RIPOTI FUPI YA MKITO,COM KWA BLOGGLERS, WANAMUZIKI, NA WADAU WA MUZIKI AFRIKA MASHARIKI.
Ndani ya muda mfupi tumeweza kuwafikia watu wengi kimuziki na pia wasanii wengi wameanza kuona matunda ya kazi zao kupitia mauzo ya online. Wa kwanza wa kumshukuru katika hili ni wewe mwenye blog. Asante kwa uzalendo wako na pia kwa kutoa support kubwa katika kuuendeleza muziki wa Kitanzania. Bado safari ni ndefu lakini tunaamini tutakuwa pamoja katika kila hatua. Mpaka sasa unaweza kujua mkito.com imwenufaisha wa wanamuziki wa Afrika Mashariki kwa mchanganuo mdogo kama ifuatavyo ikiwa tangu mwezi wa tano ianze kazi rasmi mpaka leo imeweza kupata downloads zaidi ya milioni 1 na kila donwloads ni sawa na tsh 250 asilimia 60 ya kiasi cha pesa hicho mara milioni 1 ndiyo kiasi walichokwishwa lipwa wanamuziki ikiwa ni tofauti na usambazaji wa nyimbo kupitia mitandao mingine isiyomnufaisha wanamuziki, hivyo tunakushauri mwanamuziki tumia mkito.com kusambaza kazi zako ili uweze kunufaika kupitia kazi zako. Usisite kutembelea ukurasa wetu www.selengakaduma.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment