio. Sambaza UJUMBE. Ninaamini kuwa wote tukizungumza bila uoga, tukiamka... tunaweza kuwa na Tanzania isiyo na ufisadi. Haijalishi wewe ni chama kipi, kilicho na maana ni- ukweli unaousimamia. Je hujachoka hizi sekeseke za hii serikali? Kwanini viongozi wetu hawahangaikii na kutatua vitu vya msingi? Afya, miundombinu, elimu nk. Ni sababu tunachagua fisi kuchunga mbuzi na wanapowala hao mbuzi eti tunashangaa! Mwaka huu, Mtanzania mwenzangu- chagua kwa busara...kwa hekima. Usimuangalie kavaa rangi gani au anatokea chama kipi...mwisho wa siku wote wanafanana fanana, ila angalia mtu binafsi, sera zake, historia yake ya maendeleo katika nchi hii na jimbo lake je yeye ndie atakaetupa uhuru? Kwa sababu ndugu yangu, sijui kama umeshashtukia...hatupo huru. Mapambano yanaendelea. Nakaaya Sumari - 2015

0 comments:

Post a Comment