Wednesday, December 31, 2014
ANGEL BENARD - NEED YOU TO RAIGN ( New Gospel Video )
ANGEL BENARD AMEKUA NI MWANAMUZIKI WAINJILI ANAEFANYA MUZIKI WA INJILI KWA STAILI TOFAUTI NA ILIYO ZOELEKA KWA WANII MBALIMBALI NCHINI. AMEWEZA AMSHA HISIA ZA WASIKILIZAJI MBALIMBALI KWA MUZIKI WAKE WAKIWAMO WAKRISTO NAWASIO WAKRISTO KUTOKANA NA STAILI YAKE TOFAUTI TOFAU ANAYOTUMIA KATIKA NYIMBO ZAKE. WAWEZA TIZAMA VIDEO YAKE HAPA CHINI ILI KUSHUHUDIA HILO. TULIWEZA HOJIANA NAE KWA NJIA YA SIMU TOKA ARUSHA. KAAHIDI MAPEMA MWAKANI KUANZA ACHIA VIDEO ZAIDI TOKA KWENYE ALBUM YAKE MPYA. MPAKA SASA BAADH YA VIDEO HIZO ZIMEKAMILIKA NANYINGINE ZIKIENDELEA ANDALIWA. MOJA YA VIDEO HIZO ZILIZOPO TAYARI NIHII HAPA CHINI.
VANESSA MDEE, NAHREEL, AIKA, AVID, BARNABA - WCD ( New Video )
Baada ya kusikiliza mdundo wao,karibu tuitizame video ya WCD ya Nahreel,Veemoney na Barnaba. Bonyeza play kuitizama hapa chini.
WIISTA - NAIYE ( New Audio )
Wiista baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu toka ajitoe Navy Kenzo na Kujiunga na NGOMA Entertainement arudi kwa kishindo na NAIYE, na amenukuuliwa akisema "2015 ni mwaka wangu, watu watalikumbuka jina la Wiista, wakae mkao wa kula...Video inakuja karibuni".
GRACE MATATA FT MAUA SAMA - HELLO ( New Audio )
HELLO! is a duet featuring Grace Matata and Maua Sama. The song is written and composed by Maua Sama and Grace Matata, produced and mixed by Ema the Boy at Classic Sound Studio and mastered by Will HD.
WEUSI FT NAVIO, COLLO, NAAZIZ & RABBIT - GERE REMIX ( New Audio )
GERE REMIX ni collaboration ya wakubwa wa Hip Hop East Africa ikiongozwa na WEUSI (Tanzania) na kuwashirikisha NAVIO (Uganda), COLLO (Kenya), NAZIZI (Kenya) na RABBIT (Kenya).
Friday, December 26, 2014
CHELLA FT BECKA - NITAFIKA ( New Audio )
Habari!Poleni na majukumu ya mwaka mzima mpaka sasa tunaelekea kuumalizia.Kwa jina najulikana kama "CHELLA" toka kundi la "MICHANO LUKUKI"Natanguliza shukrani zangu kwa sapoti yenu katika mwaka unaoisha na niwatakieni heri ya christmass na mwaka mpya.Katika kuelekea kuumaliza mwaka nautambulisha kwenu wimbo wangu mpya ujulikanao kama "NITAFIKA"Niliomshirikisha "BECKA TITLE"toka kundi la "B.O.B CLICK".Wimbo umefanyika chini ya studio za Tongwe record,chini ya producer "GEOF MASTER/MANUVA'.Ni wimbo ambao upo kwenye album yangu mpya iliyoko sokoni ijulikanayo kama "RUDI MKOA"/Dar imekupa kiburi".Mawasiliano yangu ni 0764191674.Naombeni sapoti yenu ili tuzidi kukuza vipaji chipukizi na muziki wetu kiujumla.#Asanteni#
Tuesday, December 23, 2014
MATUNZO ZERO UNITY - FURAHA YETU ( New Audio )
Wimbo mpya kutoka kundi jipya aliloanzisha Young Killer Msodoki. Kundi linaitwa Matunzo Zero Unity na wimbo wao wa kwanza unaitwa Furaha Yetu. Download wimbo hapa:
Monday, December 22, 2014
ROSSO - LAI LAI ( New Audio )
Artst name; ROSSO Jina la wimbo; LAILAI Hii Ni nyimboyangu mpya from iringa town, Imefanywa na Sampamba record&dazzy. contact za RASSO 0786429012 NAHITAJI SUPPORT YAKO na msaada pia AHSANTEEEEEEEEE
Saturday, December 20, 2014
MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU ALIE BADILI MAISHA YAWATU ZAIDI YA 117 MILLION DUNIANI KWOTE ( Makala Maalumu kwa Msimu wa X Mass )
![]() |
Brian Deacon ndani ya filamu ya "JESUS" Mwaka 1979. |
Ikiwa leo ni siku chache ambazo zimebakia kuelekea tar 25/12 yakila mwaka ambapo wakristo wote ulimwenguni wanakumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo kama mkombozi wa ulimwengu, Yesu Kristo aliyekuja duniani takribani miaka 2000 iliyopita.Ukurasa huu umeamua basi kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu kama mwana sanaa inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, Ukurasa huu umeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.
![]() |
Brian Deacon Punde Baada ya Kumaliza Igiza filamu ya "JESUS" Mwaka 1980 |
![]() |
Watu wakitizama filamu ya "JESUS" Punde baadaya ya Kukamilika mwanzoni mwa miaka ya 1980 ambayo Brian Deacon ndio alikua mwigizaji Mkuu |
![]() |
Sehemu ya Picha aliocheza Bwana Brian Deacon Kama Yesu katika filamu ya "JESUS" Mwaka 1979 |
![]() |
Watumishi wamungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya "JESUS" Katika Vitongoji vya huko Kongo |
![]() |
Huyu ndie Brian Deacon Mwigizaji Mkuu wa filamu ya "JESUS" alivyo sasa. |
Friday, December 19, 2014
MR.X MAS FEAT MYRA - IZZO BIZNESS ( New Video )
IZZO BIZNESS Drops the Visuals to his Viral release MR.XMAS. The Video was Directed by ( F2K and KHALFANI ) Produced by DUPY and Mastered by FUNDI SAMWELI. Hii ni zawadi ya Izzo kwa mashabiki wake Msimu huu wa X Mass, tar 25 itakua Birth day yake.
Thursday, December 18, 2014
ANGEL BENARD - LINDA MOYO WAKO ( New Audio )
LINDA MOYO WAKO ni wimbo wa 9 kutoka kwenye album ya nyimbo 10 NEW DAY ya ANGEL BENARD: "Ni inspirational song ambayo inalenga kuonya na kushauri namna mtu mwenye ndoto au maono fulani yatatimieje. Ni maneno yenye faida kumsaidia mtu namna ya kuishi na watu 'si kila achekae akupenda, tabasamu ni mwamvuli kuficha yalo ndani ya mtu' sasa ili kujiepusha na tabu na watu, jua we ni nani, unaenda wapi na waliokuzunguka ni watu wa namna gani."
SHILOLE - MALELE ( New Audio )
Kwa wale wote ambao bado hawajapata wimbo mpya wa Shilole basi ndiyo huu hapa. Umetungwa na Barnaba wa kutoka THT na producer ni Nahreel.
909 - NJOO HAPA ( New Audio )
Baada ya mafanikio mbali mbali yakiwemo kuachia Mixtape yao ya kwanza (Here Goes Nothing), na kuperfom kwenye stage mbali mbali kwa mwaka 2014 sasa Mwaka unavyoelekea ukingoni,kundi la muziki 909 wanakuetea wimbo wa kusikiliza na uwapendao msimu huu wa Kristmasi, ikiwa bonus track ya Album yao inayotarajiwa kutoka mwanzoni mwa mwaka 2015
Tuesday, December 16, 2014
IZZO BIZNESS FT MYRA - MR X MAS ( New Audio )
Mr.Xmas @Izzo_bizness Nina Preview STREET Video ya MR.XMAS hapa hahaa I'm Impressed...ila kwasasa Enjoy Audio hapa
BOBRAY TZ FT DEFXTRO - SWAG (New Audio )
Wimbo kutoka kwa Bobray TZ amemshirikisha producer maarufu DefXtro wa Noiz Arachuga. Wimbo unaitwa SWAG.
Friday, December 12, 2014
ANGEL BENARD - DREAMER ( New Gospel Audio )
Wimbo wa 8 Wiki ya 8 kutoka kwenye album ya NEW DAY ya ANGEL BENARD yenye nyimbo 10, unaitwa DREAMER. "I'm letting go, all of my pity parties,I'm building up my life again..yeah... no more hiding behind my fears, I'm standing up, once again." - Angel Benard. Download hapa pamoja na lyrics: https://mkito.com/song/dreamer/7922
PVCAMBO FT MR BLUE - BAEBY ( New Audio )
Mwanadada hatari sana PVCambo akiwa na track yake mpya ambapo Mr Blue ameshirikishwa. Wimbo unaitwa BAEBY
Tuesday, December 9, 2014
ALICHOKIANDIKA AISHA SANDIGA KWA DIAMOND PLATNUMZ ( Storry )
STORRY HII TOKA KWA AISHA SANDIGA ( Mtangazaji Ebony Fm Iringa ) Wow, worth sharing: HONGERA DIAMOND PLATNUMZ! Ngoja niseme kidogo kitu nilichojifunza kwa huyu kijana. Kuna wakati fulani Hezron Michael (Paul Mashauri) aliwahi kuandika kuhusu msanii wa muziki wa bongofleva Diamond akisifia bidii yake lakini sasa naelewa zaidi. Diamond huyu alikuwa hana hela ya kwenda studio mara ya kwanza (mtaji wa biashara) lakini hii hai kuwa kizuizi kwake. Kwa kuwa alitaka kutoka moyoni aisee hela ilipatikana! Ilikuwaje? Mama yake alimpa mkufu akauze ili apate hela ya studio. Na alienda studio. The rest is history. Sasa ili unielewe hapa naomba unisikilize kidogo. Unamjua Joseph Kusaga? Labda humjui. Huyu ni mmiliki wa Clouds FM na Clouds TV. Niliwahi kumsikiliza LIVE akisema kuwa wakati alipopata wazo la kufungua kituo cha redio mtaji "uligomba". Kwa kuwa alitaka saana kufungua redio alimfata mzazi wake akaomba HATI YA NYUMBA ili akakope pesa benki! Can you imagine? Mzazi alimpa akijua hiyo dream ikifa nyumba hawana. Hela ilikopwa nyumba ikawekwa rehani and the rest is history! Unamjua Jeff Bezoz? Kama humjui nisaidie tu kugoogle. Lol. Anyway. Huyu ni moja ya matajiri 20 wakubwa duniani. Hivi sasa akiwa No. 18 kwenye Forbes list utajiri wake ukiwa $32 billion! Lakini huyu bwana wakati anataka kuanzisha mtandao wake wa Amazon.com hakuwa na mtaji. Sasa huyu alichofanya aliwafata wazazi wake ambao walikuwa ndo wamestaafu. Akawaomba pensheni yao ili afungulie biashara. Can you imagine wazazi waliwaza nini? Wanamuuliza biashara gani anawambia ni mambo mapya ya internet nataka niuze vitabu kwa kutumia internet. Hawakuelewa lakini kwa vile alitaka wamkopeshe hiyo pensheni by hooks and crooks aisee walimpa! And the rest is history. Hebu jiulize leo wazazi wake wanaishije? Jiulize mzazi wa Jay Kusaga leo kama anashida ya nyumba (kama yupo hai.. Na kama yu hai aishi miaka mingi zaidi). Jiulize mama wa Diamond Platnumz leo anaishije. Kwanza tunavyoongea hayupo bongo yuko zake Sauzi na mwanaye! Yes. Jiulize kama ana shida ya hela ya kunulia mkufu tena. Sasa wengi mna woga! Ndoto unayo lakini ukiulizwa kidogo tu: We Salome unaomba hela ya biashara ukishindwa hela yangu itakuwaje..? Au ukiambiwa elimu ulishindwa biashara utaweza? Unajiinamia kesho unaenda kwenye mkesha kuomba Mungu afungue njia nyingine! Pshuuu! Hivi humo kichwani kuna maji au? Afu ukisikia watu wanafanikiwa ooh Freemason ooh one day nitamiliki na kutawaka. Tawala kwanza fikra zako! Fursa zinazidi kuja na kukupita uko tu reception unapata laki tatu kwa mwezi na degree yako ya Mass Communication! Pshuuu. Diamond alipouza mkufu hela nyingine alipeleka studio kurekodi nyingine akaenda British Council kusoma English! Mambo ya "Good morning" mambo ya "let me read the contact once again.." nini. Huyu ni mtu anayeona mbali. Wasanii Wangapi walikuwa maarufu kabla yake but hawakuwaza kama yeye. Niwataje? Halafu haohao wanamsengenya na kumponda. Hivi wasomi wangapi wanajua lugha zaidi ya Kiswahili. Honestly. Hivi nitajie wasomi wangapi wameitangaza nchi hii kimataifa kama Diamond Platnumz. Kila siku wasomi tunapost picha za graduation. "Thank God I have made it. Xoxo". You have made what? Joho au? Joho hata wanafunzi wa Nursery School wanavaa mbona. Ilipotokea uvumi kuwa anapewa degree ya heshima kila mtu alisema ooh sijui nini.. Umeitangaza nchi wewe?!! Diamond anasomesha watoto watatu IST. Unajua ada ya IST lakini? Au unadhani naongelea gari IST. Naongelea International School of Tanganyika ambao watoto wa mabalozi wa nchi za nje ndo wanasomeshwa na nchi zao! Huyo ni Diamond Platnumz! Wewe umesomesha wangapi hata shule ya Kata na una Masters ya UDSM sijui ya Mzumbe sijui ya Edinburgh, nk. Mentality is everything. Sasa Mungu akubariki wewe au yeye? Kila siku uko kwenye maombi ya kufunguliwa na kuinuliwa unarudi nyumbani saa tano usiku Diamond anatoka studio saa saba za usiku. Who is hard working? Siku ya mwisho walokole tutaabishwa na watu tunaowaona "namna gani vipi". Mungu atupe ujasiri wa kufanya makuu! Mentality ya utajiri haiangalii elimu. Shigongo na wewe nani kasoma zaidi. Nani tajiri? Nani anaweza kuitwa na rais awambie vijana kwenye TV kuhusu biashara Shigongo au wewe mwenye Degree ya biashara kutoka CBE? Jiulize maswali magumu. Usijipe FALSE HOPES. Ati hata nikikosa hela mbinguni naenda. Sikia wewe, kuna watu hawakwendaga mbinguni kwa sababu tu hawakumvisha mtu aliyekuwa na uhitaji wa Nguo. "Nalikuwa uchi...." Hilo tu. Nilikuwa namchekesha cousin wangu Haruni Leonard kuwa unaweza kwenda mbinguni ukamkuta BOB MARLEY na huku wewe ulikuwa unaimba gospel. Kama unataka kufanikiwa hebu acha excuses. Sina mtaji. Sina muda. Kwani kuna mwenye kiwanda cha kuzalisha muda? Muda wa Escrow uliupata. Muda wa kukaa kubadilishana mawazo na watu upate mtazamo mpya huna eti. We kaa hapo? December ndo hiyo imefika! Diamond akirudi hukawii kusikia kaenda ikulu. We roho inakuuma hata kazini kwako tu hutambuliki. Hukawii kusikia kaenda Marekani kufanya shoo. We mwisho wako Tabata Bima Buguruni Posta hata huko hawakujui. Success has nothing to do with your religion but your MENTALITY. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA NAMTUNZI ....
SHIZZE - SHINE ( New Audio )
Msanii wa Ragga kutoka nchini Kenya anakuletea wimbo wake mpya SHINE. Msanii SHIZZE amefanikiwa kushinda tuzo ya Best Ragga and Dance hall ya mwaka 2013 na pia amefanikiwa kuwashirikisha wasanii wakubwa wa nchini Kenya pamoja na nje ya Kenya.
MZUNGU KICHAA - TWENDE KAZI ( New Audio )
OFFICIAL PRESS RELEASE Mzungu Kichaa releases his first Swahili single since his award winning debut album Tuko Pamoja. The single titled ‘TWENDE KAZI’ (Let’s Work) is from his EP ‘HUSTLE’ which was released on the 12.12.12. Mzungu Kichaa and P Funk Majani have produced the song. With over 50 Bongo Flava albums to his name Majani is without a doubt the Godfater of Bongo Flava, one of East Africa strongest and most popular urban genres. Twende Kazi has been nominated for a Danish Music Award as Best World Track. The song is released on Mzungu Kichaa’s own label Caravan Records. It has been mixed and mastered at Copenhagen’s Winding Road Studios by Flemming Rasmussen, who, apart from producing some of Denmarks biggest artists, produced Metallica’s first four albums. “Staying true to who I am, this single off my EP ‘Hustle’, is first and foremost for my Tanzanian fans. However I will be pushing my personal boundaries when Hustle hits the streets; The EP also has two songs in English and a collaboration with one of my favorite Kenyan artists. I am very excited about this release, as I have been dying to show my non-Swahili speaking fans what I write about in my music”. The songs nomination for a Danish Music Award shows that Tanzanian Bongo Flava has a wider appeal than ever before. Since the release of his debut album, Tuko Pamoja, Mzungu Kichaa has been actively touring in Denmark with his Tanzanian band, which explains how the artist landed this nomination. Mzungu Kichaa has also toured Africa, with several concerts in Kenya, Uganda and Tanzania. Twende Kazi encourages youth to take their futures into their own hands. It condemns jealousy and the idea that success comes easily. Please see the lyrics for Twende Kazi below: CONTACT: Louise Kamin +255 789 275 947, +255 763 022 022 CRTanzania@gmail.com T: @caravanrec
TEL OMAINO - NIPENDE ( New Audio Coming soon )
Kutoka kipande cha Tunduru one,anaitwa Tel omaino,msanii wa bongo fleva yupo kwenye hatua za mwisho za kuachia ngoma yake mpya itakayoitwa 'nipende' ikiwa imefanyika studio za mkubwa music chini ya utayarishaji wa producer Necka beat. Soon Ujio wake utasomeka hapa hapa kwenye Ukurasa wetu. Anaomba support yako mdau na maoni, pale ikibidi.
Saturday, December 6, 2014
ANGEL BENARD - NUMBER 1 ( New Gospel Audio )
Wimbo wa 7 kutoka kwenye album ya NEW DAY ya ANGEL BENARD unaitwa Number 1. "Katika number one, Ninazungumzia tabia za Mungu zinazomfanya yeye kuwa namba moja kwangu na hivyo ninakuwa nasimulia habari zake." - Angel Benard
TID FT NAZIZI - PRESSURE ( New Audio )
Mwanamuziki mkongwe TID anakuletea wimbo wake mpya uitwao PRESSURE aliomshirikisha NAZIZI kutoka nchini Kenya.
Saturday, November 29, 2014
WILLIAM OTUCK - ZAWADI YA X - MASS ( New Audio Album )
Album mpya ya Krismasi! Huu ndiyo wimbo wa utambulisho kutoka kwa William Otuck: https://mkito.com/song/zawadi-ya-x-mas/4691 Album nzima inapatikana hapa: https://mkito.com/artist-profile/otuck-william/964 Krismasi hii, Santa hatokuwa akitoa zawadi peke yake. Na hata hivyo inaonekana kuwa baadhi watamzidi katika hilo linapokuja suala la muziki! Otuck William, muimbaji wa soul, athibitisha hilo kwa kuleta mbele yako bidhaa mpya itakayobadili sura nzima ya msimu wa Krismas mwaka huu kimuziki. Ni santuri itakayokuwa imebeba nyimbo kumi na tano (15) mahususi kabisa kwa ajili ya Krismas. Akizungumzia album hiyo Otuck anasema; "“Zawadi Ya Krismasi” ni album yenye nyimbo 15 iliyotayarishwa kwa ushirikiano wa kwangu mwenyewe na Nach B, mtayarishaji kutoka studio za Beats Bank Music zilizopo jijini Mbeya. Hii si album ya dini (Gospel) japokuwa imebeba baadhi ya nyimbo za zamani za kidini za Krismas, ambazo tumezitayarisha katika mahadhi tofauti kidogo, lakini ni album inayohusu Familia, Matumaini, Faraja, Imani na Upendo. Kwa kadri ya ufahamu wangu inaweza kuwa album ya kwanza kabisa ya Krismas kuwahi kutengenezwa Tanzania au Afrika Ya Mashariki kwa ujumla”. Ni wazi kwamba kila mtu anatamani kujua nini hasa Otuck ametuandalia, kitakachodumu kwa muda mrefu na kutufariji kila ifikapo msimu kama huu. Album hiyo itakuwa ikipatikana katika mtandao wa Mkito.com kuanzia Tar 26 Novemba 2014. Lakini pia itauzwa katika mfumo wa CD. Kwa mawasiliano zaidi ya namna ya kupata CD hizo au kuwa wakala wa usambazaji, andika barua pepe kwa otuckwilliam@gmail.com au piga simu nambari +255712168011
ANGEL BENARD - UFUNDISHE MOYO ( New Audio )
ANGEL BENARD - UFUNDISHE MOYO WIMBO WA 6 WIKI YA 6 KATI YA NYIMBO 10 ZINAZOTARAJIWA TOKA KWA WIKI 10 MFULULIZO. "Ni sala ambayo ninamuomba Mungu anifundishe kumuabudu katika roho ya kweli, na siyo tu nikiwa katika shida au ninapohitaji msaada fulani."
Wednesday, November 26, 2014
LAMECK DITTO - HERI YA CHRISTMAS ( New Audio )
Msimu wa Christmas ndiyo unatufikia sasa na wimbo wa kwanza wa Christmas ndiyo huu hapa kutoka kwa Ditto. Ditto ambaye ameandika nyimbo nyingi ambazo ni hits kubwa katika muziki wa Tanzania pia ni mwimbaji na mwalimu wa muziki Tanzania House of Talent.
NAVY KENZO - MOYONI ( New Audio )
Wimbo mpya kutoka kwa Navy Kenzo unaitwa MOYONI na unatoka kwenye album mpya ya NIROGE. Wimbo unaongelea wapenzi wawili ambao wanataka kuchukua hatua nyingine kubwa katika uhusiano wao. Wimbo umekuwa produced na Nahreel mwenyewe.
QUICK ROCKA FT YOUNG DEE - BISHOO ( New Audio )
Wimbo mpya kabisa kutoka kwa bingwa wa tongue twister. QUICK ROCKA anakuletea BISHOO ambao ni wimbo amemshirikisha Young Dee.